Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi,Faustine Maijo akitoa taarifa ya taasisi hiyo ya utekelezaji wa utendaji kazi ya kipindi cha mienzi mitatu iliyopita. |
Na Walter
Mguluchuma,Katavi
TAKUKURU Mkoa wa Katavi kwa
kipindi cha miezi mitatu imefatilia utekelezaji wa
miradi 11 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya
shilingi Bilioni 9.5 katika sekta mbalimbali zikiwemo
na sekta ya Elimu na afya na kubaini mapungufu
mbalimbali yakiwemo kutofuata taratibu za manunuzi.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo akitoa taarifa mbele ya waandishi wa Habari
TAKUKURU Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha miezi mitatu imefatilia utekelezaji wa miradi 11 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 9.5 katika sekta mbalimbali zikiwemo na sekta ya Elimu na afya na kubaini mapungufu mbalimbali yakiwemo kutofuata taratibu za manunuzi.
Wameweza kupokea malalamiko 65 ambapo
taarifa zinazohusu rushwa zilikuwa 35 na zisizohusu
rushwa 30 huku serikali za mitaa ikiwa ilaongoza
kwa kalalamikiwa na wananchi waliopelela malalamiko yao.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa
Katavi, Faustine Maijo wakati akitowa taarifa ya utendaji kazi wa
Taasisi hiyo ya Kuzuia na Kumbana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa
Katavi ya utendaji kazi wa kipindi cha miezi mitatu ya Otoba 2023 hadi
Desemba 2024 kwa wandishi wa Habari.
Maijo ameeleza kuwa kwa kuzingatia kuwa
serikali imepeleka miradi mingi ya maendeleo kwa
wananchi na kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya
utelelezaji wa miradi mbambali ya Maendeleo kwenye maeneombalimbali
ya wananchi.
Baadhi ya waandishi wa Habari mkoa wa Katavi wakiwa katika mkutano na mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi
Kwa kutambua hilo TAKUKURU Mkoa wa
Katavi katika kipindi hicho imefatilia jumla ya
miradi 11 inayotekelezwa katika Mkoa huu yenye thamani
ya Tshs 9,579,630,108 kwenye sekta za elimu , afya na
ufundi sitadi (VETA )
Katika kufatilia miradi hiyo
inayoendelea kutekelezwa TAKUKURU wamekuwa wakiifatilia
kwa karibu sana na katika ufatiliaji wa miradi hiyo
11 wameweza kubaini baadhi ya mapungufu kwenye miradi
hiyo ikiwemo ucheleweshaji wa miradi na pia kutofuatwa
kwa taratibu za manunuzi.
Kuhusu malalamiko Maijo ameeleza kuwa
wameendelea kupokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa
wananchi yanayohuasiana na Rushwa ambapo wameweza kupokea
malalamiko 65 kati ya hayo 35 yalihusu Rushwa na 30 hayakuhusu
Rushwa na malalamiko hayo yalihusu sekta za Serikali za
Mitaa 23, Kilimo 2,Binafsi 2 TFS 1, Maji 1, Ardhi
1, Makazi ya Wakimbizi 2, Polisi 1 na Afya 1.
Amefafanua kuwa taarifa zinazohusu
Rushwa zimeshughulikiwa kwa mujibu wa sheria
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007
hali ambayo imepelekea Takukuru Mkoa wa Katavi
kuanzisha uchunguzi wa majalada 35 ya uchunguzi wa
awali kati ya hayo majalada matatu
yamekamilika na katika kipindi hicho mashauri 2
yamefunguliwa Mahakamani na kufanya kesi zinazoendelea kuwa
9.
Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa wa Katavi
amesema katika kipindi cha Januari hadi
Machi 2024 wameimarisha juhudi za Kuzuia Rushwa kwa
kuendelea kufatilia utekelezaji wa miradi
ya maendeleo.
Kwa kuhamasisha na kutoa elimu ya
ushiriki ya ushiriki wa wananchi katika
vita dhidi ya Rushwa kupitia vyanzo mbalimbali
za uelimishaji ikiwemo vipindi vya radio na katika
mikusanyiko mbalimbali kwa kutumia mwongozo wa
TAKUKURU RAFIKI.