WANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani akifunga Mdahalo awamu ya Tatu baina ya waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi

Na Walter Mguluchuma-Katavi

Waandishi wa  Habari wa  Mkoa wa  Katavi wameaswa  kufanya kazi zao  kwa  kuzingatia  maadili ya  kazi zao  ili  kuondoa  migongano baina yao na  jeshi la  Polisi  linapokuwa linatimiza majukumu yao ya  utendaji wa  kazi kwenye matukio mbalimbali .

Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi wakiwa katika picha ya paomoja na kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Kaster ngonyani baada ya mdahalo huo

Waandishi wa  Habari wa  Mkoa wa  Katavi wameaswa  kufanya kazi zao  kwa  kuzingatia  maadili ya  kazi zao  ili  kuondoa  migongano baina yao na  jeshi la  Polisi  linapokuwa linatimiza majukumu yao ya utendaji wakazi kwenye matukio mbalimbali 

Wito huu umetolewa  na  Kamanda wa Polisi wa  Mkoa wa  Katavi Kaster Ngonyani  wakati akifunga   mdahalo wa  awamu ya  tatu  uliowashirikisha  Wandishi wa   Habari wa Mkoa wa Katavi  uliofanyika  katika  ukumbi wa   ST  Mathias wenye  lengo kuimalisha   uhusiano  wa kazi    baina ya wandishi na jeshi la polisi na  ulinzi  na usalama kwa wandishi wakati wa matukioya hatari .

Amesema  ilikuweza  kuondoa  mingano  ambayo inaweza  kutokea  kati ya  wandishi wa  Habari na  Jeshi la  Polisi  wanapokuwa  wanateleza  majumu yao   ni   vema  wandishi wakafanya  kazi zao kwa kuzingatia  maadili yao na  vilevile  polisi nao wafanye kazi kwa kuzingatia  maadili yao ya  kazi .

Amebainisha kuwa  midahalo  hiyo mitatu iliyofanyika  baina ya Polisi na  wandishi wa  habari  imejenga  mahusiano  mazuri zaidi kati ya pande hizo mbili  na   mahusiano hayo yataendelea kuwa  endelevu  zaidi  katika  utendaji wa  kazi .

Kamanda  Ngonyani  amewahakikishia  wandishi wa  Habari  kuwa  jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi  linaendelea  kuwalinda na  kuhakikisha wanakuwa salama  pindi wanapokuwa wanatimiza  majukumu yao kwani  wao  hilo ni jukumu lao la  kuhakikisha wandishi     pamoja na wananchi wanakuwa salama .

Amesema  jeshi la  Polisi linatambua kuwa  wandishi wa habari  ni watu muhimu sana  kwenye  shughuli zao  za kila siku  kwani wamekuwa  wakiwatumia  kutowa taarifa zao mbalimbali   kwenda  kwa wananchi kupitia  vyombo vyao  na  kuendelea  kuufanya  Mkoa wa Katavi kuendelea  kuwa salama zaidi

Amewasisitiza  Askari  Polisi  wote  kuhakikisha wana waona  wandishi wa  habari kuwa ni  marafiki zao kwani ndio  vipaza  sauti za kazi zao wanazofanya  na vilevile  polisi na wandishi wanapokuwa wanafanya kazi zao  vizuri   ndio  kunawafanya waweze kuaminika zaidi

Kamanda  Kaster  Ngonyani  amewashukuru   Muungano wa  Club  ya  Wandishi wa  Habari  Tanzania (UTPC)  kwa  kuweza  kuandaa  midahalo hiyo    mitatu kwani  iweza kujenga zaidi  mahusiano  katika ya  jeshi la  polisi na wandishi wa  habari .

Nae  Afisa wa Jeshi la  Polisi  Mkoa wa Katavi  Juma Jumanne  amewahimiza kutoandika habari  ambazo  zinaweza   kujenga chuki kwenye jamii.

Aidha amewasisitiza  wasitumie vitisho  wakati wanapokuwa wanatafuta habari kwani kunaweza  kuwafanya  usalama wao  ukawa  hatarini  pia waepuke  kuwa washabiki wa  chama  cha siasa  kunawafanya washindwe kuaminiwa na kujengewa  chuki  kwenye  jamii.

Katibu wa  Club  ya  Wandishi  wa Habari Mkoa wa Katavi  Pascal Katona amesema    midahalo  hiyo walioifanya  imefanya   kuwepo na  uwelewa  mkubwa  zaidi wa  utendaji kazi kwa  wandishi wa habari na polisi  hasa  kwenye  maeneo yanayohusu  usalama .

Amesema    ushirikiano huu  ulipo  hautakuwa  umeishia  kwenye  midahalo hiyo  tuu bali utakuwa  endelevu kwani jeshi la Polisi na wandishi wa habari ni watu walikaribu   katika  utendaji wao wa kazi na  ameishukuru UTPC kwa kuona  umuhimu wa kuwaletea  midahalo hiyo mitatu kwenye  Mkoa wa Katavi .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages