MKOA WA KATAVI WANUFAIKA NA SERIKALI YA RAIS SAMIA

Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akielezea Mafanikio ya Miaka 3 kwa Mkoa wa Katavi Chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan

Na Walter Mguluchuma-Katavi

Mkoa wa Katavi umenufaika  na  Serikali ya awamu ya  Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia  Suluhu  Hassan  kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake  kwa kupokea  zaidi ya shilingi Tilioni  1.2  kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi mbambali ya maendeleo na kutatua changamoto  kwa wananchi .

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akiwa katika kongamano hilo la kuelezea Mafanikio ya serikali ya Awamu ya Sita kwa Mkoa wa Katavi.

Mkoa wa Katavi umenufaika  na  Serikali ya awamu ya  Sita inayoongozwa na   Rais Dkt Samia  Suluhu  Hassan  kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake  kwa kupokea  zaidi ya shilingi Tilioni  1.2  kwa ajiri ya utekelezaji wa miradi mbambali ya maendeleo na kutatua changamoto  kwa wananchi .

Hayo yamesemwa  na  Mkuu wa Mkoa wa Katavi   Mwanavua  Mrindoko  katika  Kongamano  kuhusu  mafanikio  ya Mkoa wa Katavi   kwa miaka   mitatu  ya Serikali ya awamu ya sita  chini ya uongozi  wa  Dkt  Samia  Suluhu Hassan 

Amebainisha kuwa Mkoa wa Katavi  ulipoanzishwa  mwaka 2012 haijawahi kupatapa fedha nyingi ambazo zimetekeleza zimesaidia  kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile Barabara ,Maji  Afya  Elimu na ujenzi wa  Bandari .

Amesema Mkoa wa Katavi huwezi kulinganisha na ile ya miaka ya nyuma ni sawa na kulinganisha usingizi na kifo  kwani kwenye kifo hakuna kuamka   kwani  Mkoa huu kwa  sasa umeamka  unasonga mbele kwa maendeleo  makubwa kwasababu  ya Serikali  inayoongozwa na Dkt  Samia  Suluhu  Hassan .

Mrindoko  amesema  Rais  ameweza kuwaletea fedha nyingi  zaidi ya Tilioni  1.246 kwa ajiri ya kutatua kero mbalimbali  kwa ajiri ya kuongeza upatikanaji wa  huduma za jamii  na kuongeza miundo mbinu mbalimbali  katika kuhakikisha uchumi wa Mkoa wa Katavi  na Taifa unaendelea kukua .

Kiasi hicho  cha  fedha zilizoletwa  zimeenda  kwenye  sekta  mbambali   kama Ofisi ya  utawala ya Mkoa , Halmashauri zote  tano za Mkoa huu , Mawasiliano  Tanesco , Tanroads , Ruwasa ,Muwasa   Tarura , ujenzi wa  Bandari ya Karema , Miradi ya  umwagiliaji,  Misitu , Tasaf  fedha zilizopelekwa  kwenye miradi  hiyo  ziweeza kufikia kiasi cha tshs  Tilioni  1.246.

Amesema  wameweza kujenga  shule  mpya 28  ambazo hazikuwepo  tangu  Mkoa ulipoanza ambazo zimejengwa katika kipindi  hiki cha miaka mitatu ambazo hazikuwepo   kati ya shule hizo za Sekondari ni  12 na  shule za Msingi  ni 16  ambazo hazikuwepo kabisa  kati ya shule hizo moja ni shule maalumu ya wasichana iliyogharimu  kiasi cha zaidi  ya shilingi Bilioni  3 ambapo shule zote hizo zimeisha anza kutoa huduma .

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu akielezea mafanikio yaliyopatikana katika Wilaya ya Tanganyika chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan 

Kwa upande wa  madarasa Mrindoko amesema wameweza kujenga  madarasa  773 na  madawati   zaidi ya 24,000 yametengenezwa  na maboma 313 kwa maana hiyo miundombinu hiyo iliyopatikana umbali wa kutoka  nyumbani kwenda shuleni umepungua  sana kwa wanafunzi  na hiyo ni mafanikio  yakuweza  kupunguza utoro na mimba  za   utotoni  na imeweza kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari .

Kuhusu  Afya  amesema   umbali kwa kwenda  kupata huduma  za afya kwa wanachi umepungua sana  na  gharama za kwenda kutafuta   matibabu kwenye Hospitali za Rufaa  umepungua  baada ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kuanza kutowa  huduma.
Mrindoko  amesema kwa sasa wananchi wa Mkoa huu wanapata  huduma za kibingwa hapa hapa  kwenye  Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa  kwa maana hiyo Rais  Dkt Samia  amewahakikisia wananchi  uwepo wa afya bora  kwa kupata tiba kamili  za kibingwa hapa hapa .

Amefafanua kuwa kuna  zaidi ya vituo 20 vya afya  zimejengwa   katika kipindi hiki na zahanati 36  hivyo  hivyo yapo  magari kumi na sita ya kubeba wagonjwa  na kama kunakuwepo    na changamoto yoyote ya  mgonjwa  magari hayo yamekuwa yakiwafikisha kwenye  maeneo husika na kuweza kuokoa uhao wa watu .


Kuhusu  upatikanaji wa  maji  vijijini  kwa sasa  upatikanaji wa  maji kwenye  Mkoa huu ni asilimia 73.7 hali  ambayo  imesaidia  kupunguza  tatizo kabisa la ugonjwa wa milipuko  kama vile kipindupindu   hasa katika Wilaya ya Tanganyika  ambako mara nyingi kulikuwa kunatokea mlipuko wa ugonjwa huo na  upatikanaji wa  maji mjini ni asilimia 60.

Ameeleza kuwa  kwa mara ya kwanza Mkoa huu  unatarajia  kuanza kutumia umeme wa  gridi    ya Taifa kuanzia  mwishoni mwa mwezi june mwaka huu   ambapo kwa sasa wanatumia umeme wa jenereta  hali  ambayo  ilikuwa  ikiathiri shughuli nyingi za kiuchumi .

Meya  Mstaafu wa Manispaa ya  Mpanda  ambae  ni  Diwani wa  Kata ya Majengo Willy  Mbogo  amesema kuwa    zamani  swala la  mtoto  kufaulu  shule ya Msingi na kwenda Sekondari lilkuwa ni  jambo geni  kutokana na uchache wa shule za sekondari .

Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga akieleza mafanikio yaliyopatikana kwenye Wilaya hiyo katika kipindi cha Miaka 3 ya Rais Samia Suluhu Hassan

Amesema ilikuwa  mtoto akifaulu  wazazi wanamfanyia  mpaka sherehe  lakini siku hizo jambo la wanafunzi kufaulu  limekuwa ni la kawaida kutokana na kuongezeka kwa shule za sekondari kuwa  nyingi .

Godfrey  Sadala   mkazi wa Manispaa ya  Mpanda amesema  kuwa  hali ya miundombinu ya barabara kwa pindi hiki cha miaka mitatu imeboreshwa sana kwani barabara za  kutoka  na kuingia  zinapitika kwa muda wote na  sasa  hivi    wananchi wanasafiri na kufika  Dares salaam kwa siku  hiyo hiyo tofauti na hapo nyuma walikuwa wanatumia siku tatu .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages