Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Seka Urio akizungumnza katika Hafla ya kutoa Bati 200 katika Kijiji cha Kapanda kwaajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Kapanda. |
Na Walter Mguluchuma-Mpanda
Benki ya NMB imetoa msaada wa bati 400 zenye thamani
ya zaidi ya shilingi milioni 13 kwa ajiri ya ujenzi
wa Shule mbili za Msingi katika Halmashauri
ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi
ikiwepo shule ya Msingi Kapanda ambayo wanafunzi wake
280 wa kuanzia darasa la awali hadi darasa la tatu wanasoma
kwa kutumia jengo la Kanisa ikiwa ni kuunga mkono
jitihada za kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita ya
kusimamia upatikanaji wa elimu bora .
Benki ya NMB imetoa msaada wa bati 400 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 13 kwa ajiri ya ujenzi wa Shule mbili za Msingi katika Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi ikiwepo shule ya Msingi Kapanda ambayo wanafunzi wake 280 wa kuanzia darasa la awali hadi darasa la tatu wanasoma kwa kutumia jengo la Kanisa ikiwa ni kuunga mkono jitihada za kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita ya kusimamia upatikanaji wa elimu bora .
Awali kabla ya kukabidhiwa kwa msada huo Diwani wa Kata ya Machimboni Raphael Kalinga alieleza kuwa shule ya Msingi Kapanda iliyokabidhiwa msaada huo wanafunzi zaidi ya wanafunzi 280 wa kuanzia darasa la awali hadi la tatu wanasoma shule kwenye jingo la kanisa ambalo hutumiwa pia kwa ajiri ya ibada kijijini hapo .Msaada huo wa
bati hizo umekabidhiwa na Meneja wa NMB
Kanda ya Magharibi Seka Urio katika hafla
ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Vijiji
vya Kapanda Kata ya Machimboni na katika Kijiji
cha Masewela Kata ya Ibindi
Amebainisha
kuwa NMB walipokea maombi kutoka
katika Halmashauri ya Nsimbo ya kuchangia maendeleo ya
elimu na walifarijika kupokea maombi hayo na
ndipo walipo amua mara moja kuweza kushirikiana
na Halmashauri hiyo ili kuwa chachu ya maendeleo ya
sekta ya elimu kwa jamii.
Amesema jumla ya thamani ya vifaa ambavyo wameweza
kukabidhi kwa shule hizo mbili ni bati 400
yenye thamani ya shilingi 13,400 ambapo shule ya
Msingi Kapanda imekabidhiwa bati 200 yenye
thamani ya shilingi 6,700,000 na shule ya Msingi
Masewela bati 200 zenye thamani ya shilingi
6,700,000.
Meneja huyo amaesema Wanatambua juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkk Samia Suluhu Hassan za kusimamia upatikanaji wa elimu bora kwa nguvu zote kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu bora kwa nguvu zote kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma hizi mjini na vijijini .
Seka
ameeleza kuwa pamoja na makubwa
mengi yaliofanywa na Serikali NMB
kama wadau wanao wajibu wa kuunga mkono
juhudi hizi maendeleo kwa kusaidia jamii
kwani jamii ndio wanaifanya NMB
kuwa hapa ilipo na kuwa kubwa
kuliko benki yoyote ili hapa nchini .
Vifaa hivyo
walivyotowa kwa Halmashauri hiyo ni moja wa
ushiriki wao katika maendeleo ya jamii na
wao kama benki inayoongoza Tanzania hivyo
wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka
inafaidika kutokana na faida walioipata .
Amefafanua
kuwa kwa miaka kadhaa NMB
imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa
wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya
elimu na afya na kusaidia kwenye
majanga yanapokuwa yametokea kwa kutambua wateja wao
wengi wanatoka kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida
kwenye jamii wao ni utaratibu wao .
Ameeleza kuwa
NMB wamekuwa wakipokea maombi mengi sana ya
kuchangia katika miradi ya jamii lakini
benki hiyo imejikita zaidi katika
maeneo ya elimu ,afya na misaada ya hali
na mali katika nyakati ngumu kama za matokeo
ya majanga .
Seka amesema Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida kwa jamii na wamekuwa wanafanya hivyo kwa zaidi ya miaka miaka saba sasa mfululizo kwa kutenga asilimia moja ya faida yao kama sehemu ya kwenye jamii inayowazunguka .
Mbunge wa
Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe
ameishukuru Nmb kwa kuweza kuwatowa msaada huo kwa
shule hizo mbili kwa kutambua mahitaji hayo
kwenye shule hizo kwa kuwa sehemu ya kumuunga mkono
Rais Samia katika kuboresha miundo mbinu ya elimu .
Alisema watoto
wanao soma kwenye kijiji hicho mazingira sio
mazuri sana ambayo yalikuwa yakiwafanya wanapofikia
darasa la nne kwenda kusoma
kwenye shule nyingine zilizombali na kijiji hicho ndio
maana wananchi wakaamua kujenga shule kijijni hapo ambayo imepewa
msaada huo wa bati na NMB.
Amesema majengo yaliyojengwa
shuleni Kapanda yote saba na vyumba vya viwili vya walimu ni nguvu
ya wananchi lengo kubwa la kujenga majengo hayo
ya shule ni watoto kubaki kwenye mazingira ya Kijiji
kwa sababu kutoka kijiji kimoja kwenda kijiji
kingine umbali ni mrefu .
Lupembe amesema yeye kama Mbunge amekuwa akitowa fedha za mfuko wa jimbo kwa kununua vifaa vya ujenzi kwenye shule ya Kapanda ambayo imekabidhiwa msaada wa bati 200 na benki ya NMB ambayo imetowa msada huo pia kwa shule ya Masewela .
Diwani wa Kata
ya Machimboni Raphael Kalinga alisema
wanaishukuru Nmb wa kuwapatia msaada wa
bati kwa ajiri ya shule ya Msingi Kapanda ambayo
wanafunzi wake wa kuanzia darasa la awali hadi la tatu wanasomea kanisani
.
Ameiomba
Halmashauri ya Nsimbo kupoleka fedha za
kuenzekea paa ya majengo ya shule hiyo ili
bati walizopewa na NMB ziweze kuenzekea
majengo hayo ili watoto wanaosomea kwenye jingo
la ibada la Kanisa watoke na wahamie kwenye shule
hiyo.