Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akiongea na wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Katavi[ RCC] |
Na Walter Mguluchuma,Katavi.
Wananchi katika Mkoa wa Katavi wameaondokana na adha kubwa iliyokuwa inawakabiri kwa muda
mrefu kuwafanya walazimike kuhamishia makazi yao
kwenye maeneo yenye Hospitali zinazotowa huduma ya kusafisha damu kufatia
Hospitali ya Mkoa wa Katavi kupatiwa mashine tatu za kusafisha damu
zitakazoanza kufanya kazi hivi karibuni .
Wajumbe mbali mbalimbali wa Kikao cha RCC Mkoa wa Katavi. |
Wananchi katika Mkoa wa Katavi wameaondokana na adha kubwa iliyokuwa inawakabiri kwa muda mrefu kuwafanya walazimike kuhamishia makazi yao kwenye maeneo yenye Hospitali zinazotowa huduma ya kusafisha damu kufatia Hospitali ya Mkoa wa Katavi kupatiwa mashine tatu za kusafisha damu zitakazoanza kufanya kazi hivi karibuni
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Jonas Mollel ameyabainisha hayo wakati wa kikao cha Kamati ya ushauri cha Mkoa wa Katavi (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huu kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko.
amesema kutokana na umuhimu wa mashine hizo za kusafisha
damu Serikali imeweza kuwatumia fedha Mkoa
wa Katavi za kununua mashine tatu za kusafisha damu( DAYALISISI
kwa ajiri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huu)na tayari
fedha hizo wameisha letewa na wameweza kununua kutoka MSD mashine tatu na
tayari zimeisha wasili Katavi .
Mbunge wa Mpanda Mjini Sebastian Kapufi akichangio hoja mbalimbali katika kikao cha kamati ya ushauri Mkoa wa Katavi[RCC] |
Amebainisha kuwa
pamoja na kuwepo kwa mashine hizo bado kuna changamoto ya jengo
litakalotumika kuwekea huduma hiyo kwani kwa sasa hospitali
hiyo haina jingo hilo maalumu ila wameisha anza kufanya utaratibu
wa kujenga jengo hilo maalumu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi .
Mbunge wa Jimbo la
Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi alikiambia kikao hicho
cha RCC kuwa kuna watu wengi wamehama hapa Katavi wengine
wamehamia Jijijini Mbeya na maeneo mengine kwa ajiri ya
kufata huduma yam ashine ya kusafisha damu
kutokana kutowepo kwa mashine hizo
katika Mkoa huu .
Amesema kutoka na umuhimu wa mashine hizo yeye binafsi kama hakutakuwa na mashariti mengine ya kitaalamu yupo tayari kutowa nyumba yake nzima iwezekutumika kwa ajiri ya kuweka mashine hizo hili wananchi wasogezewe huduma karibu .
Alisisitiza kuwa kutokana
na mahitaji makubwa ya wananchi kwa huduma hiyo aliomba mashine hizo zifungwe
mapema na zianze kutowa huduma kwa wananchi wa Mkoa huu ambao wengine
wanazimika kupanga vyumba vya kuishi huko Mbeya na
wapo waliopanga vyumba kwa kipindi cha miezi sita kwa ajiri
ya kuwa karibu na huduma hiyo .
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Mwanamvua Mrindoko alisema huduma ya
mashine za kusafisha damu ni muhimu sana zianze kutolewa kwa
wananchi wa Mkoa huu kutokana na mahitaji yalipo kwa sasa kwa wananchi .
Amesema kama swala la upatikanaji wa fedha za ujenzi wa jingo hilo maalamu litakalotumika kwa ajiri ya utoaji wa huduma hiyo Mkoa utaangalia namna ya kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuwezesha huduma hizo zianze kutolwa na mapema kama ambavyo Serikali ilivyokusudiwa .