UTPC YAZINDUA KAMPENI KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Muungano wa vilabu vya Habari Tanzania(UTPCl)Kenneth Simbaya   akizungumza na Wadau wa Habari pamoja na Waandishi wa Habari katika Uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia.

 

Na Irene Temu.

Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)umezindua kampeni ya siku 16 kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo imelenga kuwaunganisha Waandishi wa Habari nchini pamoja na wadau wengine kupaza sauti kwa pamoja kupinga vita vitendo hivyo vya kikatili.

Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)umezindua kampeni ya siku 16 kupinga Ukatili wa Kijinsia ambapo imelenga kuwaunganisha Waandishi wa Habari nchini pamoja na wadau wengine kupaza sauti kwa pamoja kupinga vita vitendo hivyo vya kikatili.

Kampeni hiyo imezinduliwa Mkoani Morogoro na ilitanguliwa na mafunzo kwa Waandishi wa Habari kutoka katika mikoa 27 ya Tanzania bara na Visiwani yaliyolenga kupiga vita vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.

Akizundua Kampeini hiyo kwa niaba ya Rais wa UTPC Deo Nsokolo, Mjumbe wa Bodi ya UTPC Lilian Lucas amesema kuwa Waandishi wa Habari wanayo nafasi kubwa kupitia kalamu zao kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto vinakomeshwa.

“Kwa sasa tuna tatizo kubwa la matukio ya ubakaji na ulawiti wa watoto wa kike na wadogo, kupitia kampeni hii tunaomba wanahabari kuungana kwa pamoja na wadau wengine kuweka nguvu zaidi za kuhakikisha tunakomesha vitendo hivi kwenye jamii,” amesema Lilian.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Keneth Simbaya amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijisia hasa kwa wanawake na watoto ni miongoni mwa ukiukwaji mkubwa uliokithiri wa haki za binadamu na kuwataka wanahabari kushiriki vyema katika kuielimisha jamii.

Amesema kuwa vyombo vya habari vina nguvu kubwa ya kuifanya jamii kupata mambo ya kujadili, ambapo amewaomba waandishi wa Habari kutumia kampeini hiyo kuifanya jamii ipate cha kujadili kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na kuyapinga.

"Waandishi wa habari kemeeni vitendo vya ukatili kwa kuandika na kuibua kila aina ya vitendo vinavyosababisha ukatili pamoja na kutoa elimu kwa kuandaa vipindi na kuzipa kipaumbele habari zinazohusu ukatili katika vyombo vyetu vya habari" amesema Simbaya

Naye Ofisa Programu, Utawala na Maendeleo ya Klabu Hilda Kileo amesema kupitia kampeni hiyo, UTPC itatumia siku16 katika kutoa elimu ikiwemo kuandaa mada na mijadala mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambapo wanahabari na wadau watatoa msoni yao kwa kuchangia mjadala utakao wasilishwa kila siku katika mitandao hiyo.

Kauli mbiu ya Kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka huu ni Wekeza, zuia Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka huu ni wekeza zuia ukatili wa Kijinsia 


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages