MKURUGENZI SOZINESS AHIMIZA LISHE BORA KIGOMA NA KATAVI KUEPUKA UDUMAVU

 

Mkurugenzi wa Neo Life Mkoa wa Kigoma,Soziness Gernasoni akielezea uhumuhimu wa lishe bora.

Na George Mwigulu, Kigoma.

WANANCHI wa Mkoa wa Kigoma na Katavi wameaswa kuzingatia matumizi ya mlo kamili wa chakula kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa mengi yanayosababishwa na mtindo wa maisha ambao unahatarisha maisha yao.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya afya ya mwaka 2021/22 hadi 2025/26 kwa Mkoa wa Kigoma ni asilimia 42.3 na Katavi asilimia 33.7 unaonesha kiwango cha udumavu miongoni mwa watoto wa umri wa miaka 0 hadi mienzi 59 jambo ambalo linahitaji juhudi za ziada kukabiliana nalo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Neo Life   Mkoa wa Kigoma, Soziness Gervasoni amesema hayo jana wakati wa kongamano la kuhamaisha lishe bora  ambalo limefanyika ukumbi wa NHC Mtaa wa Lumumba Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani hapo ambapo ameeleza kama taasisi wanawajibu wa kuisadia serikali kutoa elimu ya mlo kamili wa chakula ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Soziness amesema jamii kwa sasa inakabiliwa na magonjwa mengi kwa sababu ya mwenendo mbovu wa maisha ya mazoea ya watu ya kutokujali lishe bora “zamani watu walikuwa wanaweza kuishi maisha mazuri ya afya ni kutokana walizingatia chakula cha asili lakini kwa sasa tumakubwa na magonjwa mengi  kwa uzembe ambao jamii inapaswa kuamka na kuchukua hatua ya matumizi ya lishe”

Mkurugenzi huyo amesema kwa mujibu wa Shirika la afya duniani (WHO),utapiamlo unamaanisha kuna upungufu au usawa katika ulaji wa mtu na virutubisho ambapo kuna makundi mawili ya utapiamlo ambao ni,kudumaa,upungufu wa uzito na virutubisho pamoja na utapiamlo ambao unatokana na virutubisho vingi ambavyo vinaweza kusababisha unene kupita kiasi.

“ viashiria  vya utapiamlo ni watoto kuonesha ukosefu wa ukuaji na wanachoka na kukasirika,maendeleo ya tabia na akili pia huwa polepole ikiwezekana kusababisha ugumu wa kujifunza” amesema dalili hizo pamoja na madhara mengi ya utapiamlo yanaweza kutokea ambapo aliwaomba kwenye katika vituo vya afya kwa uchunguzi wa mwili na wataulizwa juu ya aina na kiwango cha chakula wanachokula watoto.

Amesema kuwa suala magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa lishe bora hayawezi kuwapata sio pekee watoto bali kuna athari nyingi zinaweza kuwapata watu wazima na wazee kwa kupoteza uzito bila kukusudia,kupoteza nguvu na udhaifu wa misuli,uchovu,upungufu wa damu,shida za kumbukumbu na mfumo dhaifu wa kinga.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya lishe wakiwa katika ukumbi wa NHC Manispaa ya Kigoma Ujiji .

Licha ya changamoto kubwa za lishe alisema Taasisi ya Neo Life inafanya kazi ya utoa elimu ya matumizi ya lishe bora kupitia mwongozo wa wizara ya afya na WHO wa kuhakikisha kila mtu anatumia vyakula vya aina tano kwa siku ambavyo ni mafuta na sukari kwa asilimia 10, Protine asilimia 20, mbogambonga na matunda kwa asilimia 30 na asimilia 40 nafaka kamili.

Soziness amesisitiza watu kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 pamoja na kupata muda wa kupumzika kwa kulala usingizi kwa saa nane bila kushituka.

Amefafanua kuwa katika maendeleo ya sayansi na teknolojia Taasisi ya Neo Life kutokana na wakati mwingine kuwa na ugumu wa upatikanaji wa vyakula ikiwa ni juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa taasisi hiyo inatoa chakula cha lishe bora Pro Vitality ambayo utunza afya na kukabiliana na magonjwa ya mtindo wa maisha.

Julius Paul,Mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji na mshiriki wa mafunzo ya lishe amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuacha tabia ya kula chakula bila kujali lishe bora kwa sababu wamechoshwa na kutumia gharama kubwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Amesema elimu hiyo inapaswa kutolewa hadi ngazi za chini ambako kuna wananchi wengi ambao hawana elimu juu lishe bora huku bado chakula chao ni cha mazoea.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages