Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Katavi Shabili Dallah akizungumnza katika kikoa hicho |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Chemba ya wafanya
biashara Mkoa wa Katavi (TCCIA)wamelalamikia baadhi
ya wakulima wa Mkoa huu kuuziwa mbolea ambayo mifuko yake ya
kuhifadhia mbolea hiyo imeandikwa Ruzuku wakati wakulima hao wanauziwa mbolea
hiyo kwa bei ya juu ambayo sio ya bei ya Ruzuku .
Chemba ya wafanya biashara Mkoa wa Katavi (TCCIA)wamelalamikia baadhi ya wakulima wa Mkoa huu kuuziwa mbolea ambayo mifuko yake ya kuhifadhia mbolea hiyo imeandikwa Ruzuku wakati wakulima hao wanauziwa mbolea hiyo kwa bei ya juu ambayo sio ya bei ya Ruzuku .
Malalamiko hayo yametolewa na Mwenyekiti
wa Chemba ya biashara , viwanda na Kilimo
Tanzania Mkoa wa Katav (TCCIA)i Shabili Hassanal
Dallah mbele ya Rais wa TCCAIA
Tanzania wakati wa kikao na wafanya biashara
wa Mkoa huu kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya
Mpanda .
Amebainisha kuwa kumekuwepo na
changamoto mbalimbali za wakulima katika Mkoa wa
Katavi moja ya changamoto hizo ni mbolea ya
ruzuku iliyoletwa katika mkoa huu zilikuwa ni za
ruzuku ambazo bado bei ilikuwa ni ile ile ya juu.
Amesema wakulima wameshindwa kuelewa kwa
kuuziwa mbolea ambayo kwenye mfuko imeandikwa ni ya
ruzuku rakini wameweza kuuziwa mfuko mmoja
kwa gharama ya tshs 150,000 hivyo wameshindwa kufahamu ni
kwanini mbolea iandikwe kwenye mfuko kuwa ni ya ruzuku halafu
wameuziwa kwa bei hiyo .
Amedai kuwa hata baadhi ya mbolea
iliyoingia kwenye Mkoa huu haikuwa na ubora hali
ambayo imesababisha baadhi ya wakulima kuweza kupata hasara
kutokana na borea hiyo kutokuwa na ubora unaositahili
Rais wa TCCIA Tanzania Vicent
Minja amesema changamoto hiyo ya mbolea
ya ruzuku kuuzwa kwa bei ya juu na mbolea nyingine
kutokuwa na ubora amesema kuwa ni kweli kumekuwepo na
malalamiko ya wakulima kutumia mbolea na kupata
kitu ambacho wakutegemea kukipata .
Ametowa mfano kwenye mbegu za
alizeti huko Singida wenye viwanda mwaka
jana wameshindwa kuzalisha mafuta ya alizeti kwasababu
mwaka jana wakulima walipelekewa mbegu ambazo azikuwa sahihi
wakulima walilima na kupanda lakini haikuota na hata
kwa wale iliota haikuweza kuzaa sawa sawa.
Minja amefafanua kuwa kwa hali hiyo ya
mbolea ni changamoto ambayo ipo Kitaifa na wao TCCIA
wanalijua na wamepanga kulikisha kwenye Wizara ya
kilimo kwa ajiri ya hatua zaidi .
Kuhusu masoko ya mazao hasa
mahindi na mpunga amesema Waziri wa Kilimo Hussen Bashe alipoteuliwa kuongoza wizara ya kilimo
alisema mkulima amelima mwenyewe mazao
yake wanaruhusiwa kuuza sehemu yoyote wanako taka kuuza
lakini baada ya muda mfupi alisimamisha tena mahindi kuuzwa
nje .
Hali hiyo ya kuzuia mahindi yasitoke nje
imesababisha gunia moja la mahindi lililokuwa likiuzwa
kwa bei ya tshs 110,000 sasa hivi linauzwa kwa bei ya tshs 30,000
wamepigiwa simu na wakulima wengi sana wanamagunia wengine kwenye maghala
yao mpaka elfu kumi na sasa hivi msimu wa mavuno
umeingia huku maghala yakiwa yamejaa mahindi
Amesema hali hiyo inaweza kufanya wafanya
biashara na wakulima waweze kufilisika kwa hali hiyo TCCIA ngazi ya
Taifa wanalifanyia kazi kwa kuwa jambo hilo wanalifahamu na halipo
katika Mkoa wa Katavi tuu.
Nae mkulima Doto Sivester amesema yeye ni mkulima wa zao la tumbaku ambapo mbolea mfuko mmoja wameuziwa msimu huu kwa dola 63 na wameambiwa ni ya ruzuku sasa wanashindwa kuelewa bei hiyo kama na ruzuku ipo kwa mkulima kutokana na bei hiyo