BABA AFUKUWA MWILI WA MAREHEMU MTOTO WAKE ILI AMWOMBEE AFUFUKE.

 



Na Walter Mguluchuma -Mpanda

Mtu  mmoja  aliyefahamika kwa jina la Fransis Agustino Nilanga  amekamatwa akiwa na Jeneza lililokuwa  ndani  na mwili wa marehemu  mtoto wake alioufukua makaburini  kwa lengo la kwenda nao nyumbani  ili kuuombea uweze  kufufuka .

Mtu  mmoja  aliyefahamika kwa jina la Fransis Agustino Nilanga  amekamatwa akiwa na Jeneza lililokuwa  ndani  na mwili wa marehemu  mtoto wake alioufukua makaburini  kwa lengo la kwenda nao nyumbani  ili kuumbea uweze  kufufuka .

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kapalangao Fransis  Feruzi  amesema tukio hilo  la kusikitisha  na  lilozua  tahaluki  kwa wananchi wa  Mtaa huo na Manispaa ya  Mpanda  limetokea usiku wa kuamkiajuzi katika  makaburi ya Kazima Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Amemtaja  marehemu  huyo  aliyefukuliwa   kwenye   kaburi la  na  baba yake  mzazi kuwa ni  Imelda  Nilanga  aliyefariki mwaka jana  mwezi wa saba  akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu .

Amebainisha kuwa siku hiyo ya tukio  majira ya saa tisa na nusu usiku alipigiwa simu wakati akiwa amelala  nyumbani  kwake alipigiwa simu na  jeshi la Polisi  iliyokuwa inamtaka  kueleza  kama  anamjua  mtu anaejulikana  kwa jina la Fransis  Agustino  Nilaga   na baada ya kutajiwa  jina hilo  aliwajibu kuwa  anamfahamu .

Baada ya kuwa amekubali kuwa anamfahamu alitaalifiwa kuwa amepatikana akiwa  na jeneza  ambalo  ndani yake  Kulikuwa  na  mwili wa marehemu  mwanae na anashikiliwa  katika kituo cha  Polisi cha Wilaya ya  Mpanda  baada ya kuwa  wamepewa taarifa na  mwendesha  bajaji ndipo walipoweza kumkamata.

Kufatia taalifa hiyo alilazimika  kwenda nyumbani kwa  baba yake na  mtuhumiwa huyo kwa kuwa walikuwa wanaishi nae jirani iliaweze kupata ukweli kama aliyekamatwa ndie  mtoto wake  basi   kwa Mzee  nilanga ni jirani  alienda kumfunguza  na baada ya kumfunguza  alimuuliza  mwanao  Fransis  yupo  ndani  akasema ngoja  amwangalie chumbani kwake na alimwangalia hamkuweza kumkuta chumbani kwake .

Feruzi amesema ndipo alipomweleza  mzazi wake kuwa mwanao  yupo  kituo cha polisi amekamatwa akiwa na   jeneza  lenye  mwili   wa  marehemu aliyemfukua   makaburini .

Amebainisha baada ya kuwa wamefika kwenye kituo cha polisi kweli walikuta sanduku lilikuwa na  mwili wa  marehemu    na  ndipo walipo pewa maelezo kuwa  Fransis  Nilanga  amekutwa na jeneza    likiwa na mwili wa marehemu katika  maeneo ya makaburi ya Kazima  baada ya kumwomba    mwendesha  bajaji amsaidie kubeba sanduku hilo kwenda nalo nyumbani kwake .

Kufatia  kupatiwa  maelezo kituoni hapo   yeye  pamoja  na  mzee  Nilanga  waliomba  wapewe   nafasi ya  kuweza kumwona  Fransis ili waweze kumtambua kama ni yeye na waliweza kumtambua kweli  ni yeye na katika mazungumzo  yake alisema  aliamua kufanya hivyo kutokana na huzuni ya muda  mrefu  ya kumkosa mwanae  aliyekuwa wa kwanza .

Alitumani  kwamba  katika  maombi  ambayo angemfanyia mwanae  licha ya kuwa amekufa toka  mwaka jana  angweza kufufuka  ndipo     siku hiyo   uzuni ilipokuwa imemshika usiku   alichukua  uamuzi wa kutoka  na jembe na kwenda makaburini kufukua mwili   wa marehemu mtoto wake  alikwenda  kuufanyia maombi  kwa kutumia  Bibilia  Takatifu

Mwenyekiti  huyo wa  Mtaa   ameeleza kuwa kwa dalili za  historia yake  inaonyesha alikuwa na shida ya afya ya akiri  ndio inawezekana ilimfanya achukuwe  maamuzi hayo  yeye  kama  mwenyekiti wa  mtaa analithibitisha tukio hilo limetokea na  mwili wa marehemu huyo walikabidhiwa  ndugu zake na waliweza kuuzika  kwenye  kaburi lilile  alikuwa amezikwa mwanzo .

Nae  mkazi wa  Mtaa huu Mona Joseph amesema kuwa tukio hilo kwake ni la kwanza toka alopoanza kuishi kwenye mtaa huo  alikuwa haja wahi kuona tukio kama hilo

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages