KATIBU MKUU CCM IMANI ZA KISHIRIKINA NI UMASIKINI.

 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi [CCM]  Taifa Daniel Chongolo akiwasili katika mkoa wa Katavi kwaajili ya ziara ya kugagua uhai wa Chama na utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi katika mkoa wa Katavi

George Mwigulu na Paul Mathias,Katavi

Wananchi wa mkoa wa Katavi wameombwa  kuacha kuwapa nguvu na fursa watu wanaodhaniwa  kuwa na uwezo wa kufichua wachawi maarufu kwa jina la Kamchape au lambalamba kwani wanafanya mambo yanayokiuka sheria za nchi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi [CCM] Taifa Daniel Chongolo akivishwa Sikafu ya ukaribisho alipofika katika viunga vya Ofisi ya Chama cha Mapinduzi [CCM] Mkoa wa Katavi

Wananchi wa mkoa wa Katavi wameobwa  kuacha kuwapa nguvu na fursa watu wanaodhaniwa  kuwa na uwezo wa kufichua wachawi maarufu kwa jina la Kamchape au lambalamba kwani wanafanya mambo yanayokiuka sheria za nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo baada ya kupokea taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko katika ofisi ya Mkoa ya Chama hicho ambapo Mrindoko alisema kuwa kitendo hicho kiliweza kuhatarisha amani na usalama wa mkoa hususani katika mwambao wa ziwa Tanganyika.

Chongolo alisema kuwa imani za kishirikina ni umasikini na kama jamii inapaswa kujifunza ni kuagalia kwa watu wengi wanaoamini katika ushirikina kwani wanaami kwenye ndoto ambazo kutekelezeka kwake ni ngumu “Achaneni kuendekeza mambo yanayoweza kutoa taswira ya umasikini kwa mkoa wetu amesisitiza.

Amesema kuwa Mkoa wa Katavi ni mkubwa ambao  umejenga historia kubwa kwa kuwa na watu wasomi kama Mhadisi Azaki Kamwele  ambaye ni mtumishi wa serikali kwa miaka mingi sambamba na Mh Mizengo Pinda Waziri Mkuu Msitaafu,Iddi Kimata Mkuu wa Mkoa Msitaafu na Mkoa wa watu wazito kwenye nchi hii hauwezi hadi leo ukawa unaendekeza ushirikina kama daraja la kufanikiwa kimaisha.

Katibu Mkuu huyo amesema ni lazima mkoa utoke kwenye kufikiri mambo kwa njia rahisi kwa sababu maendeleo hayapatikani nduba,kupuliza,kupiga lamli na kutengeneza mambo lahisi kwenye mambo yanayohitaji kufuata utaratibu.

Ukiona watu wa namna hiyo wala usipate shida angalia wanaishi kwa masharti mtu anaweza kuwa nang”mbe 1000 lakini kwake haruhusiwi kula nyama nusu kilo kwa wiki sababu masharti yanayotolewa na watu wanaopenda kupulizapuliza…achaneni na maisha hayo kwani niafadhari uwe na ng’ombe 10 uwe na uhuru wa kula nyama Amesema  Katibu Mkuu huyo.

Amesisitiza kuwa Mila potofu zinawagombanisha,zinawatenganisha na zinawatengenezea uadui usio na maana na zinawakwamisha kwenye shughuli za maendeleo….akija mtu hapa akapiga na kamchape yake akawaambia ukilima shamba hili hutavuna mwaka huu unaacha kwa sababu unaamini alichosema je yeye ni Mungu?,yeye ni mvua?,yeye ni ardhi?na yeye ni mbegu?.” Alihoji Chongolo ambapo wananchi walijibu kwa kukataa kuwa sio Mungu.

Aidha katika hatua nyingine Chongolo amewaletea salama za rais Samia Suhulu Hassain ambapo alisema atanabua matatizo ya watu wa Mkoa wa Katavi na kama chama wanakazi kubwa ya kusimamia ilani ya chama hicho ili kuweza kuondoa changamoto hizo.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Daniel Chongolo yupo kwenye ziara ya siku 5 katika Mkoa wa Katavi ambapo atakangua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo sambamba na kuangalia uhai wa chama hicho.

Zuena Rashidi,Mwananchi na mkazi wa mtaa wa Kawajese ameshukuru ujio wa katibu mkuu huyo kwani anaamini kuwa utakuwa sehemu ya kusikiliza kero za wananchi na kufanyiwa kazi kwa muda muafaka.

Amesema kuwa CCM ilipewa dhamana ya kuongoza serikali hivyo wanapaswa kuwajibika kwa kutatua kero ambazo zimekuwa kikwazo kwa usitawi wa uchumi.

Jumanne Magaga anasema kuwa mkoa wa Katavi unachangamoto nyingi hususani ya migogoro ya mashaba,mipaka kati ya wananchi na hifadhi mbalimbali zilizopo mkoani Katavi ambapo kama Katibu Mkuu huyo ataweza kuzishughulikia wataweza kuishi kwa amani.

Mwananchi huyo ameeleza kuwa Katibu Mkuu anapaswa kuwaonya watendaji wa serikali ambao wamekuwa kikwazo cha wananchi kwenye kufanikisha maendeleo yao kwa kuwa wabadhirifu na wapenda rushwa.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages