Baadhi ya Nyumba zilizowekwa alama ya kubomolewa kupisha Mradi wa Maji wa Bwawa la Milala eneo la Mtaa wa Mtemi Beda Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi |
Na Walter Mguluchuma,Katavi
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Mtemi Beda Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameiomba Serikali iweze kuwalipa fidia zao za makazi wanayoishi baada ya kutakiwa kupisha ujenzi wa wa Maji wa Miji 28 katika Manispa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.
Nelia Nelson mkazi wa mtaa wa Mtemi Beda akiiomba serikali kuwalipafidia ili waweze kupisha maeneo hayo kwaajili ya Mradi wa Maji. |
Mmoja wa wakazi hao Gebo Katagwa
amedai kuwa wanalia kilio kikubwa sana kwa sababu toka
Serikali ya Mkoa wa Katavi ilipotoa agizo la kuwataka waondoke kwenye
maeneo hayo na kuzuiawa kuendeleza majengo yao hawaoni kinachoendelea kwao
zaidi ya wao kuwa hatarini ya kubomokewa na nyumba wanazoishi .
Baadhi ya Nyumba zilizowekwa alama ya kubomolewa kupisha Mradi wa Maji wa Bwawa la Milala eneo la Mtaa wa Mtemi Beda Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi |
Amebainisha kuwa toka mwezi wa kumi mwaka huu
walivyofanyiwa tathimini hawajaambiwa lolote mara baada ya kuwa
limefanyika zoezi hilo na kupewa kusaini fomu za fedha wanazotakiwa
kulipwa na kisha kuondoka jumla hivyo wanaiomba Serikali iwasaidie
walipwe fedha zao wakajenge makazi mengine ya kuishi ili
wasije wakafa bure na mvua amesema Katagwa .
Lucia Evaristi
amesema Serikali iwalipe mapema ili na wao wajuwe
sehemu wanayoelekea kwani wanao watoto ambao wanatakiwa kuanza cheke chea
na darasa la kwanza mpaka sasa hawajuwi wanaelekea wapi kwa kuwa
hawajalipwa fidia zao .
Amebainisha kuwa wameendelea
kukaa ndani na karatasi zao ambazo walifanyiziwa tathimini
wanaiomba Serikali kwa kuwa imeisha amua kuwahamisha kwenye
maeneo hayo basi waweze kuwalipa kwamuda muafaka .
Faridi Paulo amesema kuwa baada ya kuwa wamefanyiwa tathimi waliambiwa kuwa watalipwa baada ya wiki mbili na wao kwa sasa wanahari mbaya kwani nyumba zao zinazidi kuharibika na kubomoka kwa kuwa wameisha ambiwa wasiendeleze kitu chochote kilehivyowanashindwa kufanya ukarabati .
Amemwomba Rais Samia awasaidie
kwa hilo ili waweze kulipwa fidia zao hizo kwani hari zao
zimekuwa ngumu kutokana na baadhi ya watu wengine kuamua
kuhama eneo hilo na kwenda kuishi katika nyumba za kupanga na
familia zao .
Nelia Nelson amaesema
kuwa wameshindwa kufanya kitu chochote hata kupanda mboga
wameshindwa matokeo yake hakuna maendeleo yanayofanyika matokeo
yake ni nyumba kuanza kubomoka basi was aid iwe kulipwa fedha
mapema ili waondoke .
Ameeleza kama wanaendelea kubaki waluhusiwe kuendelea kufanya maendeleo kama walivyokuwa wakifanya maendeleo ya
makazi yao na shughuli nyingine za kujiongezea kipato chao kama hapo
awali .
Diwani wa Kata ya Misunkumilo
Afred Matondo amesema kuwa ni kweli wananchi hao wa Mtaa
wa Mtemi Beda wapatao zaidi ya 140 wanadai fidia yao kwa ajiri ya
kupisha eneo la bwawa la Milala kunakotekelezwa mradi wa Miji
28 ambapo Serikali bado wapo wanaendelea na mchakato wa
kuwalipa fidia wananchi hao .
Hivyo hadi sasa kwenye eneo hilo
la wananchi wengi wanao lalamika wameisha fanyiwa tathimini ya
malipo yao isipokuwa watu wachache tuu ambao ndio bado
kufanyiwa .
Diwani wa Kata ya Misunkumilo Afred Matondo akielezea mchakato wa fidia kwa wananchi hao |
Amesema licha ya taratibu hizo kuwa zinaendelea kumekuwepo kwa baadhi ya changamoto ya baadhiya wananchi ambao hawajajitokeza kufanyiwa tathimini na kusababisha kukamilika kwa zoezi hilo hata hivyo yeye kama Diwani amepanga kwenda kufanya mkutano na wananchi hao ili awaelimishe kwani ni vigumu watu kulipwa kabla ya kujiridhishs kwanza .