Waziri wa Ujenzi Innocent Bashugwa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi anaejenga Barabara ya Kibaoni Sitalike Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi |
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa
amemwangiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Tanzania
kutoipatia mkataba wowote wa kutengeneza Barabara mpya hapa
nchini kampuni ya kichina ya CHINA RAILWAYS SEVENTH GROUP
COMPANY LIMITED [CRPSG] mpaka hapo kampuni hiyo itakapo kuwa imekamilisha
miradi iliyonayo kwa sasa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amemwangiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Tanzania kutoipatia mkataba wowote wa kutengeneza Barabara mpya hapa nchini kampuni ya kichina ya CHINA RAILWAYS SEVENTH GROUP COMPANY LIMITED [CRPSG] mpaka hapo kampuni hiyo itakapo kuwa imekamilisha miradi iliyonayo kwa sasa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga akimwelezea Waziri wa Ujenzi Innocent Bashugwa umuhimu wa Barabara ya hiyo kwenyw Wilaya ya Mlele |
Kufuatia hali hiyo Waziri Bashugwa amemwagiza Mtendaji Mkuu
wa Tanroads Tanzania kutoipatia kazi kampuni hiyo mpaka itakapokuwa
imekamilisha miradi yake ambayo imepewa na Serikali kwenye maeneo
mengine hapa nchini.
Ameeleza kuwa mpaka sasa kuna miradi mitano wanayoitekeleza hapa mchini huku wakitekeleza miradi hiyo kwa kusuasua.
Aidha Bashungwa amepata mashaka kwa kuwepo na mitambo mingi ikiwepo magari yanayotumiwa na mkandarasi huyo kuwa ni mabovu hivyo amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya ujenzi kupeleka timu ya wataalamu kwenye mradi huo kuikagua ili kuweza kufahamu mangapi yanafanya kazi pamoja na kuchukua hatua kimkataba kwa mwandisi mshauri .
Amebainisha kuwa Serikali imeendelea kuboresha miundo mbinu ya Barabara katika Mkoa wa Katavi inayounganisha Mkoa huu na mikoa mingine kama vile barabara ya lami Mpanda Vikonge kwenda Kigoma km 37 inafanya kazi Vikonge Luhafe km 25 ujenzi wake upo asilimia 57.4.
Amezitaja Barabara nyingine kuwa ni Luhafe Mishamo pamoja na barabara inayoelekea Bandari ya Karema kuanzia Kagwira yenye urefu wa kilimota zaidi ya 112 mkandarasi wake ameisha patikana na Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kumkabidhi Barabara mkandarasi iliaweze kuanza kazi .
Diwani wa Kata ya Kibaoni Victor Kabanga akimuomba waziri wa Ujenzi Innocent Bashugwa jitihada zifanyike kukamilisha Barabara hiyo kwa wakati. |
Kaimu Mtendaji Mkuu waTanroads Mhandisi Doroth Mtenga amesema kuwa ujenzi wa Barabara hiyo ya kutoka Kibaoni kuelekea sitalike unagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 88.725 kutoka mfuko mkuu wa Serikali kwa asilimia 100 .
Mhandisi Mtenga amefafanua kuwa mradi huo kuwa nyuma ni pamoja utekelezaji wake kuwa tofauti ukilinganisha na mpango kazi wake na kuchelewa kuleta wataalamu wake kwenye mradi kama ilivyotakiwa kimkataba .
Awali Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alimweleza Waziri Bashungwa kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo inatakiwa kukamilika June 2025.