Uongozi wa Jeshi la Polisi na Viongozi wa vyama vya Siasa na wadau wengine wakiwa katika picha ya Pamoja na waandishi wa habari mkoa wa Katavi baada ya mdahalo huo. |
Na Paul Mathias-Katavi
Baadhi
ya wadau wa maswala ya habari katika mkoa wa Katavi wameupomgeza Umoja wa klabu
za waandishi wa Habari Tanzania [UTPC] kwa kuja na mpango maalumu wa kufanya
midahalo baina ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari kwa lengo la kudumisha
umoja na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao.
Baadhi ya wadau wa maswala ya habari katika mkoa wa Katavi wameupomgeza Umoja wa klabu za waandishi wa Habari Tanzania [UTPC] kwa kuja na mpango maalumu wa kufanya midahalo baina ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari kwa lengo la kudumisha umoja na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao.
Wadau
hao wamebainisha hayo katika Mdahalo wa Nne baina ya Jeshi la Polisi na
waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa St Mathias
Manispaa ya Mpanda.
Amani
Mahela Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanya biashara Mkoa wa Katavi akiwa katika
mdahalo huo amesema midahalo itakwenda kupunguza msuguano wa kiutendaji baina
ya waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi kwakuwa kila mmoja atakuwa ametambua mipaka ya kazi yake.
Ameeleza
kuwa tangu midahalo hiyo ianze kufanyika tangu mwaka jana imekuwa na tija
kiundendaji baina ya makundi hayo mawili katika katika kutekeleza majukumu yao.
‘’Kuna
kitu ambacho nakiona kimepadwa kizuri kimahusiano lakini pia kinaleta uhuru kwa
waandishi wa habari sababu ya midahalo hii’’ –Mahela
Edina
Buzima Katibu wa UWT Mkoa wa Katavi akimwakilisha Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi
akichangia mada katika mdahalo huo amesema waandishi wa habari ni chachu kwa
kuchochea maendeleo kupitia kuipasha habari jamii.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi wakiwa katika Picha ya Pamoja na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi na viongozi wa Siasa baada ya Mdahalo huo |
‘’Tunatambua
umuhimu wa vyombo vya habari tunashukuru kwa mdahalo huu sisi kama wadau
nawapongeza sana UTPC kwa mdahalo huu niwakumbushe tu kuzingatia swala la usawa
wa kijinsia katika masuala ya kihabari hasa katika matukio mbalimbali wapeni
nafasi waandishi hawa wa kike’’-Buzima
Kwa
upande wake David Mutasya Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi
kwa niaba ya kamanda wa Polisi mkoa mkoa wa Katavi amesema kuwa midahalo
imekuwa na tija kubwa tangu ianze mwaka jana baina ya waandishi wa habari na
jeshi la polisi katika mkoa wa Katavi.
Amebainisha
kuwa kupitia midahalo hiyo kumekuwa na utamaduni wa kubadilioshana habari baina
ya waandishi wa habari na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuendelea kuimarisha
ulinzi kwa wananchi kupitia taarifa.
Walter
Mguluchuma Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Katavi
ameushukuru Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC kwa kuona
umuhimu wa kuwezesha midahalo hiyo kufanyika baina ya waandishi wa Habari na
Jeshi la polisi.
Mguluchuma ametoa wito kwa waandishi wa habari mkoa wa Katavi kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao ili kuepusha migongano isiyokuwa ya lazima katika majukumu yao.