Na Walter Mguluchuma,Katavi.
Serikari ya Mkoa wa
Katavi imejikita katika kuhakikisha maliasili zote
na maeneo yaliyohifadhiwa yanalindwa kwa mujibu wa
sheria za uhifadhi juhudi hizo zinadhihirishwa kutokana
na kuwepo kwa ongezeko la wanyama pori kwenye maeneo ya Mkoa
wa Katavi yaliyohifadhiwa tofauti na hapo awali .
Serikari ya Mkoa wa Katavi imejikita katika kuhakikisha maliasili zote na maeneo yaliyohifadhiwa yanalindwa kwa mujibu wa sheria za uhifadhi juhudi hizo zinadhihirishwa kutokana na kuwepo kwa ongezeko la wanyama pori kwenye maeneo ya Mkoa wa Katavi yaliyohifadhiwa tofauti na hapo awali .Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko[Katikati]akiongoza kikao cha Kamati ya ushauri Mkoa wa Katavi,RCC
Hayo yamesemwa
na Afisa wanyama pori wa Mkoa wa Katavi Josephina Rupia
wakati akisoma taarifa ya utunzaji wa mazingira na
uhifadhi wa maliasili kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa
Kataci (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa
Mkoa huu taarifa hiyo aliyoisoma kwa niaba ya Katibi Tawala
msaidizi wa Mkoa wa Mkoa wa Katavi wa uchumi na
uzalishaji .
Amebainisha kuwa
katika kuhakikisha maliasili na maeneo yote
yaliyohifadhiwa yanalindwa kwa mujibu wa sheria jitihada
hizi zimeanza kuonekana kwa kuwepo kwa ongezeko la wanyama
pori katika maeneo yaliyohifadhiwa katika Mkoa huu ammbapo
makundi makubwa ya wanyama kama Tembo , Mbwa
mwitu , Tandala , Twiga , Simba na wengineo wanaonekana
wazi katika barabara ya Mpanda kwenda Tabora wakati hapo nyuma ilikuwa ni
hadimu kuwaona kwenye barabara hiyo.
Juhudi hizi zinakwenda sambamba na ongezeko la wawindaji wa kitalii waliotembelea mapori ya akiba ya Rukwa , Inyinga na Ugala ambapo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita jumla ya wawindaji 80 na watalii 92 walifika kwenye mapori hayo .
Rupia alisema
Serikali ya Mkoa wa Katavi imeendelea kujiimarisha katika
suala zima la utalii kwa kuhakikisha vivutio vya utalii
vinapatikana ndani ya Mkoa vinatangazwa ndani a nje ya
nchi kwani hadi sasa kwa kipindi cha miaka mitano watalii
waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi ni watalii
watalii wa nje 4,809 watalii wandani 14,281wageni
wakazi 732.
Utunzaji wa
mazingira na uhifadhi wa maliasili na vyanzo vya maji
ni shughuli mtambuka ambazo zinafanywa na sekta
mtambuka katika Mkoa huu na mamlaka za Serikali za mitaa,Hifdhi ya Taifa
ya Katavi , TAWA ,TFS ambapo katika wilaya za Mlele
Mpanda na Tanganyika wamekasimiwa shughuli hizi za
uhifadhi wa maliasili ,mazingira na vyanzo vya maji .
Amefafanua kuwa
katika kuhakikisha shughuli hizi zinakuwa shirikishi
zaidi Mkoa umehakikisha jamii,taasisi za umma na binafsi
zinashiriki kikamilifu katika utunzaji wa mazingira ,uhifadhi
wa vyanzo vya maji na upandaji miti katika maeneo
yaliyopoteza uoto wa asili na katika vyanzo vya maji
inaendelea kutolewa .
Na juhudi hizi za
Mkoa wa Katavi zimeleta matunda kwa kufanikisha upandaji wa
miti 7,051,000 kwa kipindi cha mwaka
2022/2023 jambo ambalo linaloonyesha namna mkoa
unavyojari utunzaji wa mazingira .
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vjijini Moshi Kakoso ameiomba Serikali ya Mkoa wa Katavi kuhakikisha inashughulikia mgogoro ulipo wa eneo la mstu wa Ntongwe Mashariki ulipo baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika na Mamlaka ya wanyama pori (TAWA)
Amesema pia kumekuwepo na
upotevu wa mapato ya fedha za vitalu vya uwindaji
katika msti wa Nkamba ambao unapakana na Wilaya ya
Nkasi kitalu hicho kipo katika maeneo mawili ya Tanganyika na
Nkasi hivyo wanaonufaika na kitalu hicho ni Nkasi peke yao .
Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amezitaka taasisi
zote zinazosimamia maliasili na mazingira kuhakikisha zinaendelea
kusimamia sheria ili kuweza kulinda maliasili za
nchi .