Na Paul Mathias,Mpanda
Muonekano wa Bwawa la Milala ambalo litakuwa chanzo kikuu cha Usambazaji wa Maji katika Mradi wa Maji Miji 28 utakaogharimu Bilioni 22 Katika Manispaa ya Mpanda |
Wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wanatalajia kuondokana na Adha ya upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama ifikapo 2025.
Hayo yamebainishwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Mpanda
[MUWASA [CPA Rehema Nelson alipotembelea
eneo la Mlima Veta ambalo litajengwa Tanki la Maji kupitia Mradi wa Maji wa
Miji 28.
Rehema amesema kuwa katika eneo
hilo kutajengwa Tanki la Maji lenye uwezo wa kuhifadhi Maji Lita Milioni 2
ambalo chanzo chake kikubwa kitakuwa Bwawa la Milala.
‘’Hapa ni eneo ambalo tutajenga
Tanki la Maji lenye ujazo wa Lita Milioni Mbili Maji haya yatashuka kwa
wananchi kupitia Njia ya Mseleleko na kuwahudumia wananchi wa Manispaa ya
Mpanda na mradi huu utakuwa umetatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa
Manispaa ya Mpanda ’’anasema Rehema.
Greda ikisafisha Eneo la Mlima Veta Mpanda Manispaa ambapo litajengwa Tanki la Maji kupitia mradi wa Maji wa miji 28 litakuwa na uwezo wa kuhifadhi Maji lita Milioni 2 |
Ameeleza kuwa kazi zitakazofanyika
katika mradi huo ni ujenzi wa chanzo cha Maji katika Bwawa la milala pamoja na
kujenga chujio la maji katika Bwawa hilo litakalokuwa na uwezo wa kuchuja maji
Lita Milioni 12 sambamba na ujenzi wa Tanki la Maji katika eneo la Mlima Veta
ambalo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi Maji lita Milioni 2 ambayo yatasambazwa
kwa wananchi wa Manispaa ya Mpanda kwa njia ya Mseleleko kwa Kilomita 40.
Amebainisha kuwa kwa sasa Muwasa
inahudumia Kata 11 za Manispaa ya Mpanda kati ya Kata 15 za Manispa ya Mpanda
na uzalishaji wa Maji kwa sasa ni zaidi ya Lita Milioni 7 huku kukiwa na
upungufu wa lita za Maji Milioni 4 kwenye kata 11 wanazozihudumia kwa sasa.
Katika hatua nyingine amesema kuwa Mradi wa
Maji wa Miji pindi utakapo kamilika utakuwa muarobaini kwa wananchi wa Manispaa
ya Mpanda kwani watapata huduma ya Maji kwa asilimia Miamoja katika kata zote 15 za Manispaa ya Mpanda.
‘’jumla ya kata 15 zinauhitaji wa
Maji zaidi ya Milioni 15 tunatalajia kwamba ukijumlisha na hizi Lita milioni 12
zitakazo zinazalishwa kupitia Bwawa la milala na hizi Lita zaidi ya Milioni 7
tutakuwa na jumla ya lita Milioni 19.3 tunaimani kwamba Kukamilika kwa mradi
huu wa Maji wa Miji 28 tutawahudumia wananchi wa Manispaa ya Mpanda’Kwa asilimia Miamoja’ ameeleza
Rehema.
Ameishuru serikali kwa kuja na Mpango huo wa Mradi wa Maji wa Miji 28 ambao utawasaidia wananchi wa Manispaa ya Mpanda kupata huduma ya Maji kwa ufasaha na kutoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi za serikali kwa kuilinda miundombinu itakayojengwa na serikali kwa manufaa ya Wananchi.