Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Mpanda ambapo amli imetolewa kwa Mwili wa Marehemu kufukuliwa na kuzikwa upya |
Na Walter Mguluchuma-Mpanda
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imeamuru mwili wa Marehemu aliyefakamika kwa majina ya Juma Andrea Bukuku uliokuwa umezikwa katika Makuburi ya Kashaulili Manispaa ya Mpanda ufukuliwe na kuzikwa upya baada ya mke wa marehemu kufungua kesi akidai marehemu mume wake alizikwa kwa imani ya Dini ya Kikiristu badala ya dini ya Kiisilamu.
Mke wa Marehemu aliyefungua Shauri hilo akiwa anatoka Mahakamani baada ya hukumu hiyo kutolewa mahakamani hapo |
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imeamuru mwili wa Marehemu aliyefakamika kwa majina ya Juma Andrea Bukuku uliokuwa umezikwa katika Makuburi ya Kashaulili Manispaa ya Mpanda ufukuliwe na kuzikwa upya baada ya mke wa marehemu kufungua kesi akidai marehemu mume wake alizikwa kwa imani ya Dini ya Kikiristu badala ya dini ya Kiisilamu.
Hukumu hiyo iliiyovuta hisia za
watu wengi wa Mji wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi imetolewa na Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mh
Gospher Luoga baada ya Mahakama kuridhika
na ushaidi uliotolewa Mahakamani hapo na
upande wa mdai na upande wa mdaiwa
Katika kesi hiyo mdai aitwaye
Rehema Saidi ambae ni mke wa
marehemu alikuwa akitetewa na Wakili Hamad
Arfi na mdaiwa ambae ni baba wa marehemu
anaitwa Andrea Bukuku alikuwa akitetewa
Mahakamani hapo na Wakili Patrick Mwakyusa
Kesi hiyo ilifunguliwa
mahakamani hapo kwa mujibu wa kifungu cha sheria
Namba 95 sura ya 33 ya mwaka 2019 na kifungu namba 9 ya
Sheria ya uchunguzi wa maiti ambapo
Reremu alifungua kesi ya kudai mwili wa marehemu
mume wake Juma Andrea Bukuku ulizikwa
kaburini ufukuliwe na uzikwe upya baaada ya
kuzikwa kwa imani ya diniya kikiristo badala ya dini ya
kisramu
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakitoka nje ya Mahakama baada ya uamuzi huo kutolewa |
Wakili wa mdai Hamad Arfi
alidai mahakamani hapo kuwa mwili wa marehemu huyo
unapaswa ufukuliwe na kuzikwa kwa upya kwa kuwa marehemu
alizikwa nje ya imani yake ya dini kwani
kabla ya kifo chake kilichotokana na kugongwa na
gari marehemu alifunga ndoa mwaka 2018 na mkewe
Rehema ya kisiramu huko huko Kigoma
Alidai kuwa Rehewa na mumewe
waliendelea kukaa pampja na marehemu huyo hadi
mwaka 2022 ndipo walipotengana na licha ya kutengana waliendelea kuwa na mahusiano nae ya karibu kwa kuwa alikuwa amezaa nae
mtoto na pia alikuwa haja mpa talala.
Hivyo alidai kuwa marehemu alifariki
Aprili 15 mwaka huu na kuzikwa Aprili 17 kinyume na mafunzo ya Dini ya kisiislamu yanavyoelekeza kwa hiyo waliomba Mahakama kutoa kibali cha mwili wa marehemu huyo ufukuliwe na
kuzikwa upya kwa imani ya dini yake .
Madai hayo yalipingwa na Wakili
wa Baba wa Marehemu Wakili Patrick Mwakyusa
alidai kuwa wao wanao wanafahamu
Jina la Marehemu ni Lwitiko Andrea Bukuku
na sio Juma Bukuku ni mkiristu
na alibatizwa katika Kanisa la Moroviani .
Wakili Mwakyusa ameimbia Mahakama kuwa kwa maana hiyo Juma Bukuku na Lwitiko Bukuku ni watu wawili tofauti kwani marehemu
wao ka mujibu wa nyaraka walizo nazo zinaonyesha kuwa ni
mkiristo .
Hakimu Mkazi Mfawidhi
wa Mahaka ya Wilaya Mpanda Mh Gospher
Luoaga wakati akisoma hukumu hiyo aliiambia Mahakama kuwa
marehemu baada ya kuwa mtu mzima alifunga
ndoa ya kiisilamu.
Kwa hali hiyo mahakama
imejiridhisha kuwa wakati wa marehemu anafunga ndoa huko
Kigoma ndipo alipobadilisha jina na kuitwa Juma
Andrea Bukuku na kuhamia kwenye dini nyingine ya
kisramu
Kutokana na umri ambao tayari
alikuwa amefikia ilikuwa sio lazima kwenye
maamuzi yake ya kubadili dini amshililishe mtu mwingine
kwenye maamuzi yake yalikuwa ni yake mwenyewe kwa kuwa
alikuwa amekuwa mtu mzima .
Hivyo alisema kutokana na
ushahidi wa pande hizo mbili mahakamu inatowa hukumu ya mwili wa
marehemu kufukuliwa na kuzikwa upya wa imani ya dini ya kisramu na
kwenye ufukuaji huo wa mwili wa marehemu kuwepo na usimamizi wa karibu wa
jeshi la polisi na maafisa wa afya
Mara baada ya hukumu hiyo Wakili
Mwakyusa alisema atakata rufaa ya kuomba mwili huo wa
marehemu kufukuliwa na kuzikwa upya .
Wakili Hamadi Arfi alisema
ameridhishwa na hukumu iliyotolewa kwani imezingatia sheria kwa kutambua marehemu alikuwa amezikwa kwa imani ya
dini nyingine.