Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akihutubia kwenye tamasha la Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amepongeza jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa kuweza kufanikiwa kufanya kazi nzuri ya kuweza kudhibiti kikundi cha uhalifu kilichokuwa kinatishia amani kwa wananchi hasa wa maeneo ya Manispaa ya Mpanda.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akifanya vipimo vya afya katika moja ya banda kwenye kwenye tamasha maalumu. |
Pongezi hizo amezitolewa wakati akiwahutubia askari wa Jeshi la Polisi pamoja na wananchi wakati wa sherehe ya Polisi Famiy day iliandaliwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na Klabu ya Wandishi wa Habari na kufanyika katika viwanja vya michezo vya polisi.
Amebainisha kuwa vitendo vya uhalifu vilivyokuwa vinafanywa na vikundi vinavyoitwa damu chafu katika Mkoa wa Katavi na hasa katika eneo la mji wa Mpanda kwa kiasi kikubwa kwa zaidi ya asilimia ya asilimia 99.5 jeshi la Polisi limeweza kufanikiwa kudhibiti uhalifu huo.
Mrindoko amesema wameshuhudia katika kipindi cha mwezi Desemba na Januari wameona hali ya utulivu imeendelea kuimalika na matukio yale ya damu mchafu yamepungua kwa kiasi cha asilimia hizo.
Amewataka kuhakikisha hicho kiasi kidogo kilicho baki kinakwisha kabisa ndani ya Mkoa wa Katavi na uhalifu mwingine wowote ambao unaleta bugudha kwa jamii ambapo unaleta madhara kwa watu wakati mwingine unatowa uhai wa baadhi ya watu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,ACP Kaster Ngonyani akifanya vipimo vya afya katika moja ya banda. |
Baadhi ya asikari wa Jeshi la Polisi wakifanya onesho maalumu wakati wa tamasha maalumu. |
Hivyo amewahakikishia Wananchi wa Mkoa wa Katavi kuwa jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi lipo kwa utayari kwa kuhakikisha hali ya usalama inaendela kuimarika zaidi kupatikana na amewaomba wananchi kuendelea kutowa ushirikiano kwa jeshi hilo kwa kuwajulisha mapema matukio ya uhalifu kabla hayaja tokea.
Mrindoka ameviagiza vyombo vyote vya usalama katika Mkoa huu kuhakikisha wanaongeza jitihada za kudumusha hali ya usalama unaendelea kuwa imara zaidi na zaidi ili wananchi waendelee kuishi kwa amani na kwa utulivu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amesema siku hiyo ya polisi ‘ Family Day’ wameamua kuifanya kwa pamoja na wandishi wa habari ili kuendelea kuwa na ushirikiano zaidi baina yao na jeshi la polisi katika kitimiza kazi zao za pambe hizo mbili..