RPC KATAVI VYOMBO VYA HABARI WAMEKUWA CHACHU YA KUPUNGUZA UHALIFU.

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,ACP Kaster Ngonyani akizungumza kwenye mdahalo awamu ya pili ulioandaliwa na UTPC.

Na George Mwigulu, Katavi.

Ushirikiano uliopo baina ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Katavi kupitia mpango wa jeshi hilo wa polisi jamii umekuwa chachu kubwa wa kutokomeza vitendo vya kihalifu mkoani humo.

Picha ya pamoja ikijumuisha Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,ACP Kaster Ngonyani, Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari MKoa wa Katavi Walter Mguluchuma,Afisa Mipango Msaidizi kutoka UTPC na baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi na waandishi wa habari.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Kaster Ngonyani amezungumza hayo leo kwenye mdahalo maalumu ulioandaliwa na Umoja Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kufanyika katika ukumbi wa St Mathias uliopo Manispaa ya Mpanda.

Lengo la mdahalo huo awamu ya pili ni kuelimishana kitaaluma,kujenga na kuimarisha mahusiano ya mashirikiano ya kikazi baina ya Jeshi la Polisi na Waandishi wa habari utakao saidia kuepuka migongano inayoweza kuhatarisha zaidi usalama wa waandishi wa habari.

ACP Ngonyani amesema Jeshi la polisi katika kutoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi waandishi wa habari wamekuwa kiungo muhimu kupitia vyombo vyao vya habari kuweza kuufikia umma kwa haraka.

“Ushirikiano huu tuliokuwa nao mwaka 2023 naomba uendelee mwaka 2024...katika kutoa elimu wanahabari ni chachu yetu hadi sasahivi mkoa wa Katavi upo salama uharifu umepungua sana hata ukiingia kwenye RB zetu kwenye vituo vya polisi makosa ni machache sana kwa kuwa waandishi wa habari na jeshi la polisi pia tumeshirikiana kupinga uhalifu” Amesisitiza ACP Ngonyani.

Akiwasilisha mada ya kuendeleza mahusiano mazuri ya jeshi hilo na vyombo vya habari,SSP Juma Jumanne amesema kuwa wanatambua umuhimu wa vyombo vya habari kwani huelimisha jamii juu ya madhara ya uhalifu,umuhimu wa utoaji taarifa za uhalifu na wahalifu mambo ambayo ni kazi ya msingi ya jeshi hilo.

SSP Juma Jumanned akitoa mada ya kuendeleza mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na Vyombo vya habari. 

Afisa Mipango Msaidizi wa UTPC akiwasilisha mada katika mdahalo uliojumuisha jeshi la polisi na waandishi wa habari Mkoa wa Katavi ambapo amesisitiza mahusiano mazuri ya kikazi.

SSP Jumanne amefafanua kuwa waandishi wa habari wanaingia kwenye migogoro na jeshi la polisi pale ambapo kila mmoja kutokutambua majukumu ya mwingine jambo ambalo linapaswa kuepukwa kwa kujengeana uwezo wa kitaaluma.

Amesema vyombo vya habari vinanafasi na jukumu la kuandika habari za kisayansi,kijamii,kimichezo,kimahakama na uchunguzi kwa ufundi,kitaalamu, kiuchambuzi wa kina  na kupaswa kuepuka kuripoti zaidi kuliko kuelimisha jamii juu ya madhara ya uhalifu.

“ nitoe nukuu hii mnielewe...mwanzilishi wa kampuni ya magazeti ya Scrips  Mr Willing Scripts, aliwahi kusema  jukumu la vyombo vya habari ni kuwastarehesha wale wanaotaabika na kuwataabisha wanaostarehe na Msimamizi wa habari wa Ikulu ya Marekani Mccury alisema huwezi kuwastarehesha au kuwataabisha watu bila kuwapa habari bora” Amesema SSP Jumanne wakati akisisitiza waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi.

 Edmund Kipungu,Afisa Mipango msaidizi wa UTPC amesema lengo la UTPC Klabu za waandishi wa habari hapa nchini zinajenga ushirikiano wa kazi kwa kuwa hufanya kazi zinazofanana japo jeshi la polisi limepewa mamlaka ya kusimamia sheria.

Walter Mguluchuma,Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Katavi akitoa hatuba ya fupi ya kufunga mdahalo wa awamu ya pili uliondaliwa na UTPC ambapo amesisitizia suala la waandishi wa habari kujiepusha na ushabiki wa kisiasa.

Afisa Mpingo huyo ameeleza kuwa mahusiano yakiimarishwa kwa vitendo utajenga usalama kwa waandishi wa habari pamoja na kutokomeza zaidi uharifu.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Katavi, Walter Mguluchuma wakati akifunga mdahalo huo amesema kuelekea uchanguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchanguzi mkuu wa mwaka 2025 waandishi wanapaswa kuepuka kujihusisha na masuala ya kisiasa kwani yatawapunguzia Imani kwa wananchi na kuhatarisha usalama wao.

Mguluchuma amesema waandishi wa habari wanapaswa kufanya kazi kwa kunzingatia maadili na kuepuka kuvuja sheria za nchi kwa sababu wao ni waandishi kwani watashughurikiwa kama wahalifu wengine.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages