Na Paul Mathias,Mpanda.
Viongozi wa Serikali za Mitaa na
Vijiji katika Mkoa wa Katavi wameagizwa kuitisha Mikutano ya hadhara kwa
Wananchi ili kusikiliza kero zao ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji kwa nafasi
walizonazo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwananvua Mrindoko ,akikagua baadhi ya Majengo ya Madarasa katika Shule ya Msingi Kasisiwe kata ya Ilembo kwenye ziara hiyo.
Viongozi wa Serikali za Mitaa na Vijiji katika Mkoa wa Katavi wameagizwa kuitisha Mikutano ya hadhara kwa Wananchi ili kusikiliza kero zao ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji kwa nafasi walizonazo.
Maagizo hayo yametolewa na mkuu
wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko katika ziara yake ya Kutembelea Miradi ya
Elimu na aliyoifanya Katika Manispaa ya Mpanda kwa lengo la kujioonea Mwenendo
wa Miradi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akikagua Nyumba ya Walimu katika shule ya Sekondari Kawalyowa. |
‘’Agizo hili nikwa wenyeviti wote
wa Serikali za Mitaa na Vijiji mkoa mzima wa Katavi itisheni Mikutano ya
hadhara someni mapato na Matumizi lakini pia sikilizeni wananchi wanakero gani
zitatueni kero hizo’’amesema Mkuu huyo wa Mkoa
Amebainisha kuwa katika mikutano
hiyo wananchi waelezwe umuhimu wa kuwaandikisha watoto wao Darasa la Awali na
Darasa la Kwanza pamoja na kujiandaa kuwapeleka watoto wao Shule kujiunga na
kidato cha Kwanza mwaka 2024.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli akielezea namna Halmashauri hiyo inavyosimamia fedha za miradi ya maendeleo kwenye Manispaa ya Mpanda. |
Katika hatua nyingine Mkuu huyo
wa Mkoa amewaonya vikali wazazi na walezi ambao hawato waandikisha watoto
wao shule ngazi ya awali na darasa la Kwanza pamoja na kidato cha kwanza mwaka
2024 na kuongeza kuwa serikali haiatawavumulia na hawatosita kuchukua sheria
kali dhidi yao.
Akiwa katika Shule hiyo ya Msingi
Kasisiwe mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa Mradi wa shule hiyo unalidhisha na
kuagiza miundombinu ya Madawati pamoja na miundo mbinu mingine ikamilishwe kwa
Haraka ili watoto waanze kutumia Shule hiyo ambayo selikali imeleza zaidi ya
Milioni 600 kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kundelea fedha za Maendeleo katika Wilaya ya Mpanda ikiwemo Manispaa ya Mpanda |
Kwa upande wake Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia kumbuli amemhakikishia
mkuu wa Mkoa wa Katavi kuwa Fedha zinazoletwa na serikali kwaajili ya
kutekeleza miradi mbalimbali katika Manispaa ya Mpanda watazisimamia kwa
uadilifu.
‘’Niku hakikishie Mkuu wa Mkoa
sisi Manispaa ya Mpanda tunahakikisha feddha zinazoletwa na serikali kwaajili
ya miradi ya maendeleo tunaisimamia na kuhakikisha Miradi hiyo inajengwa ili
wananchi wapate huduma’’ anasema Kumbuli