Na Mwandishi wetu
Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura uzinduzi wake unatarajia kufanyika Julai 1 mwaka huu Mkoani Kigoma na mgeni rasmi kwenye uzinduzi anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa .
Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura uzinduzi wake unatarajia kufanyika Julai 1 mwaka huu Mkoani Kigoma na mgeni rasmi kwenye uzinduzi anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa .
Akizungumza na Wandishi wa Habari Mjini Unguja leo Mei 15 Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Jaji ( Rufaa ) Jacobs Mwambegele amesema hadi kukamilika kwa ha kwa daftari la kudumu la wapiga kura linatarajia kuwa na wapiga kura 34,746,638.
Amebainisha kuwa kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 dafftari ilnatarajia kuwa na wapiga kura 34,746,638 kutoka 29,754, 699 ya mwaka 2020 ikiwa ni ongezeko la wapiga kura 5,586,433 sawa na asilimia 18.7 .
Amesema zoezi hilo litahusu wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi na watakao kuwa wametimiza umri huu ifikapouchaguzi Mkuu wa 2025 pa moja na wale watu ambao watakuwa wamepoteza sifa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi au sheria nyingine yoyote
Pia zoezi hilo litatoa furusa kwa wapiga kura walioandishwa awali na ambao wamehama kutoka Mkoa au Wilaya moja kwenda Wilaya nyingine waweze kuhamisha taarifa zao kutoka Kata au jimbo walioandikishwa awali na kutowa furusa kwa wapiga kura walioandikishwwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina...'' amesema Jaji Mwambegele .
Mwenyekiti huyo amesema kuwa zoezi hilo la uboreshaji wa daftari litahusisha pia kutowa kadi mpya kwa waluiopoteza au kadi za kuharibika na kuondoa wapiga kura walipopoteza sifa za kuwemo kwenye daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuukana uraia wa Tanzania na kifo .
Kwa upande wa Zanzibar uboreshaji wa daftari utamuhusu mtu yeyote ambae aliyeko Zanzibar ambae hana sifa za kuandikishwa na tume ya uchaguzi ya Zanzibar lakini anasifa ya kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ...''a mesema Jaji Mwambagele
Amesema tume imefanya ununuzi wa vifaa vya uandikishaji ikiwepo ununuzi wa BVR Kits 6 ,000 zinazotumia vishikwambi kuchukua taarifa wapiga kura ikiwemo picha, saini na alama za vidole .
Tofauti na mashine za BVR zilizotumika katika uboreshaji wa mwaka 2015 na 2020 zilizokuwa na uzito wa kilo 35 BVR Kits za awamu hii ni nyepesi zenye uzito wa kilo 18 ambazo zitaweza kubebeka kiurahisi ...''amesema Jaji Mwambegele .
Amesema , Tume imeanzisha mfumo uboreshaji kwa njia ya mtandao uitwao Online Voters Registration System(OVRS) ambao utamwezesha mpiga kura aliyemo kwenye daftari kuanzisha mchakato wa awali wa kuboresha taarifa zake kwa njia ya Mtandao kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta .
Baada ya kukamilisha mchakato kwa njia ya mtandao mpiga kura atalazimika kufika kituo cha kuandikisha wapiga kura ili kukamilisha mchakato na kupatiwa kadi yake ya mpiga kura... 'amesema Jaji.