Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrimdoko akizungumnza na waandishi wa habari ofisini kwake |
Mkoa wa Katavi
wameandaa maadhimisho ya wiki ya mwana Katavi kwa muda wa siku saba
zitakazomsaidia mwananchi wa Mkoa wa Katavi na Wanzania kwa
ujumla kuweza kujifunza mbinu mbalimbali za kisasa za
kuhusu sekta mbalimbali na kutangaza vivutio vya utalii
vilivyopo katika Mkoa wa Katavi .
Mkoa wa Katavi wameandaa maadhimisho ya wiki ya mwana Katavi kwa muda wa siku saba zitakazomsaidia mwananchi wa Mkoa wa Katavi na Wanzania kwa ujumla kuweza kujifunza mbinu mbalimbali za kisasa za kuhusu sekta mbalimbali na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika Mkoa wa Katavi .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Mwanamvua Mrindoko amesema Mkoa wa Katavi umeaandaa wiki
maarufu inayojulikana mwana Katavi ukiwa ni utaratibu
huo ambao utumika kwenye siku ya wiki hiyo kumwelimisha mwananchi
wa Mkoa wa Katavi na Watanzania kuhusiana na mambo mbalimbali .
Wiki hiyo
itaanza Oktoba 25 hadi Oktoba utaaribibu huu ulionzishwa na Mkoa wa
Katavi ambayo ndani ya wiki nzima kutakuwa na
shughuli mbalimbali zitakazo kusaidia wananchi kwenye mambo
mbalimbali lengo kwa kujifunza maswala ya sekta mbalimbali na
kutangaza utalii.
Alizitaja baadhi ya sekta
hizo kuwa ni kilimo ,ufugaji uvuvi ,uwekezaji ,madini
michezo na sekta inayohusiana na utalii wa vivutio vyote vya utalii
vilivyopo katika Mkoa wa Katavi baadhi ya vivutio hivyo ni
Hifadhi ya Taifa ya Katavi maporoko ya maji Nkondwe,
chem chem ya maji moto ,Mto mapacha andaki
lililotumiwa na Wabeligiji wakati wa vita vya Dunia
Mrindoko
alisema kauli mbiu ya wiki hiyo ni
inasema Katavi yetu talii wekeza imalisha uchumi kwa
maendeleo endelevu na wataendelee na kauli mbiu hiyo muda wote wa wiki
hiyo ili kuwahamasisha wananchi kuendelea kujishughulisha na
shughuli za kiuchumi kwa kuleta maendeleo endelevu .
amefafanua kuwa kila siku
kutakuwa na sekta kadhaa zinazohusika na tukio la siku ambapo
zitapewa kipaumbele katika kueleza shughuli zake
na kueleza tekinojia mbalimbali zinazotumika katika uzalishaji wa
biashara ,ujasiliamali utalii
na nyinginezo .
amesema
Halmashauri zote zimejiandaa kushiriki kwenye wiki hiyo kwa
kushiriki kikamilifu na zimepanga kuleta wananchi wengi zaidi
kutokana na hamsa kubwa ambayo imefanywa hadi sasa.
Mwaka 2022 walifanya kwa
mara ya kwanza na waliweza kupata mafanikio kwa kushilikisha wananchi na
wadau pamoja na taasisi za kifedha . na wananchi walishiriki kwa
wingi na kuweza kujifunza kwa kupatiwa elimu mbalimbali .
Nae Mkazi wa
Manispaa ya Mpanda John Sanane amesema kufanyika kwa wiki hiyo ni furusa kubwa
kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi na Wanzania kwa ujumla kwa kuweza kufahamu
furusa zilizopo katika Mkoa huu.
Pia ni nafasi kwa Mkoa
kuweza kutangaza vivutio vyake kwani licha ya kuwa na vivutio vingi ndani ya
Mkoa huu bado havija fahamika vya kutosha hivyo wiki hiyo
ndio wakati wa kutangaza zaidi .