Mwanamvua Mrindoko Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizungumnza na waandishi wa Habari ofisini kwake |
Na Walter mguluchuma-Katavi
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza Wakuu wa
Wilaya za Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanafatilia na
kuthibiti bei ya Sukari elekezi iliyopangwa kuuzwa
Mkoa wa Katavi inauzwa kwenye maeneo yote .
Baadhi ya waandishi wa Habari mkoa wa Katavi wakiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanafatilia na kuthibiti bei ya Sukari elekezi iliyopangwa kuuzwa Mkoa wa Katavi inauzwa kwenye maeneo yote .
Mkuu wa
Mkoa ametoa maagizo hayo wakati alipokuwa akitowa taarifa
mbele ya wandishi wa habari ofisini kwake juu ya hali ya upatikanaji
wa sukari ndai ya Mkoa huu ambapo hadi sasa hakuja tokea hali
ya upungufu wa sukari .
Amebainisha kuwa
hadi sasa Mkoa umepokea sukari ya kutosha ambapo kwa kipindi cha mwezi
mmoja na nusu wamepokea tani 244 za sukari na zipo kwa
wasambazji wakubwa wawili na tayati zimeisha anza kuuzwa kwa
wafanya biashara wengine.
Amesema kuwa kwa kipindi hiki hawatarajia mwananchi kukosa sukari dukani na pia hawatarajia mfanya biashara yoyote wa reja reja kukosa bidhaa ya sukari dukani kwake .
Mrindoko ameeleza kuwa sukari hii inatolewa kwa utaratibu
ambapo Serikali imeisha lipia kodi na ndio maana imeweka bei elelezi kwa
kupitia walaka wa GN ya Serikali namba
40 A na B ya tarehe 23 ya mwezi
Januari 2024 na kwa mujibu wa GN hiyo bei elekezi
ya Sukari kwa Mkoa wa Katavi kwa reja reja ni
kati ya tshs 2,900 na tshs 3200 kwa kilo moja ya sukari na
bei hiyo inauzwa kwa Mkoa mzima bila kujali yuko Wilaya gani .
Kwa hiyo bei
hii elelezi kwa mapenzi yake makubwa kwa
wananchi Rais Samia Suluhu Hassan ameisha ilipia
kodi na ndio maana kukawa na walaka elekezi ambayo haita
husisha maswala ya kodi na hasa kwa mlaji wa
mwisho ambae ni mwananchi .
Amesisitiza kuwa
wafanyabiashara wakubwa wanaosambaza sukari wahakikishe
wanapouza wazingatie bei elelezi na wanapouza lazima wauze kwa
wafanya biashara wa rejareja ambao wanaleseni za biashara na
pia wakati wa kuuza na kununua wazingatie sheria za Serikali na
kutowa resiti wakati wa mauzo .Bidhaa ya sukari ikiwa inashushwa katika mkoa wa Katavi kwaajili ya kupunguza tatizo la uhaba wa sukari
Amewaagiza wafanya
biashara wote wa rejareja kuhakikisha wanauza bei elekezi ya
sukari kwa kilo moja kwa tshs 2.900 na 3,200 na kwamaana hiyo
anapiga marufuku katika Mkoa wa Katavi sukari kuuzwa
kwa zaidi ya bai hiyo hivyo wananchi wanunue kwa kuzingatia bei hiyo na
sio zaidi ya hapo .
Kwa hiyo vyombo
vya dola katika Mkoa wa Katavi wamekuwa wakipita kila maeneo
kuona kama kuna mtu ambae amekiuka maelelezo hayo
ya Serikali na ndio maana siku ya juma tano tarehe 28 mwezi huu wa
pili wamewakamata wafanya biashara wa rejareja wakiuza sukari kwa bei ya
juu ya elekezi na tayari hatua mbalimbali za kisheria
zimechukuliwa na serikali ya Mkoa wa Katavi haitachoka
iwe mchana au usiku wakipata taarifa ya mfanya biashara kuuza bei
ya juu watamkamata tuu.
Amewagiza wakuu wa Wilaya zote za Mkoa huu kupitia kamati zao za usalama kuhakikisha wanafatila na kudhibiti bei elelezi ya sukari ndio inayouzwa kwenye maeneo yao yote .
amewataka viongozi dola ngazi ya Mkoa pamoja
na ngazi ya Wilaya Tarafa Kata na
Vijiji pamoja mtaa washirikiane kusimamia jambo
hili na kuhakikisha sukari inafika kwa wananchi na inauzwa katika
bei elelezi .
Nae Salome
John Mkazi wa Mtaa wa Kawajense amesema
kuwa hari ya upatikanaji wa sukari kwenye maduka yalipo
kwenye mtaa wake ni yakuridhisha kwani haja wahi kufika
dukani anapokuwa anahitaji sukari na kukosa muda wote sukari ipo .
Kwa upande wake Michael Lumalisha mkazi wa Mtaa wa Majengo amebainisha kuwa yeye changamoto ya sukari amekuwa akiisikia tuu kwenye vyombo vya habari kwenye baadhi ya Mikoa lakini kwa Mkoa wa Katavi hajawahi kusikia kuwepo na changamoto hoyo kwani sukari muda wote inapatikana.