Na walter Mguluchuma-Katavi
Wakala wa barabara Tanzania [TANROADS]Mkoa wakatavi wamefungua barabara inayo unganisha Mkoa wakatavi na Rukwa pamoja na hifadhi ya taifa ya Katavi iliokuwa imefungwa kwa muda wa siku 18 kutokana na mto katuma kujaa maji kwenye daraja la stalike.
Wakala wa barabara Tanzania [TANROADS]Mkoa wakatavi wamefungua barabara inayo unganisha Mkoa wakatavi na Rukwa pamoja na hifadhi ya taifa ya Katavi iliokuwa imefungwa kwa muda wa siku 18 kutokana na mto katuma kujaa maji kwenye daraja la stalike.
Meneja wa Tanroads Mwandisi Martin Mwakabende amesema wamefungua barabara hiyo kufuatia maji kuwa yamepungua na wameweza kufanya matengenezo kwenye maeneo yalio kuwa yameharibika na wamejiridhisha kabisa barabara hiyo muhimu kwa uchumi wa wanananchi wa wa mikoa ya Katavi na Rukwa nanchi jirani za Kongo Burundi na Rundwa inapitika kwa magari yote ya abiria na mizigo
Amebainisha kuwa barabara hiyo ilifungwa toka tarh8 mwezi uliopita kufuatia nvua kubwa zinazo endelea kunyesha hapa nchini hali iliopelekea kutokuwepo kwa usalama kwenye eneo la daraja hilo
Kwa watumiaji wa vyombo vya moto na abiria .
Mhandisi mwakabende ameeleza kuwa Tanroad mkoa wakatavi wananmshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kutuma fedha za dharura na kufanya matengenezo ya eneo hilo na maeneo mengine ya mkoa wa Katavi kufanyika kwa haraka sana .
Amefafanua kuwa kama Mkoa wamepokea kiasi cha zaidi ya shilingi Bilion 1.3 na anawashukuru wananchi kwa uvumilivu kwao wakati wa kipindi hicho ambacho eneo hilo lilikuwa halipitiki.
Mwakabende amesema wenzetu wa Tanapa wamepata changamoto kubwa kwakuwa eneo lao la makazi yako upande wapili na wanapohitaji huduma hulazimika kuvuka kwenye daraja hilo kwa hiyo iliwalazimu kwenye kipindi chote hicho ambacho barabarabara hiyo ilikuwa imefungwa kutembea zaidi ya kilometa 70 kwenda kutafuta huduma za mahitaji yao .
Wao kama mkoa na wizara ya ujenzi wamekisha peleka maombi rasimi kuomba Tanroads ifikilie namana ya kulijenga hilo daraja kwa ubora ambao utakao weza kuhimili maji katika vipindi vyote vya nvua maombi hayo wamekwisha yapeleka toka mwaka jana ambapo mtendaji mkuu wa Tanroad amekwisha yapeleka kwenye nwizara ya ujenzi .
Bitris Msuya mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Katavi amesema kuwa kujaaa maji kwenye daraja la mto huo kulisababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya eneo la hifadhi na maeneo ya makazi yanayo zunguka hifadhi na kupelekea hata idadi ya watalii wanao tembelea hifadhi kupungua .
Hivyo kukatika kwa mawasiliano iliwalizimu kuzunguka kwa kutembea umbali mrefu kwakupitia kizi mkoani Rukwa kupitia kibaoni kuja makao makuu ya mkoa wakatavi
Nawakati mwingine walikuwa wanalazimika kwenda kutafuta huduma zamahitaji yao katika mkoa wa Rukwa kutokana na juhudi na Tanroads Mkoa wakatavi ambao walifika toka changamoto ilipotokea nakuweza kuonyesha ushirikiano mkubwa kwakujali uhai wa watu na mali zao barabara hii wanaitegemea sana kwani ndio kiunganishi cha hifadhi ya Katavi na mikoa ya Rukwa Kigoma na Tabora.
Mwenyekiti wa kijiji cha stalike selemani Kabebi kuwa kulikuwepo na changamoto nyingi kwa wenzao wa Tanapa ambao huduma nyingi hutegemea kuzipata kutoka kwenye kijiji chake lakini walikuwa wakishindwa kufika na kulazimika kupita njia ndefu ya mzunguko kufuata mahitaji katika kijiji cha stalike
Ameiomba serikali kwakuwa sasahivi daraja hilo linapitika waangalie namna yakuliboresha zaidi kwa kuliinua juu ili liweze kupitika kwa usalama zaidi kwani hali kama hiyo iliwahi kutokea mwaka 1979