Rais wa Chemba ya Biashara,Viwanda na Kilimo Tanzania [TCCIA] Vicent Minja akizungumnza na wafanyabiashara wa Mkoa wa Katavi. |
Wafanya Biashara Mkoa wa Katavi wameshauriwa kujiunga na TCCIA ili waweze kuwa na nguvu ya pamoja ya kuweza kuungana na nguvu ya pamoja katika kujadili changamoto zao kwenye Biashara na kuziwasilisha sehemu husika ili ziweze kufanyiwa kazi .
Rais wa TCCIA Taifa akiwa akiendesha kikao cha Wafanyabiashara mkoa wa Katavi akiwa na viongozi wa TCCIA Mkoa wa Katavi na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Wafanya Biashara Mkoa wa Katavi wameshauriwa kujiunga na TCCIA ili waweze kuwa na nguvu ya pamoja ya kuweza kuungana na nguvu ya pamoja katika kujadili changamoto zao kwenye Biashara na kuziwasilisha sehemu husika ili ziweze kufanyiwa kazi .
Wito huu umetolewa na Rais wa Chemba ya Bishara ,Viwnda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Vicent Minja wakati wa kikao chake na Wafanyabiashara mbalimbali wa Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda kwenye ziara ya siku mbili Mkoani hapa .
Amesema wafanya biashara wa Mkoa wa Katavi hawezi kufanikiwa kwenye kutatua changamoto zao kama hawatakuwa wameungana na kujiunga na TCCIA kwakuwa chombo hicho ndicho chenye mamlaka ya kusikiliza kero zao na kuzipeleka katika ngazi za juu za zenye mamlaka.
Baadhi ya Wafanya biashara walio hudhuria kikao hicho wakimsikiliza Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara,Kiwanda na Kilimo Tanzania Vicent Minja. |
Amebainisha kuwa Chemba hiyo imeshuka katika ngazi ya Wilaya na Mkoa ili wafanya biashara waungane na kujadili changamoto zao na kuzipeleka Serikalini ili ziweze kufanyiwa kazi .
Minja amesema wafanyabiashara hao watafanikiwa katika kutatua changamoto zao kwa kuungana kupitia Mwavuli wa [TCCIA] hivyo nilazima kuhakikisha wanatumia umoja huo ili kufanikisha Malengo yao ya Kibiashara.
Amewasisitiza waweze kutumia Chemba ya wafanya biashara ya Katavi kwakuwa serikali hutatua changamoto za wanananchi kwa kuangalia idadi ya wahusika katika jamii husika
Amesema changamoto kubwa ambayo ameiona Katavi watu hawatumii vizuri ofisi ya Chemba ya Mkoa wa Katavi kwani mjasiliamali yoyote anaweza kuwa mwanachama wa Chemba hata kama ni wakulima wenye kikundi kitendo cha watu kutojiunga ndicho kinachowafanya washindwe kusikilizwa changamoto zao .
Ameeleza kutokuwa na elimu sahihi ya kodi kuna waumiza sana wafanya biashara na hilo amekuwa akilizungumza yeye kwenye mikoa yote anayopita na kuwashauri chemba za mikoa kuweka wahasibu ambao watakuwa sehemu ya kuwasaidia wafanyabiashara kuhusu Kodi.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Katavi Shabili Hassanal Dhalla alisema kumekuwa na changamoto ya wafanya biashara wa Mkoa huu kutoana umuhimu wa kujiunga na chemba ya wafanya biashara ila wanapokuwa wamepatwa na changamoto ndipo wanapoona umuhimu.
Amemwomba Rais wa TCCIA kutowa nafasi ya utendeleo kwa wafanya biashara wa Mkoa wa Katavi pindi inapokuwa imetokea nafasi ya kwenda nje ya nchi kwa ajiri ya mafunzo wawe wanamchukua hata mmoja wa kutoka katika Mkoa huu.Ameoimba Serikali kufungua mikapa ya kwenda kuuza mazao ya wakulima hasa kwenye nchi za Uganda Kenya na Kongo ambako Mahindi na mpunga walikuwa wakiiuza huko kwani kwa sasa mazao hayo hayana soko huu na yamejaa kwenye maghara ya wafanya biashara .
Mhasibu wa TCCIA Mkoa wa Katavi Kelvin Mbogo amesema wanaanzisha dawati maalumu la Kodi kwa wafanyabiashara kwa lengo la kuwaelimisha maswala mbalimbali yanahusu kodi kutokananan na baadhi yao kutokuwa na elimu sahihi ya Kodi.
Judithi Baraga Mzabuni wa chakula katika Mkoa huu amesema wao wamewekwa kwenye VAT wakati manunuzi yao karibu asilimia 90 hayakatwi lisiti za mashine ya EFD matokeo yake wamekuwa wakilipa VAT asilia 18 kwa hela nyingine za mfukoni mwao .
Ameeleza Changamoto ya kutolipwa kwa wazabuni madeni yao kwenye Halmashauri pindi anapokuwa amehamishwa Wakukurugenzi kwenye Halmashauri na kuja kwa wakurugenzi wapya imekuwa ni sababu ya wazabuni kutolipwa Fedha zao kwa wakati .