TANROADS KATAVI WATEKELEZA MIRADI YA ZAIDI YA BILIONI 400 KWA KIPINDI CHA AWAMU YA SITA

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende akielezea utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya Kitaifa inayotekelezwa katika mkoa wa Katavi kupitia serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha Miaka mitatu.

 Na Walter Mguluchuma-Katavi

Wakala wa  Barabara  Tanzania (TANROADS)  Mkoa  wa  Katavi  kwa  kipindi  cha  miaka   mitatu ya  uongozi wa  awamu ya sita  inayoongozwa  na Rais   Dkt  Samia  Suluhu  Hassan  wanatekeleza   miradi    nane ya  ya kimkakati ya  Kitaifa   yenye    zaidi ya   shilingi    zaidi ya  Bilioni 400.

Mkuu wa Kitengo cha Matengenezo ya Barabara TANROADS Mkoa wa Katavi Mhandisi Albert Laizer akielezea namna ambavyo TANROADS wanavyosimamia matengenezo ya Barabara na Madaraja hali inayofanya Barabara zipitike kipindi cha mwaka mzima.

Wakala wa Barabara  Tanzania (TANROADS)  Mkoa  wa  Katavi  kwa  kipindi  cha  miaka   mitatu ya  uongozi wa  awamu ya sita  inayoongozwa  na Rais   Dkt  Samia  Suluhu  Hassan  wanatekeleza   miradi    nane ya  ya kimkakati ya  Kitaifa   yenye    zaidi ya   shilingi    zaidi ya  Bilioni 400.

 Hayo yamesemwa  na  Meneja wa  TANROADS Mkoa wa  Katavi  Mwandisi  Martini  Mwakabende  wakati alipokuwa akitowa  taarifa ya  utekeleza wa  miradi  wa shughuli  za utekelezaji wa  miradi ya   ya kimkakati inayoendelea kutkelezwa  katika  Mkoa huu mbele ya wandishi wa  Habari .

Mwandisi  Mwakabende  amesema  katika  kipindi cha  uongozi wa  Rais wa  awamu ya  sita  Dkt  Samia   Suluhu Hassan   Wakala wa  Barabara  Tanzania (TANROADS)Mkoa wa  Katavi  wanatekeleza  miradi  8 ya kimkakati ya  Kitaifa   yenye  jumla ya shilingi   Bilioni 410.81.

Ambapo  miradi  hiyo itakapokuwa imekamilika yote  itaufanya  Mkoa wa  Katavi  kuwa  na   mtandao wa  barabara   zenye  kiwango cha lami   zitakuwa  na  urefu wa kilometa  548.45kwa  Mkoa  mzima huu.

Amesema  TANROADS  Mkoa  wa Katavi wanapongeza  juhudi kubwa  za  Serikali ya  awamu ya sita  kwa kukamilisha  ujenzi kwa kiwango  cha  lami kwa   barabara  ya  Mpanda   hadi Tabora   pamoja na kuanza kwa ujenzi wa   lami  kwa  barabara za  Vikonge  Luhafwe yenye  urefu wa kilomata  25, hadi  Mishamo Kilometa  kilometa  37.35.

Amezitaja  barabara  nyingine kuwa ni  Kibaoni  hadi  makutano ya  Mlele   kilometa 50   Kagwira   hadi Karema  kilometa 110.29 pia  wanamiradi ya    lami katika   miji  kwa  ujenzi wa  kiwango cha  lami  katika   miji ya  Mapili  kilomita   Mbili ,  Ilunde  kilometa  nne   Maji  Moto   kilometa  2.5  Usevya kilometa  4.13 Kawajense  kilometa  3  na   Mpanda  hadi airport  kilometa  tatu  nakufanya jumla ya kilometa  18.73 walizoweka  kwenye  maeneo ya  miji .

Kuhusu  taa za  barabarani  wameweza  kuweka  jumla ya taa  719 sawa  na  asilimia 77  zenye  thamani ya  shilingi Bilioni 2.4  zimewekwa  na kufanya  Mkoa wa  Katavi  kuwa na taa  za  barabarani   jumla 932  zenye  thamani ya   Shilingi  Bilioni 2.9.

Mkuu wa  Kitengo cha  matengenezo ya  Barabara   TANROADS   Mkoa  wa  Katavi  Mwandisi Albert   Raizer  amesema  hali ya  barabara kuu kwa  ujumla  ni nzuri na  zinapitika    vipindi vyote  na  barabara  za  Mkoa  zinapitika  katika  kipindi chote  cha mwaka .

Raizer  amefafanua kuwa  TANROADS  M koa wa  Katavi  wameendelea  kupokea  kupokea  fedha  kutoka  Serikalini   kwa  ajiri  ya  ukaguzi  wa   madaraja  na  kuhakikisha  kuwa  barabara  zinapitika  kwa muda wote .

 Kuhusu  ujenzi wa  madaraja   amesema  shughuli za  ujenzi    yote ya  miradi ya  madaraja  imekuwa ikifanywa na wakandaeasi wazawa   chini ya  usimizi wa Tanroads na wameweza kusimamia   ujenzi wa  madaja makubwa  kama yafuatayo  Daraja  la Mirumba   lenye  urefu wa mita 42 60, ujenzi wa  daraja  la  mto Rugufu mita 42, na  ujenzi wa  mto  Kavuu

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages