Mkuu wa mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumnza na waandishi wa Habari ofisini kwake.
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza Makamanda wa Jeshi la Polisi na Magereza wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanamchukulia hatua mfungwa anae tuhumiwa kufanya kitendo cha ukatili cha kumbaka mtoto wa miaka 13 .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi wa kwanza Kushoto akiwa na maafisa wa Magereza wakisikiliza maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewaagiza Makamanda wa Jeshi la Polisi na Magereza wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanamchukulia hatua mfungwa anae tuhumiwa kufanya kitendo cha ukatili cha kumbaka mtoto wa miaka 13 .
Agizo hilo amelitowa leo wakati aliokuwa akizungumza na Wandishi wa Habari ofisini kwake kuhusiana na tukio lililotokea wiki iliyopita la mfungwa mmoja wa Gereza la Kilimo la Kalilankulunkulu kudaiwa kumbaka msicha wa miaka 13 jina limehifadhiwa wakati alipokuwa akitoka shambani kupanda mpunga .
Mrindoko alisema kama ambavyo ilivyotararibu za
sheria ilivyo kwa mtu yeyote ambae atakae
husika katika kufanya tukio lolote la ubakaji
bila kujari cheo hali yake na umri wake ni
lazima sheria zichukuwe mkondo wake .
Amesema tukio hili limeisikitisha
Serikali ya Mkoa wa Katavi kwani jambo hili
limemuhisisha mfungwa ambae alikuwa kwenye
chombo cha dola hivyo jambo hili linashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria .
Amesema kumekuwepo na tahaluki juu ya tukio la mtoto ambae jina
limehifadhiwa Mkazi wa Kijiji cha Kawanzige ambae
anadaiwa kubakwa na mfungwa wa gereza hilo mnamo tarehe
29 mwezi wa pili ambapo kwa sasa tukio hilo
linafanyiwa kazi na vyombo vya Dola .
Mkuu huyo wa Mkoa wa Katavi anamwagiza Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Katavi na Mkuu wa Magreza
wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanamchukulia hatua
aliyehusika kufanya kitendo hicho cha kikatili .
Amewaondoa mashaka wananchi ambao wamekuwa na mashaka
kuwa jambo hilo linaweza lisishughulikiwe amewahakikishia wananchi kuwa jambo hili litashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria za nchi na wala hakutakuwa na upendeleo
wowote ule wala kitu ambachokitakacho fichwa jambo
hilo anahakikisha linashughulikiwa kwa sheria kwa ailimia mia moja
.
Amesisitiza kuwa swala hili litashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria na taratibu jambo hili lipo kwenye mikono ya
sheria na linashughulikiwa kama ambavyo
linavyoshughulikiwa likitokea kwenye sehemu nyingine.
Aliwaomba wazazi na jamii ya wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa
kuwa matukio ya ubakaji yamekuwa yakilipotiwa lakini
kumekuwa na tabia ya wazazi wanapotakiwa kwenda kutowa ushahidi
Mahakamani wamekuwa hawaendi na matokeo yake wamekuwa
wakisababisha watuhumiwa kuachiwa huru .
Amewaomba wazazi wa na walezi ktoa ushirikiano wa ushahidi pindi kesi hizo zinapokuwa zinaendelea katika vyomo vya kutoa haki.