![]() |
Stella Paul,Mkazi wa mtaa wa Misukumilo akiendelea na kazi yake ambayo humpatia kipato cha fedha za kujikimu. |
Na George Mwigulu,
Katavi.
BAADHI ya wanawake wajasiliamali wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameiomba serikali kuharakisha mchakato wa mfumo mpya wa utoaji wa mikopo kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kuendelea kukuza biashara zao zitakazo chochea ukuaji wa uchumi na maendeleo.
![]() |
Marry Daniel akiendelea na majukumu yake ya kazi . |
Serikali kwa muda wa mrefu sasa imesitisha zoezi la utoaji wa mikopo hiyo kupitia halmashauri zote nchini ambazo hutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili kukopesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu baada ya kubaini ubadhirifu na wizi wa fedha hizo huku baadhi ya wakopaji wengine kushindwa kurejesha mikopo hivyo serikali kuwa kwenye mchakato wa kutumia mfumo mpya unaotajwa kuwa ni kibenki.
Wakizungumza
kwa wakati tofauti 8, October 2023 baadhi ya wanawake hao katika mitaa ya
Misukumilo, Kawajense na Tulieni Manispaa ya Mpanda wamesema wamekuwa wahanga wa
kukosa mikopo ambayo iliwasaidia kukuza biashara zao na kuinua uchumi wa
familia.
Christina
Michael, Mjasiliamali na mkazi wa mtaa wa Tuleni Manispaa ya Mpanda anasema
kuwa serikali kupitia ofisi ya Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa fedha za serikali wahusika wote wa wizi wa fedha za mikopo walitajwa
hivyo anashangaa kuona bado wanamaisha mazuri ili hali wao bado wanahangaika na
umasikini.
Mjasiliamali huyo ameeleza kuwa fedha za mkopo walizokuwa wakipata ziliinua zaidi pato la kila siku na kuinua maisha yao kwa ujumla “Tuliweza kusomesha watoto wetu, kugharamia matibabu, mavazi na kuboresha makazi yetu” amesema Christina.
![]() |
Nyumba ya Marry Daniel Mkazi wa Mtaa wa Misukumilo ambayo ameijenga kutokana na kazi yake ni kutengeneza kokoto ambazo zinatumika kwenye ujenzi. |
Suzana
Paul, Mkazi wa mtaa wa Kawajese anasema licha ya nia ya serikali kuwa ni njema
ya kusitisha mikopo lakini imegeuka kuwa kero kwa sababu hawana sehemu nyingine
ya kukopa fedha kwa riba nafuu.
Amesema
uendeshaji wa biashara zao umekuwa mgumu huku hali ya maisha ikiendelea
kudidimia hivyo kuiomba serikali kuharakisha mchakato wa kurudisha huduma ya
utoaji wa mikopo.
Marry
Daniel, Mkazi wa mtaa wa Misukumilo mjasiliamali na mama wa watoto wanne
amesema kuwa wanawake wengi wegeukia shughuli za kugonga mawe ya kutengeza
kokoto zinazotumiwa kwenye ujenzi mbalimbali ili mradi waweze kuongeza kipato
chao.
Ameeleza
kuwa baada ya kutelekezwa na mume wake hakuwa na namna nyingine ya kufanya
zaidi ya kujinga na wanawake wengine ambao kazi yao ni kutengeneza kokoto.
“Ndoo moja ya
lita 10 yenye ujazo wa kokoto ni Tshs 500 tuko hapa na kikundi chetu kinaitwa HAPA KAZI TU hali sio nzuri kwa sababu
wengi wetu hapa hatuna waume ambao tunaweza kusaidizana kufanya majukumu ya
kuhudumia familia” Amesema
Marry ambapo amesisitiza kama mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu
itarejeshwa kwa wakati itawasaidia.
Stella Paul, Mwanakikundi wa HAPA KAZI TU amesema kuwa licha ya changamoto za kifedha na kuhudumia familia anazopata lakini kazi yake ya kutengeneza kokoto kwa kushirikiana na mume wake ameweza kujenga nyumba na kuvuta umeme.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumzia suala la mikapo wakati wa
ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo katika
kikao cha ndani amesema kuwa serikali bado inampango wa kuendelea kutoa mikopo
hiyo bali bado wanasubiria utaratibu mpya wa utoaji wa mikopo hiyo.
Mrindoko amewaomba wajasiliamali mbalimbali kuwa na uvumilivu wakati utaribu mpya unatengenezwa kwani serikali inatambua umuhimu mkubwa mikopo hiyo ambayo ni chachu kubwa ya maendeleo kwa makundi hayo.