Mgojwa akiwa akisafirishwa katika gari la wazi kutoka Kata ya Karema hadi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi kwa kutumia Gari la Kanisa Katoriki. |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Katika hali isiyo ya kawaida gari aina ya Pikapu likiwa wazi la Parokia ya Karema limetumiwa kumsafirisha mgonjwa aitwaye Peter Lungu umbali wa kilometa 112 kutoka kituo cha Afya cha Karema alikokua amelazwa hadi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi baada ya kituo hicho kukuwepo kwa gari la kubebea wagonjwa .
Mgojwa huyo akiwa amefikishwa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Katavi baada ya Safari ya muda kutoka Karema |
Katika hali isiyo ya kawaida gari aina ya Pikapu likiwa wazi la Parokia ya Karema limetumiwa kumsafirisha mgonjwa aitwaye Peter Lungu umbali wa kilometa 112 kutoka kituo cha Afya cha Karema alikokua amelazwa hadi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi baada ya kituo hicho kukuwepo kwa gari la kubebea wagonjwa
Gari hilo la pikapu lililombeba mgonjwa huyo
ilikuwa na namba za usajiri T 176 BGU mali
ya Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda lillilokuwa
likiendeshwa na Padri Emili Sibomana paroko msaidizi wa
parokia ya Karema
.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa mke wa mgonjwa huyo
Eliza Apolonali ambae alikuwa amemsindikia
mume wake hadi kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wakiwa
wanatokea kwenye kituo cha afya Karema walikokuwa wakipatiwa
matibabu .
Amesema mume wake alikuwa amelazwa kwenye kituo cha
Afya cha Karema kwa muda wa siku mbili kwa tatizo la
ugonjwa wa shikizo la damu (BP)kutokana na hali yake kuendelea
kutokuwa nzuri siku ya jumanne tarehe 10
makaktari wa kituo cha afya Karema walitowa rufaa ya
mgonjwa huyo kwenda kutibiwa katika hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Katavi .
Amebainisha kuwa baada ya kuwa wamepewa rufaa hiyo waliendelea
kusubiria kupatiwa gari la kubeba wagonjwa ambalo halikuwepo kituoni hapo
pasipokuwa na mafaniko yoyote yale licha ya mgonjwa wao
hali yake kuendelea kuwa kuwa mbaya
Kutokana hali ya mgonjwa kuendelea kutokuwa nzuri siku
iliyofuata walipata wazo la kwenda kwenye Parokia ya
Kanisa Katoliki ya Karema kwenda kuomba msaadawa
usafiri ili waweze kuokoa uhai wa ndugu yao.
Eiza ameeleza kuwa baada ya kufika parokiani Karema
walimkuta Paroko msaidi Padri Emili
Sibomana paroko wa parokia wa parokia hiyo Padri
Nicodemo Kiyumana alikuwa yupo safari hata hivyo
paroko msaidizi alikubali kuwapatia msaada wa gari la Kanisa
hilo aina ya pikapu la azi
Nae Padri Sibomana amesema ndugu wa mgonjwa huyo
walifika parokiani kwake majira ya saa tano asubuhi
na baada ya kusikiliza shida waliokuwa nayo ya usafiri alilazimika kutowa gari Kanisa aina ya pikapu
licha ya kuwa gari hilo sio maalumu la kubebea mgonjwa lakini
alilazika kutowa msaada huo .
Ameeleza ilipofika saa tano na nusu aliweza kufika
kwenye kituo hicho cha afya Karema na waliweza
kumpakia mgonjwa huyo na kulaza kwenye bodi ya
gari ambalo aliweka godoro na kisha walianza
safari ya kumsafirisha mgonjwa kumpeleka katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huku wakiwa wameambatana na dakitari mmoja wa
kituo hicho
.Kutokana na kipindi hiki cha masika kuwa na mvua huku
gari hiyo ikiwa ipo wazi aliona safari hiyo kuwa
ilikuwa ni ngumu sana hali ambayo ilkuwa ikimlazimu
alipokuwa njiani akikutata wingu la mvua kusimamisha gari
alikuwa akiendesha na kuanza kusali kumwomba Mungu awasaidie
ili mvua isimnyeshee ili aweze kumfikisha
salama hospitalini mgonjwa huyo
Padri Sibomana amesema kutokana hali hiyo
safari ya kumfikisha mgonjwa ilichukua muda mrefu
waliweza kutumia zaidi ya saa sita hadi
kufika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa waliweza
kufika majira ya saa kumi na moja na nusu jioni
Nao baadhi ya watumishi wa kituo hicho waliongea na Jamhuri
kwa nyakati tofauti kutotaka kutajwa kwa majina yao wamesema
kituo hicho cha Afya Karema kinahudumia wagonjwa
wanaokuwa wamepewa rufaa kutoka kwenye Zahanati sita
zilizopo kwenye Tarafa hiyo ilipo mwambao mwa
ziwa Tanganyika inayopakana na Nchi ya DRC.
Wamebainisha kuwa kituo hicho kimekuwa na changamoto kubwa ya
kutokuwapo kituo hapo na gari la kubebea wagonjwa licha ya Serikali
kutowa gari kwa ajiri ya kubebea wagonjwa gari la kituo
hicho limekuwa halikai kwenye kituo cha Afya na badala
yake linakaa Majalila yalipo makao makuu ya Wilaya
umbali wa zaidi ya kilometa 130.
Wamesema kutokana na gari la kituo hicho kuwa mbali na
kituo mgonjwa anapokuwa amepewa rufaa
huwa wanalazimika kutuma taarifa yalipo
makao makuu Halmashauri yao kwa ajiri ya kumchukua
mgonjwa alipewa rufaa .
Wamebainisha hata hivyo mara nyingi gari limekuwa halifiki
kituoni hapo kwa wakati unaweza ukaomba gari leo saa
nane mchana gari linafika kesho yake saa mbili
au saa tatu asubuhi matokeo yake ya kuchelewa kuwasafirisha
wagonjwa kumekuwa kukisababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza uhai
wakiwa njiani na wengine kufikishwa hospitalini wakiwa wamechoka .
Wamedai kuwa kumekuwapo na tabia ya kutoa kipaumbele zaidi
cha kuwasafirisha wajawazito pindi wanapokuwa wameomba
usafiri wa gari la wagonjwa kuliko wagonjwa wengine kwani
kunawakati wamekuwa wakiambiwa gari la wagonjwa halina mafuta .
wamesema watu wamekuwa wakipata changamoto ya kuwasafirisha kwa
boda boda wagonjwa kutoka kwenye zahanati kuwapeleka kwenye
kituo cha afya Karema kutokana na gari la kituo hicho cha
Afya kutuwepo
Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Wilaya ya
Tanganyika Moshi Kakoso amekiri kuwepo kwa changamoto
ya gari la kubebea wagonjwa kwenye kituo hicho cha afya kilichoko mwambao
mwa Ziwa Tanganyika
Amesema kuwa Halmashauri ya Tanganyika inavituo vya Afya vitatu ambapo magari ya kubebea wagonjwa yapo mawili tuu hivyo kulingana na jografia ya Wilaya hiyo ndio maana magari yanalazimika kukaa kwenye Makao makuu ya Wilaya yaliko katika Mji wa Majalila