Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stuart Kiondo akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi kwa Kipindi cha July na September. |
Na walter Mguluchuma,Katavi
Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Katavi kwa
kipindi cha Mwezi wa Saba na Mwezi wa Tisa 2023 imeweza kufatilia utekelezaji
wa Miradi 12 yenye thamani ya zaidi ya
Shilingi Bilioni 3.2 katika sekta ya elimu na kubaini uwepo wa
mapungufu mbalimbali .
Baadhi ya waandishi wa Habari mkoa wa Katavi wakitekeleza Majukumu yao wakati wa Kikao hicho. |
Kaimu Mkuu wa
Takukuru Mkoa wa Katavi Stuart Kiondo amewaambia
Wandishi wa Habari wakati akitowa taarifa ya utekelezaji wa kazi wa
Taasisi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi September mwaka huu.
Amesema katika
kipindi hicho wameweza kusaidia kufichua ubadilifu wa
fedha za Umma Shilingi Bilioni 1.23 ambazo watumishi
wa Halmashauri ya Mpimbwe walifanya ubadilifu wa Fedha hizo
Watumishi hao
walikuwa wakifanya malipo kwa mafundi na miradi hewa
kwa kutumia mawakala na watu na watu mbalimbali
wanaotowa huduma za Kibenki kupitisha fedha hizo haramu na wanaendelea
kufanya uchunguzi dhidi ya ubadilifu huu wa fedha
za umma.
Kiondo ameeleza kuwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba Takukuru Mkoa wa Katavi wamefatilia miradi 12 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.25(3,250,750,000) iliyopo katka sekta ya elimu na inaendelea kufatiliwa kwa karibu kutokana na mapungufu mbalimbali ambayo walioibaini .
Katika kipindi hicho Takukuru wameendelea kupokea malalamiko na wameweza kupokea malalamiko mbalimbali na wameweza kupokea jumla ya malamiko 73 katika ya malalamiko hayo 54 yalihusu Rushwa na 19 hayakuhusu Rushwa .
Malalamiko
yaliyohusu Rushwa yalihusu sekta za Serikali za Mitaa 41,Mapato 2,
Binafsi 1,Maji 1,Kilimo 2, Magereza 4, Elimu Msingi 2, kutokana
na malalamiko hayo majalada 5 yapo katika uchunguzi wa wazi na
yamefunguliwa majalada na malamiko 9 uchunguzi wake umekamilika .
Katika kipindi hicho mashauri sita yamefunguliwa Mahakamani na kufanya kesi ambazo zinaendelea kufikia 13 ambapo kwenye kipindi hiki wameweza kushinda kesi mbalimbali za watu waliowafikisha Mahakamani .
Katika hatua
nyingine Kiondo amewaonya watu wote ambao wamekuwa wakipita mitaani na
kuwatapeli watu kuwa wao ni maafisa wa Takukuru waache mara moja
kwani kwa wale watakao bainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao .