AKAMATWA NA JESHI LA POLISI KATAVI AKIWA NA PINGU NA FUNGUO ZAKE.

 

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,ACP August Urio

Na George Mwigulu,Katavi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja akiwa na vifaa vya Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi ambapo lengo lake ni kuvitumia kwenye matukio ya kiharifu.

Kaimu kamada wa Jeshi la Polisi wa Mkoa huo, ACP August Urio akitoa taarifa leo kwa Waandishi wa Habari katika mahabusu ya wilaya Mpanda amesema kuwa mtuhumiwa huyo ni miongoni mwa watu 83 waliokamatwa kwa makosa mbalimbali kwa kipindi cha mwenzi Desemba mwaka uliopita.

Urio amefafanua kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo akiwa na vifaa vya Jeshi kama vile sare za Jeshi la Wananchi na Polisi,Pingu zikiwa na funguo zake pamoja na mkanda ni matokeo bora ya doria  na misako wanayoifanya kubaini,kuzuia na kutanzua uhalifu.

Kaimu kamanda huyo ameeleza katika msako huo Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na dawa za kulevya zidhaniwazo kuwa mirungi gramu tatu,watu nane wakiwa na dawa za kulevya zidhaniwazo kuwa ni bhagi kg 4 na kete 90 pamoja na watuhumiwa 17 wakiwa na pombe  haramu ya moshi kiasi cha lita 405.

Aidha watu 56 wanaojihusisha na matukio ya wizi,uporaji,uvunjaji na unyang’anyi  wamekutwa wakiwa na vielelezo za wizi Pikipiki nne MC.456 BCS aina ya Fekoni,MC 861 DDR aina ya Kinglion, MC 104 DWL aina ya Sanlg na aina ya Sanlg isiyokuwa na namba “ tumewakamata pia na mbolea za ruzuku mifuko 48.Npk mifuko 29,Can mifuko 11 na Urea mifuko 8” Amesema Urio.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limepata mafanikio ya kesi mahakamani ambapo watuhumiwa 108 wamefikishwa mahakamani ikiwa watuhumiwa 28 wamehukumiwa vifungo gerezani,watuhumiwa 26 wamehukumiwa kulipa faini,watuhumiwa 10 wameachiwa huru na 44 bado  kesi zao zinaendelea mahakamani.

Vilevile Jeshi la Polisi linawaomba wananchi wa Mkoa wa Katavi kuongeza ushirikiano katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa zitakazo saidia Mkoa kuendelea kuwa salama.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages