AGIZO LA RC KATAVI WANAODAI FEDHA MRADI WA MAJI KATAMBIKE MKADARASI AJITOKEZA KULIPA.

Mkurugenzi wa Kampuni ya ukandarasi ya Plancon (T) Limited,Othman Dunga akizelezea jinsi alivyopokea maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko ambapo amesema ujenzi wa mradi wa maji Katambike utagharimu fedha Mil 780.

Na George Mwigulu, Nsimbo.

MKANDARASI wa Kampuni ya Planco (T) Ltd ameanza kuchukua hatua za kuhakikisha analipa madai ya fedha ya zaidi ya milioni tatu kwa vibarua ambao walichimba mitaro kwenye ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Katambike Kata ya Ugalla halmashauri ya Nsimbo wilaya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko wakati akikagua ujenzi wa mradi wa maji Katambike wakati wa ziara ya kikazi aliyofanya Feburary 16,2024 aliyoifanya halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda.

Hatua hizo ni matokeo chanya ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko aliyoifanya Feburary 16,2024 katika halmashauri hiyo ya kukagua ujenzi miradi ya maendeleo ambapo wakati akisikiliza kero za wananchi suala la ucheleweshaji wa malipo ya fedha kwa vibarua yalitolewa kwake.

Mrindoko alichukua hatua ya kutoa maagizo kwa kampuni Planco (T) Ltd kuhakikisha ndani ya siku saba inalipa fedha ya vibarua na ifikapo mwenzi wa nne mwaka huu ujenzi wa mradi wa maji Katambike unakamilika kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wanaopata tabu ya maji kwa muda mrefu.

Othman Dunga, Mkurugenzi wa kampuni akisema ofisini kwake leo February 18 amekili kupokea agizo hilo na amechukua hatua tayari za haraka za kuhakikisha malipo hayo yanafanyika.

Mkurugenzi huyo ametoa tangazo tayari kwa vibarua wote wa ndani na nje ya mkoa waliofanya kazi ya kuchimba mitaro kuhakikisha ifikapo siku ya alhamisi Febuary 22, 2024 wanafika kwenye eneo la mradi Katambike kwa ajili ya kuanza kufanya malipo.

“Ni kweli kampuni yangu inadaiwa na vibarua kwa bahati mbaya walio wengi baadhi yao wako nje ya mkoa wa Katavi walikuja kufanya kazi na wakaondoka kwahiyo ili waweze kulipwa tumetoa agizo na tumeshawapa taarifa wafike siku ya alhamisi kwenye site Katambike ili kila moja aweze kupata haki yake” Amesema.

Asisitiza kuwa watapima kila sehemu ambayo kiabarua amefanya kazi kwa ajili ya kila mmoja alipwe fedha kutokana na kazi alizozifanya na kwamba agizo la Mkuu wa Mkoa halina tatizo na  litatekelezwa kama jinsi alivyoagiza.

Baadhi ya maafisa wa Mkoa wa Katavi wakiwa wameambatana na Mkuu wa Mkoa Mwanamvua Mrindoko alipotembelea mradi huo.


Dunga amebainisha licha ya mkataba wake wa ujenzi wa mradi wa maji Katambike unamwelekeza kuhakikisha ifikapo mwenzi wa nne mwaka huu kuwa amemaliza ujenzi huo lakini kwa juhudi anazofanya mradi huo utakamilika mwenzi wa tatu.

“Namwakikishia Mkuu wa Mkoa wa Katavi na wananchi wa kijiji cha Katambike na Kata ya Ugalla  kwamba mradi huo utakamilika ndani ya mwenzi ujao wa tatu na wananchi wote watapata huduma ya maji.Sasa tunachofanya kampuni ipo kazini na mimi sitaondoka na sijaondoka mkoani Katavi hadi mradi huu ukamilike” Amesema.

Katika hatua nyingine amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kazi nzuri ya kufuatilia utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) wa ujenzi wa miradi katika mkoa wake kwa kuwa ni wajibu wake na anaifanya kazi hiyo kwa ukaribu sana.

“Nichukue fura hii kumshukuru rais Dk Samia Suluhu Hassain kwa kazi nzuri ya kumwaga miradi mingi kwenye nchi nzima na kutupatia fursa nzuri wakandarasi kuweza kutumia fursa hiyo na serikali kuendelea kuwaamini wakandarasi wa ndani” Amesema Dunga.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko anaendelea na ziara yake katika mkoa huo ambapo amekuwa akikagua utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoa huo na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages