KAMPUNI YA UNUNUZI WA TUMBAKU YA PREMIUM ACTIVE YATOA MADAWATI YA ZAIDI YA MILIONI 50

Meneaja Shughuli wa Premium Tanzania Nico Roussos wa[ pili kushoto] akimkabidhi Mfano wa hundi ya zaidi ya Milioni 50 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika katika hafla hiyo.


Na Walter Mguluchuma,Katavi

Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya PREMIUM ACTIVE Tanzania inayofanya kazi ya  kununua Tumbaku katika maeneo yanayolima Tumbaku katika Mkoa wa Katavi imetoa  msaaada wa zaidi ya shilingi milioni 50 kwa ajiri ya sekta ya elimu zitakazotumika  katika kutengenezea madawati kwa shule za Msingi na Sekondari .

Meneja Shughuli wa Kampuni ya Premium Tanzania Nico Roussos akielezea namna Kampuni hiyo imekuwa mdau wa Maendeleo katika mkoa wa Katavi.

Kampuni ya  ununuzi wa Tumbaku ya PREMIUM ACTIVE Tanzania inayofanya kazi ya  kununua Tumbaku katika maeneo  yanayolima Tumbaku katika Mkoa wa Katavi imetoa msaaada wa zaidi ya shilingi milioni 50 kwa ajiri ya sekta ya elimu zitakazotumika  katika kutengenezea madawati kwa shule za Msingi na Sekondari

Mfano wa  hundi wa fedha hizo imekabidhiwa n kwa  mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Onesmo  Busweru  ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika na imekabidhiwa kwa niaba ya kampuni ya Premium na  Meneja  shughuli wa  Kampuni hiyo Nico   Rousss kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika .

Akikabidhi  mfano wa hundi hiyo Meneja  shughuli wa Kampuni ya PREMIUM Nico Rousss  alisema  kampuni  hiyo  imetowa kiasi hicho  cha fedha ambazo zitagawiwa kwenye maeneo ya Kata zote zinazolima Tumbaku ikiwa ni  katika sehemu ya kuchangia maendeleo katika maeneo yote yanayolima Tumbaku  katika Mkoa wa Katavi .

Amebainisha kuwa  Kampuni hiyo licha ya kununua tumbaku  wao ni sehemu kubwa sana ya  wadau wa kuleta maendeleo katika Mkoa wa Katavi na ndio maana wameamua kutoa kiasi cha Tshs  50 300,000 katika sekta ya elumu kwa ajiri ya kutengeneza  madawati ya shule za Msingi na Sekondari .

Katika kufanikisha   mchango huu kwenye jamii Kampuni hiyo  ilipokea maombi ya miradi  ya kipaumbele kwenye kila Kata  yenye  vyama vya ushirika vya Msingi  vinavyofanya kazi na Kampuni ya PREMIUM   kwa  hari hiyo sio  rahisi kwa sasa kutimiza miradi hiyo  kwa wakati mmoja .

Amefafanua kuwa kwa sasa Kampuni ya PREMIUM  imweza kutowa kiasi hicho cha fedha kiasi cha Tshs  50,3000,000 ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi tshs 31,800,000 ni kwa ajiri ya Wilaya ya Tanganyika  Tshs  Wilaya ya Mpanda   tshs 11 ,250,000 na Wilaya ya Mlele Tshs 7,220,000 hivyo  kampuni hiyo wanayofuraha kubwa wa kuwa wadau waliorudisha faida yao kwenye maendeleo ya Jamii

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Onesmo Buswelu akiishukuru Kampuni ya Premium kwa Mchango ilioutoa kwa Mkoa wa Katavi.

Meneja  Uhusiano  na Usimamizi wa Kampuni ya Premium A ctive Yusuph   Mahundi amesema  kampuni hiyo inafanya kazi katika  maeneo yote ya Mkoa wa Katavi  kwa Wilaya ya  Tanganyika ndiko wanakofanya kazi katika sehemu kubwa  na  katika msimu wa kilimo uliopita wamefanya kazi  katika vyama vya msingi 14 na katika vyama hivyo walitowa malengo ya uzalishaji kili 11.6 lakini ilipofika mwisho wa msimu  waliweza kununua kilo milioni 8.3 ambazo ndio zilikuwa zimezalishwa .

Ambazo kwa ujumla wake zilkuwa na thamani ya dola  19.7 kwa fedha za kitanzania ni sawa na shilingi Bilioni 47.4  ambapo  kwenye fedha hizo kiasi cha Dola 500,000 waliweza kulipa   ushuru kwenye Halmashauri za maeneo yanayolima Tumbaku  ambazo ni sawa na fedha za Kitanzania zaidi ya Bilioni 1.4 ,

Mahundi alieleza kuwa wanaamini kiwango hicho cha fedha ni kikubwa  ambacho kinaweza kuleta maendeleo ya  chachu kwa wananchi  wa Mkoa wa Katavi na pia kwa  Halmashauri za Mkoa wa Katavi .

Baadhi ya watumishi Katika mkoa wa Katavi waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika Wilaya ya Tanganyika.

Ameeleza kuwa msimu ujao wa kilimo  Kampuni hiyo inatarajia kununua kilo za Tumbaku  milioni 11. 7 ambapo wameweza kuingia   mikataba ba vyama 16   vya ushirika  vya msingi kwa ajiri ya kununua tumbaku kwenye vyama hivyo na wanaendelea  kuvishukuru vyama hivyo kwa kuendelea kuwaamini na kufanya nao  biashara na Premium .

Mbunge  wa Jimbo la  Mpanda  Vijijini  Moshi   Kakoso alisema kiasi hicho  cha fedha kilichopokelewa kitatumiwa  vizuri kwenye maeneo yoye ya Halmashauri za Mkoa wa Katavi .

Ameiomba  kampuni hiyo   isiwachoke pindi watakapokuwa  wamewaomba tena msaada  kama huu kwa ajiri ya   huduma kwenye sekta nyingine kwani yeye anatambua kuwa  kampuni hiyo ya Premium ni kubwa hapa Duniani kwani inashika nafasi ya tatu kwa ukubwa wa makampuni yanayo nunua Tumbaku .

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Mh Moshi Sulemani Kakoso akizungumzia namna Kampuni ya Premium imekuwa na mchango katika Halmashauri za mkoa wa Katavi kupitia Ushuru.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa ambae ni  Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika  Onesmo  Buswelu   ameishukuru  Kampuni hiyo kwa kuguswa  na kile walichoweza kupata kama faida yao na kisha sehemu  kuirudisha kwa wananchi kwenye  kufanya shughuli za maendeleo katika sekta ya elimu .

Amesisitiza kuwa  Halmashauri zote  zilizopata fedha hizo kwa ajiri ya kutengeneza madawati zihakikishe ifikapo Desemba 31 ziwe zimekamilisha utengenezaji wa madawati hayo na wazingatie yawe na ubora ili watoto wa wakulima wa Tumbaku na wasio wakulima kuweza kuyatumia .

Amesema Kampuni hiyo ni miongoni mwa  makampuni yanayo nunua Tumbaku katika Mkoa wa Katavi na ni kampuni ambayo imekuwa ikifanya vizuri sana kwa kuwalipa wakulima wake kwa wakati malipo yao pasipo kuchelewa hivyo anaipongeza kampuni hiyo kwa hilo .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages