WAKULIMA WA TUMBAKU WACHOMEWA TUMBAKU ZAIDI YA EKARI 15 ZENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 40

Baadhi ya Tumbaku zilizochomwa kwenye Kijiji cha Mtambo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

 Na Walter Mguluchuma-Mpanda

Wakulima wa Tumbaku wa  Kijiji  cha   Mtambo  Wilaya ya  Mpanda wamechomewa zaidi ya  Ekari za 15 za Tumbaku zenye  thamani ya  zaidi ya   shilingi  Milioni 40 zilizokuwa  zimekaushwa  na  nyingine  zilizokuwa  shambani kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na Askari wa wakala wa Misitu [TFS]

Moja ya Bani la kukaushia Tumbaku lililochomwa huku wakulima wakiwa hawaelewi tumbaku yao watakaushia wapi

Wakulima wa Tumbaku wa  Kijiji  cha   Mtambo  Wilaya ya  Mpanda wamechomewa zaidi ya  Ekari za 15 za Tumbaku zenye  thamani ya  zaidi ya   shilingi  Milioni 40 zilizokuwa  zimekaushwa  na  nyingine  zilizokuwa  shambani kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na Askari wa wakala wa Misitu [TFS]

Tukio la  kinyama na  la kikatili  limetokea  hapo  tarehe  23  mwezi huu  huko  katika  eneo  la  Kijiji  cha  Mtambo  Halmashauri ya  Nsimbo  Wilaya ya  Mpanda Mkoa wa Katavi .

Paul luhanja mmoja wa wahanga wa kuchomewa  tumbaku yake  na   mabani matatu ya kukaushia  tumbaku   amesema  yeye  alikuwa amelima  ekari sita za zao la  Tumbaku   na  kati ya ekari hizo  ekali nne  zikuwa  zimevunwa  tayari  tumbaku na zilikuwa  stoo  zikisubiri soko  hata hivyo hakuweza kuokoa chochote kile  kwani zote ziliteketezwa kwa moto .

Janeth Jailos mmoja ya wakulima walioathirika baada ya Tumbaku yake kuchomwa Moto

Amesema  mbali ya kuchoma  tumbaku yake iliyokuwa  kwenye  stoo   askari hao  ambao idadi yao ilikuwa sita na walikuwa  na   silaha  mbili   bunduki  waliweza kuchoma  pia Tumbaku   nyingine  ambazo  zilikuwa bado zipo  kwenye  mianzi ya kukaushia tumbaku na kuzichoma.

Kati ya  bani zake  alizokuwa  nazo za kukaushia tumbaku waliweza kumchomea  bani tatu  zenye tumbaku na  bani mbili waliziacha kwa kuwa hazikuwa na tumbaku  na walipokuwa wanawachomea walikuwa wakiwatolea  maneno ya kuwatisha na kuwaambia pia  ngoja wapate  hasara .

Amesema kila alipokuwa akijaribu kuwasihi  waache kuchoma   tumbaku hiyo walikuwa wakimuongezea kichapo kwa kupigwa fimbo kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake licha ya kuchomewa tumbaku yake waliweza pia kumchome sola yake ya umeme wa jua na waliweza chukua kiasi cha tshs 58,5000  ambazo zilikuwa kwenye nguo.

Amemwomba   Rais  Dkt  Samia  Suluhu  Hassan na  Waziri  waweze kusaidia  kufatilia tukio hili  kwani walioathirika na tukio hilo ni wengi wapo watoto wanao soma,kuna  kodi ya Serikali ambayo ingelipwa  ushuru .

Nae Silivanus Kaponela mkulima  mwingine aliyachomewa tumbaku yake siku hiyo amesema yeye alikuwa yupo shambani kwake na mkewe wanavuna tumbaku na  ghafla  aliona askari  wanashuka kwenye pikipiki zao  na  ndipo waliposhuka na kuanza kuchoma tumbaku zao

Mwenyekiti wa   bodi  ya  Ivungwe Amcos Nikilias Nicolaus almeeleza  kuwa  yeye  tukio  la kuchomewa  wakulima wake alilipata  siki  hiyo  hiyo ya tukio  na alijulishwa   kuwa  kati  ya   zaidi  ya  ekari  15 zilizochomwa    ekari zaidi ya 11 zilikuwa za wakulima wa Amcos yake na ekari  nne zilikuwa za wakulima wa  Katumba Amcos .

Amesema  imekuwa ni ajabu kuona tumbaku inaadhibiwa wakati wenye mashamba hayo wapo  na  wamekuwa wakilima  hapo kwa muda  mrefu  na  athari ilitotokea ni kubwa kwa wakulima wake ambao kwa kiasi  cha wakulima wa Amcos ya Ivungwe wamepoteza zaidi ya dolla 20,000 na pia  Amcos  nayo imekosa  mapato   ya  Serikali kwa kuchomwa tumbaku hiyo .

Hamadi Juma mmoja ya Mkulima aliechomewa Tumbaku yake kwenye Shambani kwake
Mwenyekiti wa  Kijiji cha  Ivungwe Kabula laibiruki ameeleza  kuwa sehemu ambayo wakulima wamechomewa tumbaku hiyo ni  eneo la  makazi na walipewa wakulima kwa masharti  ya  kufanya shughuli za kilimo   na sio kwa ajiri ya kujenga  majengo ya kudumu .

Amebainisha kuwa     toka  amekuwa  mwenyekiti   hawajawahi kuambiwa  eneo  hilo kuwa ni  eneo la hifadhi isipokuwa  imekuwa tuu ikitokea matukio ya kupigwa kwa wananchi   na askari wa  Maliasili .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages