Na Mwandishi wetu,Mlele
Wadau mbalimbali wa Maendeleo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wameombwa kuendelea kujitokeza kuwasaidia watu wenye
ulemavu ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha
kundi hilo linaishi bila changamoto yeyote.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga akiwa katika picha ya Pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na watu wenye ulemavu waliopatiwa viti mwendo. |
Wadau mbalimbali wa Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa katavi wameombwa kuendelea kujitokeza kuwasaidia watu wenye ulemavu ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha kundi hilo linaishi bila changamoto yeyote.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa
Wilaya ya Mlele Majid Mwanga wakati
akikabidhi viti mwendo 18 vya watu wenye ulemavu kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mlele vya walemavu vilivyotolewa na wadau wa Maendeleo Tanzania Big
Game Safari.
Mwakilishi wa Tanzania Big Game Safari akitoa neno la shukrani kwa Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kwa kuendelea kuwa wadau mhimu katika masuala ya Maendeleo kwa wananchi |
‘’tuwashukuru sana Tanzania Big
Game safari kwa msaada huu wa vitimwendo kwa watu wenye ulemavu tuwaombe sana wadau wengine kuendelea
kuwasaidia waleamavu’’amesema Dc Mwanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Teresia Irafay amewapongeza Tanzania
Big Safari kwa kuendelea kuona umuhimu wa kutoa viti hivyo kwa walemavu ili
viwasaidie katika shughuli zao.
Mwakilishi wa Tanzania Big Safari
yenye Makao makuu yake Jijini Arusha amesema kuwa wataendelea kushirikiana na
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele katika Sekta ya Elimu na Maendeleo ya Jamii kama
sehemu ya kuungana na serikali katika kuwatumukia wananchi kwa vitendo.
Nao baadhi ya walemavu waliopatiwa viti mwendo hivyo wamesema wameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kuendelea kufanya kazi na wadau mbalimbali ikiwemo Tanzania Big Game safari ambao wameonyesha mfano mzuri kwa kutoa msaada huo kwao.