JESHI LA POLISI KATAVI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WANAHABARI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akiwa katika mdahalo na waandishi wa habari na jeshi la polisi mkoa wa Katavi ulikuwa unajadili masuala ya ulinzi kwa waandishi wa habari wakati wakitekeleza majukumu yao kwenye mazingira ya hatari.

 

Na Paul Mathias,Katavi

Jeshi la Polisi katika mkoa wa Katavi limesema kuwalitaendelea kushirikiana na waandishi wa habari  katika utekelezaji wa amajukumu yake ya kuhakikisha usalama wa Raia na mali zao unaimalishwa kwa wananchi.

Rais wa Umoja wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzania [UTPC] Deogratius Nsokolo akielezea namna UTPC ilivyo jipanga kuhakikisha Waandishi wa Habari na Jeshi la polisi hapa nchini wanashirikiana kwa pamoja katika kazi kwa lengo la kuimarisha usalama.

Jeshi la Polisi katika mkoa wa Katavi limesema kuwalitaendelea kushirikiana na waandishi wa  katika utekelezaji wa amajukumu yake ya kuhakikisha usalama wa Raia na mali zao unaimalishwa kwa wananchi.

Hayo yamebaimishwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani wakati akifungua mudahalo maalumu kati ya jeshi la polisi na waandishi wa Habari mkoa wa Katavi ulioandaliwa na Umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania [UTPC ]pamoja na Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Katavi[KTPC]

Waandishi wa Habari mkoa wa Katavi wakiwa na maafisa wa Polisi mkoa wa Katavi kwenye Mdahalo huo.

Ngonyani amesema kuwa waandishi wa Habari katika mkoa wa Katavi wamekuwa chachu kwa jeshi la polisi kwa kuupasha umma habari mbalimbali zinazoiasa jamii kujiepusha na vitendo vya uharifu katika Shughuli zao za kila siku.

Ameeleza kuwa waandishi wa Habari wanamchango mkubwa wa kuisaidia jamii katika kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikijitokeza pamoja na mmomonyoko wa maadili katika jamii ambao umekuwa chanzo cha kuibuka kwa Makundi ya watoto watukutu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kiharifu.

Waandishi wa habari mkoa wa Katavi na Jeshi la polisi mkoa wa Katavi wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya Mdahalo.

Katika hatua nyingine ameushukuru Umoja wa Klabu za uandishi wa Habari Tanzania [UTPC] na umoja wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Katavi[ KTPC] kwa kuandaa mhadalo kuhusu Ulinzi na usalama kwa mwandishi wa habari katika maeneo ya hatari hatua ambayo itasaidia kupunguza migongano ya kiutendaji baina ya jeshi la polisi na waandishi wa Habari kwenye matukio ya hatari.

‘’Niishukuru sana UTPC kwa kutukutanisha hapa leo baina yetu jeshi la polisi na waandishi wa habari naimani tutatoka hapa tukiwa tunaimba wimbo mmoja ambao ni kuzuia uharifu na vitendo vya kiharifu sisi kama polisi na waandishi wa habari kupitia kalamu zao wataandika na kuiambia jamii kutokuwa sehemu ya uharifu  ‘’anasema Ngonyani.

Kwa upande wake Rais wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzania [UTPC] Deogratius Nsonkolo amewaasa waandishi wa habari kufanya kazi yao kwa weledi kwa kuzingatia Miiko ya kazi yao pasipo kuathiari kundi lolote kwenye jamii ili kuepuka kuzua taharuki kwenye jamii.

‘’Sisi waandishi wa habari tunamaadili yetu tuyafate na kuyatimiza tukienda kinyume tutaharibu kila kitu kwenye taifa letu tunapotengeneza uwajibikaji kwa viongozi tumejenga mahusiano ya kufanyakazi na Jeshi la Polisi basi tusifichue maovu ambayo yanafanyika kwenye maeneo ya kazi  kitu cha masingi ni kuzingatia maadili ’’ anasema Nsonkolo.

Alinanuswe Edward Mwandishi wa Habari mkoa wa Katavi akichangia hoja mbalimbali kwenye mdahalo

Katika hatua nyingine Nsokolo ameeleza kuwa waandishi wa habari wataemdelea kuwa wadau wa usalama kwa kuandika habari zinazolenga kuzuia uharifu kwenye jamii ili jeshi la polisi kuchukua hatua kwa uharaka kupitia taarifa za waandishi wa habari

Amesema kuwa Umoja wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania zinalengo la kuhakikisha zinachochea maendeleo kwenye mikoa kupitia waandishi wa Habari kwa kuandika na kutangaza changamoto na suluhu ya matataizo hayo kwa lengo la kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa wananachi na taifa zima kwa ujumla.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages