Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akiwa hutubia wajumbe kwenye kikao hicho
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Katavi (RCC) imepitisha mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kuu na Halmashairi zake zote tano za Mkoa huu ikiwa imelenga kutatua kero mbalimbali za wananchi na kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo .
Wajumbe mbalimbali wakiwa katika kikao hicho cha Kamati ya ushauri Mkoa wa Katavi.
Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Katavi (RCC) imepitisha mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kuu na Halmashairi zake zote tano za Mkoa huu ikiwa imelenga kutatua kero mbalimbali za wananchi na kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo .
Mapendekezo hayo ya Bajeti ya msimu wa fedha wa 2024/2035 yamepitishwa na kikao hicho cha RCC kilichofanyika katika ukumbi ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko .
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua
Mrindoko amewaambia wajumbe wa Kikao hicho
cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Katavi kuwa Mkoa
wa Katavi umeomba kuinidhishiwa Bajeti ya kiasi
cha Shilingi Bilioni 126 ambapo bajeti ya
msimu uliopita ilikuwa ni kiasi cha shilingi
Bilioni ` 116 bajeti ya msimu huu ukiwa
imeongzeka la asilimia saba sawa na
ongezeko la asilimia sita
Mrindoko amewweleza wajumbe wa kikao hicho kuwa kwa kipindi cha miaka miwili Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika Mkoa wa Katavi kwa kuhakikisha fedha za kuleta maendeleo kwenye Mkoa huu zinapatikana .
Na katika kipindi hiki cha miaka
miwili ameweza kuleta kiasi cha zaidi
ya shilingi Bilioni 818 kwenye
sekta mbalimbali zilizopo katika Mkoa
huu vikiwemo sekta za uchukuzi , afya
,kilimo , maji barabara ,elimu na
nyinginezo .
Amebainisha kuwa fedha
hizo zimeweza kusaidia sana kwa kuweza
kuongeza huduma mbalimbali kwa wananchi na kupunguza
baadhi ya kero zilizokuwepo .
Kikao hicho cha RCC Mkoa wa Katavi kimepitisha mapendekezo ya kuanzisha Wilaya mpya ya Mpimbwe na Jimbo jipya la Karema pamoja na Kata mbalimbali na vitongoji ,Mitaa na Vijiji.