Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari kwenye ofisi za Takukuru |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imefatilia utekelezaji wa miradi mitano inayotekelezwa katika Mkoa wa Katavi yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5.82.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa TAKUKURU
Mkoa wa Katavi Faustine Maijo wakati alipokuwa akitowa
taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo mbele ya vyombo vya
habari .
Amesema kwa kuzingatia miradi
ya maendeleo ni mali ya wananchi ambako Serikali imepeleka fedha katika eneo hilo ndio
maana Takukuru wanafatilia kwa karibu utekeleza wa
miradi yote inayotekelezwa kwenye Mkoa wa Katavi
.
Hivyo kwa kipindi cha cha miezi
mitatu ya kuanzia januari 2024 hadi machi
wameweza kufatilia miradi mitano kwa ukaribu
yenye thamani ya shilingi Bilioni 5.82 katika sekta za miundombinu na elimu
Kuhusu malalamiko ya Rushwa amesema
Takukuru katika kipindi hicho cha miezi mitatu wamepokea
malalamiko 41 yanayohusiana na vitendo vya rushwa
katika ya malalamiko hayo 38 yalikuwa ni ya rushwa na matatu
hatakuwa ya rushwa .
Maijo amefafanua kuwa kutokana na taarifa
hizo za malalamiko ya rushwa wameweza kufungua majalada 38
yalitokana na taarifa hizo ambapo uchunguzi wa majalada
matatu umekamilika na katika kipindi hicho cha miezi
mitatu mashauri manne yamefunguliwa mahakamani
na kufanya kesi nane zinazoendelea mahakamani .
Katika hatua nyingine Mkuu wa
Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo amewaonya watu
ambao wamekuwa wakiwatapeli watu kwa kujifanya wao ni maafisa wa Takukuru
waache mara moja kufanya hivyo .