Mkuu wa Mkoa wa Katavi mwanamvua mrindoko amewaonya watendaji wa zembe katika ngazi Kata,Mitaa na Maafisa Tarafa kufanya Kazi Kwa uwajibikaji Kwa kutatua keto za Wananchi kwenye maeneo wanayoyasimamia.
Baadhi ya Watendaji wa Kata,Mitaa na Maafisa Tarafa wakiwa katika kikao kazi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko |
Mrindoko ameyasema hayo alipokutana
na watendaji hao katika kikao Kazi Cha kukumbushana wajibu na Majukumu yao ya
Kila siku katika kuisadia serikali
kiutendaji.
Amesema kuwa watendaji wa mitaa na Kata pamoja na Maafisa Tarafa ndiyo mboni ya serikali katika ngazi ya Kata Kwa kuwahudumie wananchi kwa vitendo kwa kutatua kero za wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph[kushoto] Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli[kulia] wakiwa katika kikao hicho. |
"Unakuta mtendaji hasomi Mapato na Matumizi Kwa wananchi hali ambayo huichonganisha serikali na wananchi tukasome Mapato na Matumizi na kufanya mikutano ya hadhara kwa wananchi sikilizeni kero zao na kuzitatua tuna ile program ya tuzungumze live huko nako tusikie mnapokea kero za wananchi"amesema mrindoko.
Kuhusu miradi ya maendeleo amewaagiza watendaji hao kutembelea miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao na kuisemea Kwa wananchi juu ya umuhimu wa miradi hiyo Kwa wananchi kwenye maeneo yao.
"Serikali ya Rais DK Samia imeleta fedha nyingi sana za miradi ya maendeleo kwenye Kata zetu huko isemeeni miradi hii na Kuitembelea kuna wengine hapa mradi upo eneo Karibu kabisa ila Hana muda wa Kuitembelea mradi huo tutembelee miradi siku tukija huko sisi ukaonekana hujui chochote kuhusu mradi husika hatuta kuacha salama "amenena Mrindoko.
Katika kuelekea msimu wa Masika
amewaagiza watendaji hao kwenda kusimamia suala la usafi wa Mazingira ili
kuepuka Magojwa yanayotokana na uchafu wa mazingira.
"Hili la usafi tutakuwa wakali sana tukikuta eneo lako Afisa Mtendaji ni chafu utasafisha wewe tunataka mji wetu uwe safi kasimamieni sana usafi wa Mazingira tunaelekea Msimu wa Masika tunataka mazingira yawe safi" anasema Mrindoko.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kwenda kusimamia ulinzi na usalama kwenye Kata zao kwa vitendo Ili kudhibiti matendo ya uharifu yanayojotokeza kwenye baadhi ya Mitaa na Kata.
"Kwenye Kata yako wewe mtendaji
unakuta Kuna Vikundi vya uharifu kama hivi vya Damu chafu na wewe upo na
hujachukua hatua yeyote fahamu kabisa hufiti kuwa hapo jiulize umefanyanini
kusaidia ulinzi na usalama uwepo kwenya Kata yako au mtaa wako" ameeleza
Mrindoko.
Kikao hicho baina ya Watendaji wa Mitaa, Kata na Maafisa Tarafa umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya manispaaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambapo mambo kadhaa wa kadhaa yamejadiliwa yakiwa na lengo la kuongeza uwajibikaji katika Majukumu ya kuwatumikia wananchi Kwa watendaji hao kwenye Kata na mitaa yao.