ACT WAZALENDO YAPATA SAFU MPYA YA UONGOZI MPANDA .

 

Viongozi wa chama cha ACT wazalendo wakiwa katika mkutano huo


Na Jackson Gerald,Katavi

Chama cha ACT   Wazalendo  Jimbo la Mpanda Mjini  wamezidi kujiimarisha  kwa kuweza  kufanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi watakao kiongoza  chama hicho kwa kipindi cha  miaka mitano  ikiwa ni hatua ya kuendelea kujiimalisha  

Chama cha ACT   Wazalendo  Jimbo la Mpanda Mjini  wamezidi kujiimarisha  kwa kuweza  kufanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi watakao kiongoza  chama hicho kwa kipindi cha  miaka mitano  ikiwa ni hatua ya kuendelea kujimalisha  

Uchaguzi huo wa kuwapata viongozi wa chama  hicho  katika jimbo la  Mpanda Mjini  ulifanyika katika ukumbi wa Kanisa  Katoliki Jimbo la  Mpanda na ulisimiwa na Amon  Simbabhaje  kutoka   ACT Wazalendo   Taifa na  na uliwashirikisha wajumbe wa mkutano  Mkuu  kutoka Kata zote  zinazounda Jimbo la Mpanda  Mjini .

Vingozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho ni  Anselimo  Majani  amechaguliwa kuwa  Mwenyekiti , Cyril Mshota  Mshota Katibu  , Juma  Bileta  Katibu  Mwenezi , Donatha  Petro Mweka  Hazina  Feisal  Hassan  Mipango na Uchaguzi , Juma  Sanda  Mwenyekiti  Ngome  ya Wazee , Anna  Paulo  Nyani  Mwenyekiti  Ngome wanawake  Abdalla  Kang;ombe  Mwenyekiti   Ngome  Vijana .

Wengine waliochaguliwa ni   Habibu  Bandya  Katibu  Ngome Wazee,  Specioza  Kambulaya  Katbu Ngome  Wanawake ,  John Mniko Katibu  Ngome  Vijana  Idd  Mvano  Mjumbe kamati ya uongozi  Abdul    Iddy  Nziguye  Mjumbe kamati ya uongozi  Fatuma  Masoud   mjumbe kamati ya uongozi


Akizuzungumza  kwa mara ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kwake  na wajumbe wa kikao hicho  Mwenyekiti wa Act Wazalendo Jimbo la Mpanda Mjini  Anselimo  Majani  alisema  anasimama mbele ya wajumbe wa kikao hicho akiwa na huraha  na akiangalia mbele  anaona mambo  mazito kwa sababu wanatengeneza shamba kwani sio kama vyama vingine ambavyo  unakuta kuna watu teyari hivyo wao wanakwenda kupambana .

A mewapongeza  wajumbe wote  wa kutoka kwenye  Kata zote  ambao wameweza kujitokeza kwa wingi na kushiriki kwenye mkutano huu   mkuu  muhimu wa  kuwachagua viongozi watakao kiongoza chama hicho .

 Katibu wa ACT   Wazalendo Joseph  Mona  amebainisha kuwa uchaguzi huu ni  muendelezo wa chaguzi  nyingine  ambapo kwa mujibu wa tataribu za chama hicho  uchaguzi kama huu utafanyika katika Majimbo yote yaliko katika Mkoa wa Katavi na kisha  utafanyika  uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa ngazi ya Mkoa.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages