Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akitoa maelezo ya Miradi mbalimbali ya Barabara iliyo chini ya Wizara ya Ujenzi |
Na Walter Mguluchuma-Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua
Mrindoko amemlalamikia Mkandarasi anaejenga barabara ya Kibaoni sitalike kwa
kujenga mradi huo kwa mwendo wa kinyonga hali ambayo inawasabishia usumbufu
wananchi wanaotumia barabara hiyo katika shuguli za kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amemlalamikia Mkandarasi anaejenga barabara ya Kibaoni sitalike kwa kujenga mradi huo kwa mwendo wa kinyonga hali ambayo inawasabishia usumbufu wananchi wanaotumia barabara hiyo katika shuguli za kiuchumi.Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko[Kulia] akitoa taarifa ya miradi ya Barabara inayojengwa katika mkoa wa Katavi mbele ya Waziri wa Ujenzi Innocent Bashugwa[Kushoto]
Malalamiko hayo ameyatoa mbele ya
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashugwa alipofika mkoa wa Katavi katika zaiara ya
siku moja ya kujionea kazi zinazotekelezwa zilizo chini ya wizara yake.
Mrindoko amebainisha kuwa
Mkandarasi anaejenga Barabara hiyo ya Kibaoni Sitalike yenye Urefu wa Kilomita
50 umekuwa unaenda kwa kusuasusua na kumuomba Waziri kuona namna ili kasi
iongezeke na wanananchi wanufaike na mradi huo.
‘’Tunatatizo katika mradi wa
Kibaoni sitalike mradi huu hauendi katika kasi iliyokusudiwa na kweli kama mkoa
na wananchi wake hatuliziki kabisa na mwenendo wa mradi ule’’-Mwanamvua
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashugwa akielezea namna Wizara yake inavyotekeleza ujenzi wa Miradi ya Barabara katika mkoa wa Katavi
Amesema kuwa mradi huo unakipindi
cha miaka Miwili sasa lakini bado haujakamilika ukiwa umefikia Asilimia 14.8 hali
ambayo kwa nanma moja au nyingine inachelewesha maendeleo ya wananchi wa mkoa
wa Katavi kupitia shughuli za kiuchumi kwenye barabara hiyo.
‘’Barabarabara hii ni mhimu sana
kwa wananchi wa mkoa wa Katavi kwa sababu halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ni
halmashauri ya kilimo tunatoa mchele mwingi sana kule asilimia 50 ya mavuno ya Mpunga,Alizeti
na Mazao mengine yanatoka huko barabahii ni uti wa Mgongo kwa uchumi wa mkoa
wetu’’-Mwananvua
Amebainisha kuwa pamoja na juhudi
zinazofanywa na serikali za kuhakikisha mkandarasi anatekeleza mradi huo kwa
kasi bado mwenendo wa mradi huo umekuwa unaenda kwa mwendo wa konokono.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi
Innocent Bashugwa amesema kuwa kutokana na uwepo wa taarifa za mkandarasi huyo
anaejenga Barabara ya Kibaoni Sitalike kuwa na kiwango kisicho lidhisha imemlazimu
kufika na kujionea hali hiyo ili kubaini tatizo lililopona hatua ambazo
tunaweza kuzichukua.
‘’Hata mimi kwa taarifa
nilizonazo barabara hii nimeona nifike mwenyewe nione kama ninaweza nikaleta
msukumo mpya wa utendaji, Barabara hii wamekuja viongozi mbalimbali akiwemo
Naibu waziri Kasekenya na viongozi wa Chama’’-Bashugwa
Bashugwa ameeleza kuwa katika
maeneo mengine ambayo mkandarasi huyo amekuwa akitekeleza miradi ya barabara kumekuwa
na kusukumana katika utekelezaji wa majukumu yake kwenye miradi hiyo.
Waziri huyo wa ujenzi
amemwakikishia Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Wananachi wa Mkoa wa Katavi kwa ujumla
kuwa suala hilo amelichukua na anakwenda kulifanyia kazi.
Ujenzi wa Babarabara ya Kibaoni
Sitalike yenye Urefu wa Kilomita 50 ilianza kujengwa Rasmi 23/6/2022 huku
matalajio ya kukamilika kwa Barabara hiyo ikiwa ni 22/6/2025.
Mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi 88,725,676,540
chini ya Mkandarasi China Railways Seventh Group Company limited.