DC :JAMILA ONGEZEKO LA BAJETI ISHARA YA MAENDELEO KWENYE HALMASHAURI

 

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akizungumnza katika kikao  cha Kamati ya ushauri Wilaya ya Mpanda maalumu kwaajili ya Kupitisha Rasimu ya Bajeti 2024/205 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmahauri ya Wilaya ya Nsimbo. 

Na Paul Mathias-Mpanda

Serikali katika Wilaya ya Mpanda imesema ongezeko la Bajeti katika Halmashauri zake inaonyesha ishara ya ukuaji na ongezeko la ukusanyaji wa Mapato ili kuwahudumia wananchi kupitia Miradi mbalimbali.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mpanda Josep Lwamba wa Pili [kushoto] akiwa na viomgozi mbalimbali katika kikao hicho.

Serikali katika Wilaya ya Mpanda imesema la Bajeti katika Halmashauri zake inaonyesha ishara ya ukuaji na ongezeko la ukusanyaji wa Mapato ili kuwahudumia wananchi kupitia Miradi mbalimbali.

Akiwahutubia wajumbe wa Kikao maalumu cha Kamati ya ushauri ya Wilaya ya Mpanda kuhusu Rasimu ya Bajeti kwa 2024/2025 kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Jamila amsema ongezeko hilo la Bajeti kwenye halmashauri hizo litakuwa na tija katika kuwatumikia wananchi.

‘’Nizipongeze Halmashauri zote mbili kwenye bajeti zao utaona Halmashauri zote zimepiga hatua tofauti na bajeti ya Mwaka uliopita hongereni kwa jitihada hizo mlizozifanya kwa kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la bajeti’’ amesema Jamila.

Wajumbe mbalimbali wakiwa katika kikao hicho cha Kamati ya Ushauri Wilaya ya Mpanda.

Ameeleza kuwa niwajibu wa kila halamshauri kuhakikisha bajeti iliyopo inatekelezwa kwa asilimia miamoja pamoja na kuhakikisha Rasimu ya Bajeti iliyopitishwa ya Mwaka 2024/2025 inatkelezwa kwa kiwango kinachotakiwa.

‘’ Rasimu ya bajeti tuliyoipitisha hapa itakapo rudishwa niwajibu wa Halmashauri kuhakikisha malengo ya bajeti yanafikiwa nilazima kujidhatiti kwenye eneo hilo la ukusanyaji wa Mapato pamoja na kutdhibiti matumizi yake na matumizi yalenge manufaa kwa wananachi wetu zile asilimia ambazo zinatakiwa kurudi kwa wananchi ziludi kwa wakati ili kutatua kero za wananachi’’ amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.

Katika hatua nyingine amemshuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan namna ambavyo amekuwa akileta fedha nyingi za miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Mpanda katika sekta mbalimbali ikiwemo afya elimu miundombinu na Kadhalika.

Leonard Kilamuhaa Kaimu afisa Idara ya Mipango akiwasilisha Rasimu ya Bajeti katika kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda.

‘’Tumeona hapa kwenye Vitabu vya Bajeti kuanzia mwaka 2022/2023 tumepokea fedha za kutosha za maendeleo kwa halmashauri ya Nsimbo Bilioni 11 Manispaa ya Mpanda Bilioni 4 zaidi ya kile ambacho walikuwa wamekusudia hizi nikwaajili ya maendeleo tu hakuna eneo ambalo halijaguswa katika fedha hizi za maendeleo amabazo Rais amekuwa akituletea kwenye Wilaya yetu ya Mpanda.’

Leonard Kilamuhaa Kaimu Idara ya Mipango Manispaa ya Mpanda akiwasilisha Rasimu ya Bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda amesema Halmashauri hiyo imepanga kukusanya na kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 27.5

Edger Mnyavanu Mkuu wa Idara ya Mipango na uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo akiwasilisha Rasimu ya Bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.

‘’Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji  wa Manispaa ya Mpanda naomba kuwasilisha kwako mapendekezo ya Mpango na Bajeti kwa 2024/2025 yenye jumla ya Shilingi Bilioni 27.5 ikiwemo matumizi ya kawaida Bilioni 19 na miaradi ya Maendeleo Bilioni 7.9 naomba kuwasilisha’’ amesema Kilamuhaa.

Kwa upande wake Edger Mnyavanu  Mkuu wa Idara ya Mipango na uratibu Halmashauri ya Nsimbo akiwasilisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema halmashauri hiyo kwa mwaka 2024/2025 imepanga kukusanya na kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 26 .889.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph [kushoto] akijadili jambo na Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli kwenye kikao hicho.

Haidary Sumry Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda pamoja na Charles Halawa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa pamoja wamesema kuwa Rasimu ya Bajeti iliyopendekezwa kwa kiasi kikubwa imelenga kwenda kutatua kero za wananchi.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kupitisha Rasimu ya Bajeti kwa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo pamoja na kupendekeza kuongezwa kwa maeneo ya utawala kweye Halmashauri hizo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages