MANISPAA YA MPANDA YAPITISHA MAPENDEKEZO YA BAJETI YA BILIONI 27.5

Baadhi ya Madiwani katika Halamshauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakiwa katika kikao hicho cha Kupitisha Rasimu ya Bajeti.

Na Walter Mguluchuma-Mpanda 

Halmashauri ya Manspaa ya Mpanda imepitisha  mapendekezo ya rasimu ya Mpango wa  Bajeti ya waka wa fedha 2024/ 2025 ikiwa imezingatia  vipaombele vya  miradi   muhimu ya  maendeleo  huku  fedha za  mapato ya  ndani zikiwa   ni zaidi ya  shilingi Bilioni 5.2

Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry akifungua kikao cha Kupisha Rasimu ya Bajeti kwa Manispaa ya Mpanda 

Halmashauri ya Manspaa ya Mpanda imepitisha  mapendekezo ya rasimu ya Mpango wa  Bajeti ya waka wa fedha 2024/ 2025 ikiwa imezingatia vipaombele vya  miradi   muhimu ya  maendeleo  huku  fedha za  mapato ya  ndani zikiwa   ni zaidi ya  shilingi Bilioni 5.2

Manispaa  hiyo kwa   mwaka   fedha wa 2022/2023 iliweza  kukusamya  kiasi cha  Tshs 25,806,650,000.00 kutoka  kwenye   vyanzo  vyake   mbalimbali  vya  mapato .

 Mapemdekezo hayo ya  bajeti yamepitishwa katika  kikao cha  Baraza  la  Madiwani la Manispaa ya Mpanda kilichofamyika  katika  ukumbi wa Halmashauri hiyo  na kuoongozwa  na Msitahiki  Meya wa Manspaa ya  Mpanda  Haidari  Sumry .

Kaimu  Mkuu wa Idara ya Mipango wa  Manspaa ya  Mpanda  Leonard  Kilamuhaa akiwasilisha   mapemdekezo ya   Bajeti hiyo  kwa   Baraza la Madiwani  aamesema kwa  mwaka ujao wa fedha wa 2024/2025 Inatarajia  kukusanya  na kupokea jumla ya  Tshs 27,553,717,500,00 huku  mapato ya  ndani  ikiwa   ni  Tshs 5,241,761,500,00.

Amebainisha kuwa  mapato ya  ndani  halisi  ni  Tshs  3,410,981,500,00  na  mapato ya   ndani fungiwa  tshs 1,830,780,000,00  ruzuku  ya Serikali   na wafadhili  ikiwa ni kiasi  cha Tshs  23,830,956,00,00  makadilio ya  mapato ya  ndani  yanaonyesha uwezo   wa  Halmashauri ya  Manispaa ya Mpanda  wa  kujitegemea kwa asilimia  18 hivyo   inagemea  kutegemea  Serikali na wafadhili kwa asilimia  82.

 Kilamuhaa alieleza kuwa   ili kuweza kufikia  malengo  ya  ukusanyaji wa  mapato ya  ndani  ya  mwaka ujao wa fedha  wamejiwekea mikakati mbalimbali ambapo ameitaja  baidhi ya mikakati hiyo  kuwa  ni  kuongeza idadi ya  [POS] Mashine za kukusanyia mapato  ili kuweza  kusaidia kuzuia mianya ya upotevu wa fedha .

Mkakati   mwingine  ameutaja kuwa ni  kuendelea kuhamasisha uwekezaji  wa  viwanda  katika  maeneo   yao  ili  malighafi  zinazopatikana  kwenye Manispaa  ziendelee kuongozeka  thamani   na kuleta tija kwa wananchi .

Msitahiki Meya wa Mamispaa ya   Mpanda  Haidari  Sumry  amewaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa      bajeti hiyo imelemga  zaidi  kwenda  kuwatatulia wananchi  changamoto  mbalimbali  na  kuwaletea     maendeleo. 

Amesemea  katika  kuhakikisha  bajeti hiyo  inalenga  kutatua  kero za wananchi    ndio   maana wametenga   fedha kwa ajiri ya  kununua  gari   jingine  la  kusomba  taka  ili  kusiwepo  na   mlundikano wa taka  kwemye  mamispaa hiyo .

Amewata watemdaji wa kuweka kipaumbele  tana cha kuchomga   barabara  kwemye  maeneo yote  ambayo yanayokuwa yamepimwa kwani kwa  mwaka  huu  wa fedha  wamweza kufanya  vizuri sana kwa kuweza kufungua barabara .

Mkurugenzi wa  Halmashauri ya  Manispaa ya Mpanda Sophia  Kumbuli  amesema kuwa   mchakato huu wa   mapendekezo ya   bajati  hauta ishia hapo  bali  unaendelea tena  kwenye  hatua   myingine  zaidi

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages