Emanuel Sanka Mrajisi Msaidizi na tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania akiwa hutubia wajumbe wa kikao hicho. |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Wakulima wa Tumbaku wanaotumia viuatilifu visivyokubalika
kwenye zao la Tumbaku wameobwa kuachakufanya hivyo kwani wanahatarisha soko la
Tumbaku Duniani kunakoweza kusababisha Tumbaku ya Tanzania kukosa soko la
Tumbaku kimataifa.
wajumbe wa mkutano mkuu wa 30 wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Katavi Lactu wakiwa kwenye mkutano wao ulifanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda wakijadili mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya ushirika wao
Wakulima wa Tumbaku wanaotumia viuatilifu visivyokubalika kwenye zao la Tumbaku wameobwa kuachakufanya hivyo kwani wanahatarisha soko la Tumbaku Duniani kunakoweza kusababisha Tumbaku ya Tanzania kukosa soko la Tumbaku kimataifa.
Wito huu umetolewa
na Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika
cha Wakulima wa Tumbaku Mkoa wa Katavi (LATCU ) Pius
Killo wakati wa mkuu tano mkuu wa 30 wa Chama
hicho uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda .
Amebainisha kuwa
wapo baadhi ya wakulima wa zao la Tumbaku
wanahatarisha soko la Tumbaku kwenye masoko ya
Kimataifa kwa kutumia viatilifu ambavyo
havitakiwi kutumiwa kwenye zao hilo kama vile
viatilifu vya kuua Mbu .
Amewasisitiza wakulima
kuacha kudanganywa na wafanya biashara wanaouza
pembejeo za kilimo ambazo baadhi ya viatilifu hivyo havisitahili
kutumika kwenye zao la Tumbaku .
Killo ameeleza
kuwa hali ya uzalishaji wa zao la Tumbaku katika
Mkoa wa Katavi imekuwa ikiongezeka kutokana na Serikali
kufanya kazi kubwa ya kufungua masoko tofauti na
hali ambayo iliyokuwepo hapo nyuma ya wakulima kukosa
masoko ila kwa sasa masoko ni ya uhakika mkulima hana
kisingizio tena bali ashindwe mwenyewe .Emanuel Sanka Mrajisi Msaidizi na tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania akiwa hutubia wajumbe wa kikao hicho.
Amefafanua kuwa
kwa msimu wa kiliomo 2022/2023 wakulima wa zao la
Tumbaku wa Mkoa wa Katavi wamezalisha kilo 11,150,776 zenye
thamani ya Dola za Kimarekani zaidi ya Milioni 25.9
ambapo kwa msimu huu wa Kilimo wa 2023/2024 wamepanga
kuzalisha kilo Milioni 20.
Kuhusu pembejeo za
kilimo amesema kuwa msimu huu
mbolea za Tumbaku zimefika kwa wakati tofauti na huko nyuma
ingawa hadi sasa changamoto walionayo wakulima ya
vifungashio aina ya nyuzi aina ya
Jute twine na New Hessian cloth.
Killo
ameiomba Serikali katika kipindi hiki cha
kuelekea kwenye msimu huu wa ununuz wa Tumbaku
wawasaidie wakulima kwa kuboresha miundo mbinu ya
barabara zilizoharibika kutokana na mvua za msimu
huu ili kuweza kumwezesha mkulima kuweza
kusafirisha tumbaku yake kupeleka kwenye soko bila
shida na kumfanya aweze kuuza kwa wakati .
Amesema kwa sasa
katika Mkoa huu unayomakampuni matatu ya ununuzi
wa zao hili ambayo ni Premium Active Tanzania
Limeted ,Mkwawa Leaf Tobacco L td na
Obamco Tobacco Ltd .
Nae Mrajisi Msaidizi wa vyama ushirika na tume ya Maendeleo ya ushirika Tanzania Emanuel Sanka amesema kuwa zipo taarifa za baadhiya vyama vinatumia viatilifu visivyokubalika kwenye zao hilo jambo ambalo ni hatari kwenye soko la Tumbaku nchini .
Amefafanua kuwa
soko la Tumbaku linamwongozo yake na lina
takiwa kukidhi matakwa ya Kimataifa ikiwa
na pamoja na kutumia pembejeo
zinazokubaliwa na Halmashauri ya Tumbaku Tanzania
Amesisitiza kuwa juhudi
zilizofanyika na serikali za kutafuta masoko ya Tumbaku haziwezi kukamishwa na
watu wachache wasiofuata taratibu.
Sanka amesema kwa sasa zoezi la upandaji miti ngazi ya AMCOS bado hairidhishi hivyo alitowa ushauri kwa kamati ya Mkoa inayokagua miti itengeneze mpango wa kuhakikisha miti inayooteshwa kwenye vitalu inapandwa mashambani na inafatiliwa mpaka inakuwa na kusitawi .
Sanka ameipongeza
Latcu Ltd kwa namna inavyoendelea
kutimiza majukumu yake kwa kuzingatia sheria
ya vyama vya ushirika Namba 6 ya mwaka 2013
na kanuni zake za mwaka 2015 pamoja na miongozo mbalimbali
waliojiwekea .
Nae mkulima wa zao
hilo Mohamed Said ameiomba Serikali iwaangalie na
wakulima wa zao la Tumbaku kwa kuwapatia mbolea ya
ruzuku kama ilivyo kwa wakulima wa zao la mahindi .
Nae Fibelti
Ngula Makamu Mwenyekiti wa Latcu
amesema kumekuwepo na changamoto ya baadhi ya wakulima
kuchanganya tumbaku wakati wa masoko kwa kuweka tumbaku
chafu hali ambayo imekuwa ikihalibu soko la
tumbaku .
Chama kikuu cha ushirika
lactu cha Mkoa wa Katavi kinajumla ya Wananachama 18 Amcos zinazolima zao la
Tumbaku ambavyo vimekuwa mhimili wa kuchangia Mapato kwenye Halmashauri husika.