Na Walter Mguluchuma,Katavi.
Benki ya NMB Mkoa wa Katavi imewakutanisha wafanyabiashara mbalimbali na kuwapatia Elimu juu ya Fursa mbalimbali za mikopo zinazotolewa na Benki hiyo kupitia NMB BUSINESS CLUB ambayo imekuwa kiunganishi kwa wafanya Biashara hao.
Baadhi ya Wafanyabiashara Mkoa wa Katavi wakiwa katika Semina hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Mpanda Social Hall[Picha na Paul Mathias] |
Benki ya NMB Mkoa wa Katavi imewakutanisha wafanyabiashara mbalimbali na kuwapatia Elimu juu ya Fursa mbalimbali za mikopo zinazotolewa na Benki hiyo kupitia NMB BUSINESS CLUB ambayo imekuwa kiunganishi kwa wafanya Biashara hao.
Mafunzo hayo ya siku moja yaliowashirikisha wafanya
biashara mbalimbali wakiwemo na wadau mbalimbali kama vile
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msajiri wa hati Ofisi ya biashara
Manispaa ya Mpanda na wadau wengine mbalimbali yalifanyika
katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda .
Kaimu Meneja wa Benki ya NMB
Kanda ya Magharibi Gadiel Sawe amesema
lengo la kuwakutanisha wafanya biashara hao ni kuwapatia
elimu itakayowasaidia kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi ili kuwawezesha kujua huduma zinazotolewa kwenye ofisi
mbalimbali wanazofanya shughuli zinazohusiana na biashara zao
.
Mwenyekiti wa NMB BUSNES CLUB Mkoa wa Katavi Raymond Kamtoni[kushoto] akiongea Jambo na Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Gadiel Sawe wakati wa Semina Hiyo. [Picha na Paul Mathias] |
Sawe amebainisha kuwa watu waliowalenga
kuwapatia elimu hiyo ni wafanya biashara wote kuanzia wamachinga
wafanya biashara waliwaacha ni wafanya biashara wale wakubwa ambao
wao nao huwa wanautaratibu wa kuwapatia elimu bila
kuwachanganya na wafanya biashara hao .
Makamu Mwenyekiti wa NMB
Business Club wa Mkoa wa Katavi Haidari Sumry amesema wao kamawafanya biashara wanaofanya biashara na NMB
kumekuwa na manufaa makubwa sana toka NMB Business Club
toka ilipoanzishwa katika Mkoa wa Katavi .
Makamu Mwenyekiti wa NMB BUSNES CLUB Mkoa wa Katavi,Haidary Sumry akielezea namna Benki ya NMB ambavyo imekuwa ikiwasaidia kwenye Biashara. |
Hivyo kwa maana ya kufanikiwa wafanya biashara
wamefanikiwa pakubwa na NMB nao
wamefanikiwa kwa kuweza kupanua wigo kwa kuendelea kupata watu
ambao wanajiunga kwenye Benki yao kwa kuendelea kupata watu
wanaoendelea kupata mikopo NMB na benki hiyo kuendelea
kuwa benki inayochochea maendeleo ya Mkoa wa Katavi .
Sumry amesema Nmb kwa sasa ni Benki
kubwa hapa nchini hivyo wajione kuwa wamekuwa wakubwa wanachowaomba waangalie ni vivutio gani ambavyo vinavyowasaidia wafanya biashara
hivyo wanachoomba wafanya biashara kwa kuangalia namna ya kupunguza liba
.
Sasa hivi wafanya biashara wameisha elimika kwa kulipa madeni bila hata ya kupigiwa simu wanajua kila mwisho wa mwezi kurejesha mikopo waone kwa kuwa kumekuwa na usalama huo wa marejesho yao kwa hari NMB waone nao namna ya kupunguza liba.
Nae mfanyabiashara Issa Idd Kapiligi
duka la rejareja na wakala wa NMB alisema wameudhuria mafunzo
hayo ambayo hufanyika kila mwaka kwa wafanyabiashara wanao
kopa NMB yanayowasaidia namna ya kufanya biashara na
kuendesha kwa ufanisi mkubwa ,
Kwenye mafunzo hayo wamejifuna mfumo mpya wa TAUSI wa kuomba leseni kwa njia ya mtandao elimu hiyo kwao imekuwa ni mpya na wameifahamu na pia wamefundishwa jinsi ya kupata hati za umiliki wa ardhimafunzo hayo yamewanufaisha .