HUDUMA YA KUSAFISHA DAMU KUANZA HIVI KARIBUNI KATAVI.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko [katikati] akioneshwa mchoro wa ramani ya jengo la kusafisha Damu litakalojengwa katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi. Picha na Paul Mathias

 Na Walter Mguluchuma-Katavi

Wananchi  wa  Katavi wanaondokana na   changamoto  ya adha waliokuwa  nayo ya kusafiri umbali  mrefu na wengine kuhamisha  makazi kwenda  katika Mikoa   mingine   kutafuta huduma ya usafishaji wa  damu  baada ya  Hospitali ya Mkoa wa   Katavi  kupatiwa  fedha zaidi ya  shilingi  Milioni 190 kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la huduma ya usafishaji wa damu .

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi,Dk Serafini Patrice mwenye Miwani akimuonyesha Eneo mkuu wa Mkoa wa Katavi mwanamvua mrindoko ambalo litajengwa jengo la kusafisha damu 

Wananchi  wa  Katavi wanaondokana na   changamoto  ya adha waliokuwa  nayo ya kusafiri umbali  mrefu na wengine kuhamisha  makazi kwenda  katika Mikoa   mingine   kutafuta huduma ya usafishaji wa  damu  baada ya  Hospitali ya Mkoa wa   Katavi  kupatiwa  fedha zaidi ya  shilingi  Milioni 190 kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la huduma ya usafishaji wa damu .

Mkuu wa  Mkoa wa Katavi  Mwanamvua  Mrindoko  amesema   usafishaji  wa damu ni kilio  ambacho walikuwa  nacho kama  Mkoa kwa muda  mrefu  lakini  sasa  wanamshukuru sana Rais  DK Samia  Suluhu  Hassan akishirikiana na viongozi wengine  wanao usimamia Mkoa wa Katavi moja kwa  moja  kama   vile  Waziri wa TAMISEMI   na Waziri wa Afya .

Amewapongeza kwjitihada kubwa walizofanya za kuhakikisha  Mkoa  unapata  fedha   za ujenzi wa  jengo hilo ambapo  mashine  za kisasa  za kusafishia damu  zilikuwa  zimeisha  letwa katika Hospitali hiyo ila  zilikuwa hazijaanza kufanya kazi kutokana na kutokuwepo kwa jengola kutolea huduma hiyo

Mashine za kusafisha Damu zikiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Katavi huku ujenzi wa jengo hilo ukiwa unakaribia kuanza.

Mrindoko  amebainisha kuwa  kiasi cha  shilingi Milioni  196  tayari zimeisha  ingia  katika  Mkoa wa Katavi kwa ajiri ya ujenzi wa jengo hilo  na  amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa  Katavi  kuwa fedha  hizo  zitasimamiwa ipasavyo  ili kuhakikisha jengo hilo linajengwa kwa wakati kwa kuzingatia ubora na thamani ya pesa .

 Amesema  Serikali ya  Mkoa  ili   kabidhiwa  na  kuaminiwa  kujenga  na kusimamia  ujenzi wa Hospitali ya Mkoa  katika ujenzi wa kwa awamu mbalimbali na wamesimamia na wataendelea kusimamia  ili kuhakikisha kila fedha inayokuja inatimiza malengo yaliyokusudiwa .

Amesema Rais  Samia  ameendelee kuujali Mkoa wa Katavi   kwa kuendelea  kuboresha  huduma za  afya   katika Mkoa huo ambao  haukuwa  na  hospitali  na sasa  tayari  ipo imekamilikana imeanza  kufanya kazi. 

Mganga   Mkuu   mfawidhi  wa  Hositali ya Rufaa ya  Mkoa wa  Katavi Dkt  Serafini   Patrice amesema kuwa  kwa  sasa  hospitali hiyo haitowi huduma ya  usafishaji wa damu  licha ya kuwa wameishapatiwa mashine za kusafishia  damu  kutokana na kutokuwa na jengo  la  kutolea  huduma hiyo .

Amesema  kupitia   ofisi ya  Mkuu wa  Mkoa wa Katavi zimeombwa Fedha  kwa ajiri ya ujenzi wa jengo   hilo  na  wanashukuru  ofisi ya Mkuu  wa Mkoa wa Katavi  na Mbunge wa Jimbo la  Mpanda   Mjini  kwa kuweza kufanikisha   fedha kiasi cha tshs 196,000,000 ambazo  tayari  zimeisha   ingia  kwenye akaunti ya hospitali hiyo.

 Amefafanua kuwa  jengo hilo   linahitaji  kiasi cha shilingi milioni 400  lakini  fedha  hizo  milioni  196  zitaweza kujenga kwa awamu ya kwanza na huduma zikaanza kutolewa bila shida  na wanatarajia kuanza kutowa huduma kwa vitanda  sita kwa wakati mmoja  na  tayari wanazo hizo mashine sita za kuchuja damu 

Dkt Patrice  amesema   mchakato wa  ujenzi wa jengo hilo  umeisha  anza  na wanatarajia  baada ya  miezi miwili au mitatu ujenzi huu utakuwa umekamilika na huduma zitaanza kutolewa kwa wananchi   na wataondokana  na changamoto    ya kusafiri kwenda umbali mrefu kutafuta huduma hiyo .

Mbunge wa Jimbo la Mpanda  Mjini  Sebastiani Kapufi  ameishukuru  serikali kwa kuleta fedha hizo za ujenzi  kwani   ndio kilikuwa kilio kikubwa cha wananchi wa  Mkoa huu kuona huduma ya kusafisha damu inatolewa katika Hospitali  hiyo .

Amesema wananchi wengine wa Mkoa huu sasa hivi wapoMwanza, Mbeya  Dodoma  na  kwingineko  kufuata  huduma ya uchujwaji wa damu  na wanazaidi ya miaka  miwili sasa wamelazimika kupanga vyomba huko ili kupata huduma hiyo na kuziacha familia zao  kwa hiyo   huduma hiyo sasa  watarudi huku  na kuendelea kupata  huduma hiyo .

 Yeye  kama  Mbunge  anayofuraha kubwa kuona  huduma  hiyo intolewa  kwenye Mkoa huu  imekuwa ni kama ndoto  kwa jinsi ambavyo ilikuwa ni  changamoto kwa  mtu alipokuwa akiandikiwa  kwenda  rufaa kupata  huduma hiyo kwenye hospitali za  Kanda .

Meya  wa  Manispaa ya  Mpanda Haidari  Sumry amesema  kuwa Serikali  imefanya  kazi kubwa ya  kuboresha huduma za  afya  na kwa  mfano tuu  ni  wananchi wa  Mkoa huu  walikuwa wakisafiri kwenda  kwenye  mikoa mingine pia kutafuta huduma za  meno  lakini sasa  hivi  hospitali hiyo imeletewa  vifaa vya kisasa       na huduma wananchi wanapatiwa hapo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages