Mkuu wa wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,Majid Mwanga akiwa na baadhi ya maofisa wa TAWA kwenye ukaguzi wa mazingira. |
Na. Kibada Ernest –Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino.
MKUU wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga amewataka wananchi waliovamia misitu ya
hifadhi na kukata miti hivyo kuacha mara moja na kuondoka na iwapo watakaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yao.
MKUU wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga amewataka wananchi waliovamia misitu ya hifadhi na kukata miti hivyo kuacha mara moja na kuondoka na iwapo watakaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Kauli hiyo imetolewa jana oktoba 20 na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga baada ya kufanya ziara ya kushitukiza na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya kutembelea na kujionea halisi ya uharibifu uliofanyika katika maeneo hayo,
Hivyo ikamlazimu kupiga marufuku uharibifu unaofanywa wa kukata miti hovyo na
kuwaagiza wakala wa huduma za mistu TFS kuhakikisha mistu inalindwa na mtu
yeyote anayetaka kukata miti lazima awe na kibali na afuate utaratibu.
Aidha amewataka Wananchi wa Wilaya hiyo wakiwemo wageni kutoka maeneo mengine nchini kuwa mabalozi ili kutokomeza uvamizi wa misitu ambayo iko hatarini kutoweka kutokana na shughuli za kilimo, ufugaji,kukata miti na uchomaji wa moto kiholela hali ambayo inatishia kuteketea kwa mistu huo.
Mkuu wa wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,Majid Mwanga akiendelea na ukaguzi wa mazingira yaliyoharibiwa baada ya kuvamiwa na baadhi ya wananchi.
Majid ameeleza kuwa uvamizi huo umesababisha baadhi ya mistu kuteketea hali ambayo inatishia kukauka kwa vyanzo vya maji na katika wilaya hiyo.
Katika hatua nyingine ameiagiza Wakala wa Huduma za Mistu,Tanzania TFS Katika wilaya hiyo kuhakikisha wanashirikiana
na Idara vyombo vingine pamoja na Idara ya Usimamizi wanyamapori TAWA na wananchi ili kunusuru misitu hiyo ambayo
iko hatarini kutoweka kutokana na uvamizi huo unaofanyika kutokana na shughuli
za kibinadamu.
“Hii mistu inatakiwa ihifadhiwe, hii mistu ndio uhai ikihifadhiwa vizuri inasaidia vyanzo vyetu vya maji”alisema Mkuu wa Wilaya.
Baadhi ya nyumba za asili zilizojengwa kwenye maeneo mbalimbali ya uhifadhi na kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira. |
Mkuu huyo wa Wilaya Mwanga amesema watu wanakata miti bila mpangilio na amejionea mwenyewe watu wanakata miti hovyo kwa shughuli zao kwa kujipatia kipato bila kuzingatia utaratibu .
Kwa sasa Suala la uhifadhi lazima TFS mhakikishe ninyi pamoja na vijiji
vinavyozunguuka mistu ya hifadhi mzungumze lugha moja wote muwe kitu kimoja ili
kuhifadhi mistu hii..
Amepiga marufuku wananchi wa wilaya hiyokukata miti bila kuwa na kibali "Hakuna kukata miti bila kibali hata kama mti ni wa kwako uliupanda wewe au uko kwenye shamba lako, lazima hatua zote zifanyike kuanzia ngazi ya kijiji na hata ukikata mti mmoja lazima upate kibali".