Mganga Mkuu wa Mkoa, Dk Jonatham Mdemu. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi
Mradi wa THAMINI UHAI
unaotekelezwa katika Mikoa mitatu nchini umesaidia sana
katika Mkoa wa Katavi kupunguza vifo vitokanavyo na
uzazi mradi huu umekuwa sehemu ya kupunguza vifo hivyo kwa kuweza
kuwaelimisha watu kuwa na wasindikizaji kwa
wajawzito kwa kuwapeleka kwenye vituo vya kutolea huduma ya
mama na mtoto na siku ya kujifungua kijifungulia kwenye vituo
badala kujifungulia nyumbani .
Afisa Mradi wa Thamini Uhai Dr Calist Nzabuhakwa |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dk Jonathan Mdemu amebainisha kuwa kwa kipindi
cha miaka mitano iliyopita vifo vya akina mama vitokanavyo na
uzazi vimeendelea kupungua ambapo kwa mwaka 2018 vifo vya watoto wachanga
vilikuwa 631 hadi kufikia Desemba 2023 vifo vya watoto
wachanga vimetoka kwa idadi hiyo hadi kufikia 270 ambavyo
vimepungua kwa zaidi ya nusu .
Kwa upande wa vifo vya
akina mama vitokanavyo na uzazi vimeendelea kupungua kwa miaka
mitatu ya nyuma kulikuwa na vifo 50 mwaka 2022 kulikuwa na vifo 36 na
mwaka 2023 kulikuwa na vifo 27 vilivyotokea katika Halmashauri zote tano
za Mkoa wa Katavi .
Ameeleza mradi
wa THAMINI UHAI umekuwa ni sehemu ya kupunguza vifo hivyo kwa
sababu wakina mama wameacha kujifungulia nyumbani idadi
yao inakwenda chini kutoka na elimu ambayo imekuwa ikitolewa na
THAMINI UHAI .
Dk Mdemu amefafanua
kuwa wajawazito wanapokuwa wamekwenda kwenye vituo vya
kutolea huduma wakiwa na wasindikizaji wao wanawasaidia wanakaa nao
wanakuwa wanaona maendeleo ya hali zao wanazokuwa nazo kabla ya
kujifungua ambapo hapo awali walikuwa wakiwazuia wajifungulie
nyumbani kwa sasa wanawasindikiza kwenda hospitali.
Amesema kwenye Mkoa huo mradi wa THAMINI UHAI umesaidia akina mama wanaojifungulia njiani kupungua ambapo kwa sasa kuna zaidi ya asilimia 80 ya akinamama wanaojifungulia katika vituo vya Afya na kuhudumiwana wataalamu wa afya.
‘Mwanzoni kulikuwa hakuna usiri sasa hivi tuna vituo vinane vimewekwa ambavyo vimesaidia kuwepo kwa faragha wakati wa kujifungua na kupelekea baadhi ya wajawazito kutoka wilaya ya Tanganyika kwenda kujifungua katika kituo cha Afya Ilembo Manispaa ya Mpanda…usiri huo umesaidia kwenda na wasindikizaji au wenza wao kuangalia mjamzito anavyosaidiwa’’ amesema Dk Mdemo.
Ameongeza kuwa ni
zaidi ya asilimia kumi ya wanaume wameweza kuwasindikiza wenza wao hivyo
bado inatakiwa kuendelea kuhamasisha halmashauri katika majengo yao
wanayojenga au wanayoyakarabati waone ni jinsi gani ambavyo wataweza
kutengeneza sehemu ya faragha ya kujifungulia kwa wajawazito
kwani kuna vituo nane pekee kati ya 130 katika Mkoa wa Katavi vinatoa huduma
hiyo.
Amesema wahudumu wa
afya ngazi ya jamii ni sehemu ya jamii tunaelewa kuwa vituo vingi
vya afya hazina watumishi wengi wa kutosha na ukiangalia maeneo mengi
wamekuwa wakitumiwa katika maeneo mengi na alitowa mfano kumekuwa na
magonjwa mengi ya mlipuko kama pindupindu kilichotokea mwaka
jana huko Karema Wilaya ya Tanganyika wailiweza kuwa na wahuduma wa
ngazi ya afya wawili kwenye kila Kitongoji ambao waliwasaidia kusambaza
vitakasa maji kwa wananchi .
Project Officer Clinkar wa Thamini Uhai Dr Calist Nzabuhakwa amesema huduma hii ya msindikizaji toka wameianzisha ina muda wa miaka mitano sasa na walianzia katika Mkoa wa Kigoma kwa Katavi wameanza mwaka 2020 na kwa Mkoa wa Katavi walianza na vituo nine kwa sasa vipo nane .
Huduma hii ya
msindikizaji wakati wanaianzisha walilenga kuangalia namna ambavyo
Thamini Uhai inavyoweza kusaidiana na Serikali namna ya kupunguza vifo
vya wajawazito au kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi walipanga
kutowa huduma ya mradi huu kwenye maeneo ambayo ni magumu kufikika kwa
sababu akina wajawazito wengi walikuwa wanafika kwenye vituo walikuwa wanafika
kwa kuchelewa kutokana kukimbilia kwa wakunga wa jadi .
Waliona huduma hii ya
msindikizaji inaweza kusaidia sana kuwaleta watu walikuwa
wanajifungulia kwa wakunga wa jadi kuweza kuwapeleka kwenye vituo vya
kutolea huduma za mama na mtoto ambapo wanapatiwa huduma
zilizosahihi kuliko kwa mkunga wa jaji ambae hanauwezo wa kumwongezea
damu mama mjamzito anapokuwa ameishiwa damu wakati wa kujifungua au
ugonjwa wa kifafa cha uzazi .
Amesema huduma hii kwenye maeneo yote waliyoanzisha vifo vya mama na mtoto vinaendelea kushuka na mategemeo yao ni kuhakikisha vifo vya akina mama ninakwisha vinabakia sifuli na wakushirikiana na Serikali wanapenda huduma hii iweze kusambaa nchi nzima haina tatizo lolote inatowa matokea chanya kwa mja mzito anapokwenda kujifungua.
Nae mtoa
huduma wa ngazi ya jamii katika Kijiji cha Nduwi Kata ya Katumba
Wilaya ya Mpanda Sofia Kayanda alisema amekuwa muhudumu
wa afya kwa kipindi cha miaka mitatu amekuwa akitowa elimu kwenye
jamii umuhimuwa msindikiza na wameisha andaa kamati ya
kumsindikiza mjamzito kwenda kujifungua hata kama mume wake anapokuwa
hayupo .
Na kunakuwepo na
watu ambao wamekuwa wameandaliwa na wanapokuwa wamepewa taarifa
wanamsindikiza mjamzito kwenda kujifungua kwa kuambatana na msindikizaji
wake ambae anae kuwa amechaguliwa na toka awali na mjazito mwenyewe kwani
msindikizaji sio lazima awe mwenza bali ni mtu aliyemwamini
mwenyewe mamzito .
Mratibu wa huduma za
afya ya uzazi na mpango wa Mkoa wa Katavi Hilida Machungwa
huduma ya msindikiza wamekuwa wakihakikisha wanafanya uzimamizi kwenye
vituo vyote nane vinavyotowa huduma hiyo kwa kuhakikisha
akina mama wanapata elimu kuanzia kwenye mahudhurio yao ya
killiniki wa wajawazito juu ya umuhimu wa wao kwenda na
wasindikizaji wakati wa kujifungua .
Wasindikizaji hao wamekuwa wakipatiwa elimu toka awali ili pale mjamzito anapokuwa amepata uchungu atakwenda nae kituoni kwa ajiri ya kujifungua kwa kuwamsindikizaji huyo atakuwa amepata elimu ya kujua majukumu yake wakati wa kujifungua .huduma hii imeleta ufanisi mkubwa kwa idadi kubwa kwa sasa kwenda kujifungulia kwenye vituo hivyo vya kutolea huduma kwa kuwa mazingira yameboreshwa.