DC: ''JAMILA WATENDAJI KATA SIMAMIENI VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI''

 

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akiwahutubia wajumbe wa kikao cha Kamati ya ushauri Wilaya ya Mpanda kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mpanda Social Hall.


Na Paul Mathias,Mpanda

Serikali katika wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imewaagiza watendaji wa Kata katika Wilaya ya Mpanda kusimamia ipasavyo uandikishaji wa Watoto wa awali na Darasa lakwanza ili waanze masomo yao Mapema mwakani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Ramadhani [kushoto] akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli wakiwa katika kikao hicho.

Serikali katika wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imewaagiza watendaji wa Kata katika Wilaya ya Mpanda kusimamia ipasavyo uandikishaji wa Watoto wa awali na Darasa lakwanza ili waanze masomo yao Mapema mwakani.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila yusuph ametoa maagizo katika kikao cha Kamati ya ushauri ya Wilaya ya Mpanda [DCC] kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mpanda Social Hall Mpanda Mjini.

Ameeleza kuwa uandikishaji wa wanafunzi wa awali na Darasa la Kwanza katika wilaya ya Mpanda haupo katika kiwango cha kuridhisha na kuwaagiza watendaji wa Kata na mitaa kwenda kusimamia zoezi hilo kwa kina ili ifikapo January watoto hao waanze darasa la awali na Darasa la kwanza.

’sasa hivi tunaendelea na zoezi la usajili wa wanafunzi wa Darasa la kwanza na Darasa la Awali usajili bado upo chini kwa Darasa la kwanza na Darasa la awali mkitoka hapa hasa watendaji wetu mhakikishe watoto wote wanao takiwa kuanza Darasa la awali na Darasa la awali wanasajiliwa kiongozi ambae hata wajibika kusimamia zoezi hili atatoa maelezo kwanini ameshidwa kusimamia zoezi hilo’’ amesema Jamimila Yusuph Mkuu wa wilaya ya Mpanda.

Amewaomba watendaji hao kutumia mikutano ya hadhara katika kata zao kutoa elimu kuhusu umuhimu wa wa wazazi kuona umihimu wa kuwasajili watoto wao kuanza darasa la kwanza na Darasa la Awali.

Katika hatua nyingine amewaomba watendaji hao kuendelea kushirikiana na wananchi katika zoezi la kuchangia chakula Shuleni ili wanafunzi wapate chakula Shuleni hali ambayo  husaidia ufaulu kwa watoto kwa kupatiwa chakula Shuleni.

Mkuu huyo wa wilaya amewaonya wananchi wanaovamia maeneo Mistu yaliyo hifadhiwa kisheria kutofanya Shuhguli za Kibinadamu katika maeneo hayo oevu ambayo ni hifadhi kwa mujibu wa Sheria.

‘’Msimamie wananchi wasilime maeneo yaliyohifadhiwa kwa mujibu wa Sheria tumeona Msitu wa Msaginya wananchi  bikoni ipo inaonekana watu wa TFS na viongozi wa serikali zetu za Vijiji walipita kuonyesha mipaka bado wananchi wanalima ndani ya hifadhi natoa elekezo kwa TFS ifanyike Doria ya kuwatoa watu wanaolima maeneo ya hifadhi’’ amesisitiza Jamila yusuph

Kuhusu suala la ulinzi na usalama Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ameagiza kila kata katika Wilaya ya Mpanda kuwa na vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuendelea kuzuia aina yeyote ya uhalifu inayoweza kujitokeza kutumia vikundi vya ulinzi shirikishi katika ngazi ya Kata.

Katika kikao hicho cha kamati ya Ushauri Wilaya ya Mpanda Viongozi wa Taasisi za serikali wamewasilisha taarifa za utendaji kazi wa Taasisi hizo kwa wajumbe wa kikao hicho na kujadiliwa lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kupitia taasisi hizo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages