WANANCHI KATAVI WATAKIWA KULIPA KODI YA PANGO YA ARDHI KABLA YA KUCHUKULIWA HATUA
Na Walter Mguluchuma Katavi.
Kamishina msaidizi wa ardhi Mkoa wa Katavi Chedieli Mrutu ametoa siku 30 kwa wananchi wote wa Mkoa wa Katavi ambao hawajalipa kodi zao wahakikishe wanalipa kodi kabla ya siku 30 watakao shindwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani
Wito huo kwa wananchi wa mkoa wa Katavi ametoa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa waKatavi ofsini kwake kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuona umuhimu wa kulipa madeni yao wanayo daiwa kwa manufaa ya maendeleo ya nchi
Kamishina msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Katavi Daniel Mrutu akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake
Amesema waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi alisha toa agizo kuwa ifikapo june 30 wamamchi wote wanao daiwa kodi hiyo wawe wamelipa vinginevyo wasipo tekeleza agizo hilo watachukuliwa kwa mujibu wa sheria za Ardhi za hapa nchin
Amebainisha kuwa katika mkoa wa Katavi kuna wananchi wengi sana ambao hawajalipa kodi kwa mujibu wa sheria kodi ambayo inayolipiwa Ardhi ni ile ambayo Ardhi imepimwa na mwananchi amemilikishwa kodi hiyo hulipwa kila mwaka na nitofauti na kodi ya majengo amabayo wananachi wanalipwa kwa kupitia luku.
Mrutu amewataka wananchi wote wanao daiwa wafike kwenye halim,ashauli zote za Mkoa wakatavi ili waweze kilipia kodi zao kwa mujibu washeria na tayari wameisha toa ilani toka Tarehe 2mwezi huu kwa wamnanch 350 wanao daiwa natayari wameanza kupunguza madeni yao ingawa kasi yao ni ndogo katika kurejesha madeni .
Viongozi mbalimbali wakisikiliza taarifa iliotolewa na kamishina msaidizi wa Ardhi
kipindi hiki ambacho waziri amekiainisha na wananchi wafuate utaratibu huowao kama Mkoa
wamejipanga katika kipindi hiki cha mwezi mzima watatoa huduma
kuanzia asubuhi mpaka saa mbili usiku kwenye ofisi zao zote za wilaya na Mkoa .
Pia kuanzia may 14 watakwenda nyumbakwanyumba kwa ajili ya
kuwaelimisha wananchi ulipajiwakodi hiyo vilevile wizara imeandaa utaratibu wa
namna ya kulipia kwa kutumia njia ya simu na kodi hii inalipwa sio kwenye
majengo tu atakama mtu anamiliki kiwanja ambacho akijajengwa ilimradi tu kiwe
kimepimwa .
Mrutu anawasihi sana wananchi wa mkoa wa Katavi waweze
kulipia kodi hizo ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa hiyo watu walipe kodi kwahamasa kwani kodi
hizo hutumiwa na serikali kwa ajili ya kusaidia kwenye maendeleo mbalimbali kwa
wananchi ikiwemo uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara na afya