![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwananvua Mrindoko akiongea na wadau wa Kilimo cha Zao la Pamba. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi
Wadau wakilimo cha zao la Pamba katika
mkoa wa katavi wameobwa kwendakusimamia kwa vitendo uzalishaji wa Zao la Pamba
kwa Msimu Ujao 2023/2024 ili kuendana na Uwezo wa Kiwanda cha kuchakata zao la
Pamba cha NGS kilichopo mkoani katavi.
![]() |
Wadau mbalimbali wa zao la Pamba wakiwa katika kikao cha wadau wa zao la Pamba mkoa wa Katavi |
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa
Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko wakati akifungua kikao kazi cha Wadau wa
Kilimo cha Pamba Mkoa wa Katavi.
Amesema kuwa kiwanda hicho kinauwezo wa kuchakata Milioni 50 za Pamba kwa msimu mmoja huku uzalishaji wa Mkoa ukiwa ni Milioni 7 kwa Msimu 2022/2023 ameeleza kuwa pamoja na ongezeko lililopo bado uzalishaji huo hauna tija kutokana na mahitaji ya Kiwanda.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kwa msimu ujao wa 2023/2024 mkoa wa katavi unatalajia kuzalisha Kilo milioni 20 ambazo zitagawiwa kunzia ngazi ya Halmshauri hadi kata ili kufikia malengo hayo.
Katika hatua nyingine amesisitiza uzalishaji wa
pamba kwa msimu uliopitahaulingani
na mbegu ambazo walichukua wakulima kilo
8,772,100 mbegu hizo ukizichanganua
zilikuwa na uwezo wa kupandwa kwenye ekari 43, 605,000 ambazo zilikuwa na uwezo wa kuzalisha kilo 17,442 000 lakini uzalishaji umekuwa ni
kilo 7,649,410hali ambayo inaonyesha
kuna upunguzu wa kilo zilizozalishwa na idadi ya mbegu walizosambaziwa
wakulima.
Mrindoko amesistiza kuwa kwa msimu huu Amcos na wataalamu wa kilimo wahakikishe idadi ya
kiko za mbegu ziendanane na lengo
la uzalishaji na wala si vinginevyo
kwani Mkoa wa Katavi bado
unapokea mvua zuri zinazofanya mazao
yaweze kusitawi bila shida hivyo kila
mmoja atambue kuwa malengo ya uzalishaji kwa msimu huu ni kilo milioni 20 kwa
Mkoa wa Katavi na kwa msimu ujao uzalishaji uongezeke na kufikia kilo milioni
40.
Amewaagiza wakuu wa Wilaya wote wa wilaya za Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanafatilia kwa karibu usambazaji wa mbegu za pamba ili kuweza kudhibiti upotevu ili kuhakikisha mbegu zinazokuwa zimetolewa zote zina kwenda shambani .
Mkurugenzi wa kIwanda
cha kuchakata pamba cha NGS
Njalu Silanga aliwatowa hofu wakulima kuwa NGS wataendelea kuwalipa wakulima wa pamba kwa wakati ili
kuweza kufikia malengo ya uzalishaji .
Aliomba tafiti ziendelee kufanyika kwani yeye alivyozunguka kwenye vijiji mbalimbali vya Mkoa wa Katavi hajaona kama mkulima wa pamba anaitaji alime kwa kutumia mbole ekumbukwe kila gharama inayoongezeka inapelekwa kwa mkulima hivyo wataalamu wetu waendelee kufanya tafiti ili wajuwe ni maeneo yapi yanayohitaji mbolea .
Nae Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Neemia James ameshukuru Bodi ya Pamba namna ambavyoinashirikiana na Mkoa wa Katavi katika kuzalisha tija ya uzalishaji wa zao la Pamba